Habari na Picha Nape, Mwigulu ziarani Sumbawanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari na Picha Nape, Mwigulu ziarani Sumbawanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  NA MWANDISHI WETU, SUMBAWANGA
  [​IMG]


  KATIBU wa NEC ya CCM, Itikati na Uenezi Nape Nnayue na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Nchemba Mwigulu, waliuteka mji wa Sumbawanga, baada ya mamia ya wananchi kufurika kwenye mkutano wa hadhara katika uliofanyika katika Uwanja wa Mndela mjini hapa.

  Kimbunga cha mkutano huo, kiliwazoa wananchi 51 waliokuwa wanachama wa CHADEMA ambao kutokana na furaha yao, waliamua kukabidhi kadi zao kwa Nape na kutangaza kujiunga na CCM. "Tunaachana na ujinga wao", alisema mmoja wa wananchi hao, Geofrey Mwanakatwe wakati akikabidhi kadi yake ya Chadema kwa Nape.

  Hadi saa tisa alasiri uwanja huo ukiwa umefurika wananchi, msafara wa Nape na Mwigulu, uliigia na kusababisha uwanja huo kulipuka kwa nderemo na vifijo kuwashangilia.

  Mwigulu ndiye alikuwa wa kwanza kuhutubia kwenye mkutano huo nchi baada ya kukaribishwa jukwaani na Nape.

  Akionyesha umahiri wake katika masuala ya uchumi, Mwigulu alisema, wanasiasa wa vyama vya upinzani kama CHADEMA ambao wamekuwa wakihamasisha wananchi kukataa kuchangia miradi ya maendeleo ni wanasiasa hao ni tatizo kwa taifa.

  Mwinguli alisema, anazo taarifa kwamba viongozi hao wamekuwa waki wakiwaambia wananchi kwamba hawana sababu ya kuchangia kwenye miradi hata inayoanzishwa katika maeneo yao kwa kuwadanganya kuwa jukumu lote ni la serikali.

  Aliwataka wananchi kutowasikiliza wnasiasa hao akisema wanachofanya wanaviza akili za wananchi, kwa kuwa hakuna nchi inayoweza kupata maendeleo bila maendeleo hayo kuhangiwa na wananchi.

  "Wananchi kataeni mawazo ya aina hii, kwanza ukiona mtu anakukataza kuchangia maendeleo ujue huyo anajihami usimuombe kukuchangia na wewe, achaneni nao kabisa", alisema Mugulu.

  Baada ya hotuba ya Mwigulu, kipaza sauti kilihamaia kwa Nape, ambaye alitoa hotuba yenye kuchoma hisia za watu na kusababisha baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo hasa vijana, kujipiga vifua mfano wa muumini aliyeingiwa na roho mtakatifu kwenye mkutano wa mahubiri ya kidini.

  Mbali na uwezo wake wa kugusa hisia za watu wakati akihutubia, maneno yake yaliwagusa wananchi, hasa pale alipofafanua kwa kina na kwa umahiri mkubwa maana ya CCM kijivua gamba na maana ya kujivua gamba kwenyewe ni nini.
  Alisema, kujivua gamba kwa CCM hakumaamishi kwamba Chama kimebadili tabia yake iliyoasisiwa nayo na viongozi walioianzisha akiwemo Baba wa Taiafa, Hayati Mwalimu Nyerere, ila imebaki pale pale katika msingi yake na wala haikubaki na uzembe na ufisadi ulioonyeshwa na badhi ya viongozi wake kabla ya mabadiliko hayo.

  "Tulichofanya ni kama afanyavyo nyoka. Baada ya kupatwa na dhoruba kwa muda mrefu katika maisha yake huishiwa uwezo wa mambo mengi, ikiwemo kukimbia, kunusa na hata kupungua ukali wa sumu yake na kwa uwezo wa Mungu hujibua gaamba na kubaki na ngozi mpya ambayo sasa humfanya kuwa na uwezo wake wa awali au uwezo huo kuongezeka", alisema Nape na kuongeza:

  "Hivyo ndivyo CCM nayo ilivyofanya. Baada ya kuongoza kwa muda mrefu tukaona Chama kinaanza kupotoka katika misingi yake. Tukasema hizi ni dalili za kuchakaa gamba, tulivue, tukakubaliana kujivua na kufanya uamuzi mgumu ambao chama kingine kisicho na misingi bora hakiwezi".

  Alisema, kutokana na hatua hiyo sasa CCM imepata ngozi mpya, na tabia zake ambazo ni itikadi na malengo yake ya kuanzishwa sasa yameongezeka ili kuleta upendo ulipokuwa umeanza kujaa kupotea,kuleta amani pale ilipokuwa imeanza kutetereka, kuleta matumaini pale yalipokuwa yameanza na kuongeza uwezo wa sumu ya kuitemea serikali katika kuisimamia kutekeleza ilani ya Chama.
  Nape aliwataka wananchi hasa vijana waliokuwa wameanza kukata tamaa, kurejesha imani zao kwa CCM, kwa kuwa ndicho chama chenye uhakika wa kusimamia maendeleo na amani na utulivu.

  Alikemea viongozi wa CHADEMA ambao wamekuwa wakisema kwamba nchi haitatawalika, akisema kwamba viongozi hao wanatamba kusema maneno hayo kwa sababu hawajui uchungu wa nchi ilivyohangaika kujenga mshikamano wa kitaifa na amani na utulivu uliopo.

  Nape alirejea kauli yake kwamba, kauli hiyo ni ndoto za mchana na kuwatukana Watanzania ambao wanafahamu kuwa wameipa CCM ridhaa ya kuongoza ili nchi itawalike.

  Katika ziara hiyo, Wajumbe hao wa sektretarieti wanatarajia kufanya mikutano kadhaa ya hadhara mkoani Rukwa katika maeneo ya Namanyere, Kabwe, Maji moto, Usevya, Kakese na Mpanda mjini.

  [​IMG]
  KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga, jana, siku ya kwanza ya ziara yake na Mjumbe wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, mkoani Rukwa
  [​IMG]
  Waliokuwa wanachama wa CHADEMA wakimpa kadi zao, Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, katika mkutano wa hadhara uliofanyika, jana, katika Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga. Zaidi ya wanachama 50 wa CHADEMA walirudisha kadi zao na kujiunga na CCM
  [​IMG]
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa CCM, Theresia Mwanakatwe, katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi, jana katika mji mdogo wa Laela, wilayani mkoani Rukwa. Jumla ya wanachama wapya 82, waliojiunga na CCM walikabidhiwa kadi. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Nchemba Mwigulu.
  [​IMG]
  KATIBU wa NEC, Uchumi na Fedha CCM, Nchemba Mwigulu akikabidhi kwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kadi za wanachama kutoka vyama vya upinzani ambazo wanachama wa vyama hivyo walimkabidhi baada ya kutangaza kuhama vyama vyao na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana, katika Uwanja wa Mandela, mjini Sumbawanga. Mbali na CUF na NCCR-Mageuzi, Chadema pekee walihama 51.
  [​IMG]
  MKAZI wa kijiji cha Ntendo, Zakaria Lusambo akimshukuru, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye baada ya kukabidhiwa baiskeli ya miguu mitatu pamoja na wenzake wanne wenye ulemavu wa miguu, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jana, kwenye Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga. Baiskeli hizo zimetolewa na Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hilary (kushoto)
  [​IMG]
  KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha CCM, Nchemba Mwigulu wakipatiwa maelezo na mmoja wa wasimamizi wa ujezi wa barabara yenye urefu wa kilometa 64 kati ya Ikana hadi Laela mkoani Rukwa, walipokagua mradi wa ujenzi wa barabara hiyo, jana wakiwa njiani kwenda mjini Sumbawanga. eneo hilo ni kati ya Kilometa 190 Kutoka Ikana hadi Sumbawanga mjini ambazo zimo katika ujenzi ili kuwa katika kiwango la lami
   
 2. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Nape, kwa spidi hiyo naona ni nzuri sana katika kukijenga Chama.

  Ushauri wangu ni kwamba musitumie muda mwingi kuwaponda wapinzani katika ziara hizo kwani udhaifu ndani ya chama mulishautangaza kwa hiyo kila mtu anajua kwamba kuna watendaji wabovu. Fuatilieni usimamizi wa shughuli za kimaendeleo kama sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama. Waambieni wafanyakazi wazembe na mafisadi siyo sehemu yao katika chama kwa wakati huu. Kisha watu waone matokeo ya kazi zenu, ninakuhakikishia utafanikiwa.

  Kila la kheri.
   
 3. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mojawapo ya kazi za chama cha upinzani ni kuonyesha wananchi makosa ambayo yanafanywa na chama tawala. Hivyo basi Chadema hawajakosea kuonyesha mapungufu ya Ccm. Alichotakiwa kufanya ni kueleza ni jinsi gani ccm itaweza kukabiliana na mapungufu hayo ambayo yameonyeshwa na chama cha upinzani.

  BTW, mbona hukutuwekea picha zote?
   
 4. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Maelfu! nadhani aliyeandika hajui hesabu!
   
 5. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nawashauri viongozi wa Chadema Sumbawanga wafuatilie na kuona ni kwa nini, na kwa jinsi gani kadi hizo za uanachama wa Chadema zilirudishwa!
   
 6. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Hizi kadi za CHADEMA mbona mpyampya? Kwa udongo wa Sombawanga kadi safi hivi? Mhh

  [​IMG]
   
 7. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wewe unafikiria wananchi wa kawaida Tanzania ni wanasiasa? NO. Wengi ni mashabiki wa siasa ndo maana Dr. akiitisha maandamano wanakwenda kwa wiki bila kujali anakadi gani. Kesho akiona huku kuna mwelekeo atachukua kadi. Kwa kifupi watanzania wengi si wafurukutwa na wakereketwa wa vyama bali mashabiki tu.
   
 8. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Asante sana. Rejea post yangu hapo juu. Unajua mmoja wa makada wa ccm juzijuzi alitamka kwenye vyombo vya habari kuwa, "Unajua siku hizi watu tunaishi kimjini-mjini"!
   
 9. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Tumbo kubwa? Njau tu inamsubua. Halafu ni kwanini mara zote wanasema wamevuna wanachama wa chedema? i think there is wrong somewhere!
   
 10. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  HEee Hee e ni watoto ndio walio[​IMG]udhuria
   
 11. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Wakati kwenye rundo la hizo''kadi'' naona ya NCCR ipo

  [​IMG]
   
 12. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Nape anakusanya watoto anadai ni wanachama wa CCM ni haibu kwa CCM, jamani! !jamani!! Nape anakiua chama
   
 13. F

  FUSO JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,339
  Trophy Points: 280
  Hizi watakuwa wameprint - si original, atupe Serial numbers to validate!!

  Hivi NAPE hana updates kwamba magamba 3 yamekataa kuvulika? namshauri arudi dar makau makuu fasta kabla mambo hayajaharibika kabisa - Teh teh teh

  Pia akumbuke naye ni gamba sababu yumo kwenye tuhuma mpya za uasisi wa CCJ - kazi bado pevu.
   
 14. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Masikini wansumbawanga mtajuta kuendelea kung'ang'ania matatizo.:fish:
   
 15. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  walichelewa ccm kuwapa kina nape nafasi kam hizi
   
 16. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nape jana kaiua sana Chadema! Kuna ulazima wa Chadema kurudi kusini tena! Kaipiga sana na kuwambia Chadema ni genge la wahuni ndio maana hawajari hata Nchi isipo tawalika! Amesema huyo alie kataa mshahara mkubwa Bungeni leo amelazimisha au pate kwenye chama masikini! Anasema dr slaa ni padre na ana fuata kanuni ya msifuate matendo yangu ila fuateni maneno yangu!
   
 17. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,164
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Mbona naona watoto ndio wengi zaidi?

  Mbona kijani ni nyingi sana, japo sijaona Malori kwa mbali!!!

  Mbona kadi zinazorudishwa ni za Chadema tuu, hawavuni kutoka vyama vingine???

  Mi nauliza tu.
   
 18. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nape ni mhuuni anakusanya watoto wa shule anadai ni wanachama wa Upinzani,Jamani!! Jamani chonde ! Chonde Nape anahua chama
   
 19. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #19
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huku ni kuua CHADEMA au kujiua mwenyewe?

  [​IMG]
   
 20. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #20
  Jun 1, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Jamani na hii picha ya wale wanafunzi hamkuiona?
  [​IMG]
   
Loading...