Habari Ndiyo Hiyoooo..


T

TAIKUBWA

Senior Member
Joined
Jan 20, 2008
Messages
120
Likes
1
Points
0
T

TAIKUBWA

Senior Member
Joined Jan 20, 2008
120 1 0
> Jumanne Mei 06, 2008 Habari za Kitaifa Habari zaidi! Aliyekutwa na kichwa cha mtoto kortini kwa mauaji Veronica Mheta na Emil SimonDaily News; Tuesday,May 06, 2008 @00:03 Habari nyingine Ajali zaua watu wawili DarPonda matatani tenaAmuua mkewe kwa kumchinja shingoMchuchuma, Liganga kupata wawekezaji karibuniHujuma kwa miundombinu ya Tanesco yakithiriSingida walia wilaya, majimbo yagawanyweAliyekutwa na kichwa cha mtoto kortini kwa mauajiPinda azungumzia mafanikio katika elimuDC Kinondoni awaonya madiwaniNyuki wavuruga uzinduzi katika ziara ya Kikwete KIJANA aliyeishangaza jamii kwa kula nyama ya kichwa cha mtu hadharani, Ramadhani Mussa (18), jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akituhumiwa kwa mauaji. Mussa na mama yake Hadija Seleman (38), walifikishwa mahakamani hapo na hawakutakiwa kujibu kitu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikilizwa kesi hiyo. Wakati Mussa na Hadija wakifikishwa mahakamani hapo, umati wa watu ulikusanyika mahakamani hapo kuwaona washitakiwa hao ambao wanatuhumiwa kumuua mtoto Salome Yohana (3). Umati huo ulikuwa na shauku ya kuwaona wahusika hao, hali iliyosababisha kukosekana kwa hewa ya kutosha katika chumba cha mahakama. Ilipotimu saa 5:00 asubuhi, Mussa pamoja na mama yake, walifikishwa mahakamani hapo kwa gari ya Toyota Landrover Defender wakiwa chini ya ulinzi mkali kutokana na wingi wa watu waliokuwapo mahakamani hapo. Akisoma mashitaka, Mwendesha Mashitaka, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Charles Kenyella alidai Aprili 25, mwaka huu katika eneo la Segerea kwa Bibi wilayani Ilala, washitakiwa hao walimuua mtoto Salome Yohana (3). Kenyella alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo aliomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine. Baada ya kusomewa shitaka hilo, mama wa mtoto huyo alijibu kuwa shitaka linalowakabili si la kweli, hali iliyoulazimu upande wa mashitaka kurudia upya kuwasomea shitaka hilo. Naye Hakimu wa mahakama hiyo, Ephemia Mingi aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 19, mwaka huu. Mtoto Salome alitenganishwa kichwa na kiwiliwili Ijumaa ya Aprili 25, mwaka huu, huko Tabata Segerea kwa Bibi ambako alipotea siku hiyo jioni akiwa amekwenda pamoja na wazazi wake kumsalimia shangazi yake. Kichwa chake kilikutwa katika himaya ya Mussa akiwa eneo la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kikiwa kwenye mfuko wa Rambo, Jumamosi ya Aprili 26, mwaka huu na kuzua tafrani na kusababisha gumzo kubwa katika Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake. Mtoto Salome alizikwa Aprili 29, mwaka huu katika makaburi ya Tabata Segerea. Wakati huo huo, kesi ya kuwajeruhi na kuwamwagia tindikali waandishi wa magazeti ya MwanaHalisi na Mseto haikusikilizwa jana kutokana na sababu za usalama. Kenyella aliomba kuahirishwa kwa kesi hiyo kutokana na kuendesha nyingine ya mauaji ya mtoto Salome Yohana (3) ambayo ilikuwa inahitaji ulinzi. Naye Hakimu Addy Lyamuya aliahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea kusikilizwa.
 
Think Global RC

Think Global RC

Member
Joined
Mar 5, 2008
Messages
24
Likes
0
Points
0
Think Global RC

Think Global RC

Member
Joined Mar 5, 2008
24 0 0
mkuu atleast uwe unafanya editing ili wana jf waweze kuvutika kusoma.
invisible vipi mzee.
 
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,864
Likes
8,686
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,864 8,686 280
ahsante mkuu ameipata hiyo atakuwa...,,tunashindwa kusoma kabisa.although inaeleweka kidogo
 
L

Lizy

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
413
Likes
285
Points
80
L

Lizy

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2008
413 285 80
TAIKUBWA Asante kutujulisha.

Inasikitisha sana. Pole kwa wafiwa, Mwenyezi Mungu amlaze Malaika wake (Salome) kwa amani.

Kesi imefika mahakamani (mbele ya haki) chini ya Mbingu. Bila shaka haki itatendeka kwa pande zote mbili (upande wa mashtakaa upande wa utetezi).

I wish I was a lawyer, (esp Criminal lawyer), labda ningeweza kujua mengi kuhusu sheria za makosa ya jinai ikiwemo ya Mauaji.

Well, upande wa mashtaka wameweza kuestablish kesi ya Murder kwa kumkamata mtoto na kichwa cha Marehemu Salome, 2nd, Mtuhumiwa amekiri (inavyosemekana) kwamba alifanya mauaji hayo kwa Imani zake za kishirikina, Uchunguzi wa Daktari (Postmoterm) sijajua inasemaje.

Najaribu kuangalia kwa nini huyu kijana alifanya unyama huu (MAUAJI)sipati jibu, Je ni hizo imani za kishirikina? (sheria ipo kimya), Self defence? (against what?,BIG NO), Provocation that caused sudden and temporaly loss of self-control? (Kwa mtoto wa miaka mitatu? not i doubt), Addiction/intoxication (kwamba kijana ni alcoholic, drug addict or glue-sniffer), ama Insanity? Jibu sina.

Mwenyezi Mungu ailaze pema roho ya Mtoto Salome.
 
Kilbark

Kilbark

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2008
Messages
568
Likes
49
Points
45
Kilbark

Kilbark

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2008
568 49 45
Toyota Landrover Defender ni ipi kati ya hizo?
 
K

Kipanga

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Messages
679
Likes
12
Points
0
K

Kipanga

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2008
679 12 0
Kwii!! kwi! kwi! kilbark acha fujo!! Kweli Toyota landrover defender hii mpya.. Tutacheki na CMC na Toyota Tanzania it might be new product done jointly by the two coys!! Mchana mwema
 

Forum statistics

Threads 1,236,606
Members 475,218
Posts 29,263,798