habari na picha: mapadri waeleza walivyopigwa mapanga na kujeruiwa


Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
13,097
Points
1,500
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
13,097 1,500

Na Eliasa Ally, Iringa
MAPADRI waliovamiwa usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita na majambazi sita waliokuwa na silaha katika Parokia ya Isimani, jimbo la Isimani Halmashauri ya Iringa Vijijini kwa nyakati tofauti wamefunguka kuwa ni Mungu tu aliyewaokoa.
Paroko Angelo Burgio akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa.
Baada ya kuvamiwa, Paroko Angelo Burgio (60) alipigwa risasi kwenye ubavu wa kushoto, Padri msaidizi, Herman Myala (36) alicharangwa panga kichwani ambapo majambazi hao walifanikiwa kupora fedha za kanisa hilo shilingi milioni 3.5 na dola za Kimarekani 100 na kutoweka.
Katika mahojiano na gazeti hili, Padri Angelo ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa wodi namba 4 alisema: “Majambazi hao walivunja mlango wa geti la kuingilia mapadri baada ya umeme wa jenereta kuzimwa na kuingia ndani.
Mwandishi: Je, walianza kukuvamia wewe au msaidizi wako?
Paroko: Walianza kumkata kwa panga Padri Myala huku wakimtaka awaoneshe chumba ambacho nilikuwa nimelala, baada ya kuona anaendelea kuumizwa aliwaonesha chumba changu.
Mwandishi: Wakati mwenzako anashambuliwa wewe ulichukuwa uamuzi gani?
Paroko: Niliposikia kelele nilitaka kukimbia ndipo walinipiga risasi ubavuni nikaanguka.
Mwandishi: Baada ya hapo kiliendelea nini?​
Padri msaidizi, Herman Myala akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa baada ya kujeruhiwa.
Paroko: Majambazi hao walijua nimekufa, walikwenda kuchukua fedha na kuondoka baada ya kuwaona wananchi wanakuja kufuatia kusikia mlio wa bunduki na mayowe yetu ya kuomba msaada.
Mwandishi: Je, ukiwaona leo unaweza kuwatambua?
Paroko: Hapana, majambazi hao walivaa mavazi ya kufunika uso na mmoja wao alikuwa na bunduki na wengine walikuwa na mapanga.Tukio hili ni baya kupindukia, lengo lao lilikuwa ni kutuua.
Diwani wa Kata ya Kihologota Tarafa ya Isimani, Costantino Kihwele alisema kuwa Padri Angelo amekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa Isimani ambapo kwa sasa anafadhili mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 4 pia anawalipia ada baadhi ya watoto yatima wanaosoma.​
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, Wiliam Lukuvi (katikati) akimjulia hali Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani mkoani Iringa, Angelo Burgio wakati alipomtembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda alipohojiwa alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema watuhumiwa wanne kati ya sita wamekamatwa.
Aliwataja watu hao kuwa ni Joseph Ngwale (30), Erasto Ngwale (38), Gaitan Kitwange na Anitha Mwinuka.
Aliongeza kuwa, wahalifu hao wanahusishwa na tukio lingine la kuvamia Kanisa la Katoliki Kihesa na kupora shilingi 500,000.​
 
N

NIMEKIMBIA CCM

Senior Member
Joined
Oct 4, 2011
Messages
193
Points
0
Age
28
N

NIMEKIMBIA CCM

Senior Member
Joined Oct 4, 2011
193 0
mtetezi wetu yu hai
 
Facilitator

Facilitator

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Messages
2,289
Points
2,000
Facilitator

Facilitator

JF-Expert Member
Joined Oct 30, 2010
2,289 2,000
Poleni watumishi. Kazi ya Bwana nayo ina vichomi vyake.
 
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,230
Points
1,500
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,230 1,500
Watesi hao wameshindwa!

"Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini Bwana atamfariji na kumtumainisha"!

Baba wasamehe wezi hao, maana hawajui watendalo.
 
marejesho

marejesho

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Messages
6,638
Points
2,000
marejesho

marejesho

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2011
6,638 2,000
Mungu peke yake ndiye mlipaji kisasi!!
 
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
12,184
Points
2,000
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
12,184 2,000
Poleni sana makasisi wetu, Mungu awape afya tele na faraja muendelee kumtumikia Mungu bila kukoma. Waliohusika watalipa hapa hapa duniani tukiwa hai.
 

Forum statistics

Threads 1,284,750
Members 494,236
Posts 30,838,738
Top