Habari na Matukio muhimu kuanzia Jumatatu - Ieo hii

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
01. WAHAMIAJI HARAMU: Zaidi ya wahamiaji haramu 1170 wamefungwa nchini, zaidi ya 200 wamo gereza la Luanda Mbeya, Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama yathibitisha.
===

02. SANAMU YA MANDELA YAONYESHWA: Rais Jacob Zuma leo ameionyesha kwa mara ya kwanza sanamu kubwa ya Nelson Mandela mjini Pretoria, ina urefu wa mita 9 (futi 30).

03. BASI LAPATA AJALI KAHAMA: Watu 31 wamejeruhiwa baada ya Basi la Bukoba Express kutoka Dar-Bukoba kupinduka wilayani Kahama asubuhi hii, OCD Kahama athibitisha.

04. BOAS ATUPIWA VIRAGO: Klabu ya Tottenham imemtimua Meneja wake Villas-Boas kufuatia kipigo cha goli 5-0 kutoka kwa Liverpool.

05. UEFA 16 BORA: Draw imekamilika, timu za Uingereza kazi ipo: Man City vs Barcelona, Man Utd vs Olympiakos, Chelsea vs Galatasaray, na Arsenal vs Bayern Munich.

06. DK LIMBU ANAWA MIKONO: Mbunge wa Magu kwa vipindi vitatu DK Festus Limbu ametangaza mbele ya waandishi wa habari kuwa hatagombea tena ubunge uchaguzi 2015.

07. MAUAJI YA MABINA: Watu 7 wamekamatwa kufuatia mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina, polisi wasema uchunguzi unaendelea.


08. LIGI YA MABINGWA AFRIKA: Ratiba ya mechi za raundi ya awali yatoka, Yanga kuanza na Komorozine ya Comorro, KMKA ya Zanzibar kuanza na Dedebit ya Ethiopia.

09. HISTORIA YAANDIKWA: UN inatafuta 6.5bn kufanikisha utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa raia 22.4m wa Syria wanaokadiriwa na utafiti kuhitaji msaada mwaka 2014.

10. MAUAJI NIGERIA: Waasi wa Boko Haram wameua zaidi ya watu 1200 Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo tangu hali ya hatari ilipotangazwa Mei 2013, UN imesema.

11. MGOMO MADAKTARI KENYA: Mwanamke 1, watoto 2 wamekufa eneo la Tana River, mgomo ukiingia wiki ya 2. Mwingine anusurika baada ya kuwahishwa hospitali ya misheni.

12. HALI TETE SUDAN: Risasi, makombora yarindima mjini Juba, ikiwa ni baada ya serikali ya Sudan Kusini kudai imezuia jaribio la kuipindua.

13. WAUZA FEDHA WAANIKWA: Ikiwa Bungeni Dodoma, Kamati ya Uchumi yadai maduka ya kubadili fedha za kigeni hutumika kusafirisha pesa haramu nje ya nchi.

14. AJALI SINGIDA: Gari dogo aina ya Land Rover likitokea Kijiji cha Dolomoni, Iramba limesombwa na maji Mto Nzalala, 5 wahofiwa kufa, 11 waokolewa.

15. DODOMA - MIUNDOMBINU: Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeitaka serikali iruhusu uwekezaji binafsi ili kuboresha barabara, reli, bandari kupitia Matokeo Makubwa Sasa.

16. UTATA TAZARA: Kamati ya Miundombinu yaliambia Bunge kuwa Zambia haijali tena mapatano yake na Tanzania kuhusu reli ya TAZARA, yataka suala hili litatuliwe.

17. UMEME BADO KERO: Kamati ya Nishati yalalamikia ukata unaokwaza jitihada za REA za kupeleka umeme vijijini. REA haina mamlaka kamili, Bunge laambiwa Dodoma.

18. 500 WAFA JUBA: Watu 500 wamekufa katika siku 2 za vurugu kufuatia jaribio la mapinduzi Sudan Kusini, yasema UN. Yaonya huenda ikawa vita ya kimbari.

19. BASI LAUNGUA: Watu 50 wamenusurika kufa baada ya basi la Taqwa kuwaka moto Ngara, Kagera, polisi wathibitisha. Lilikuwa likitoka Dar kwenda Burundi.

20. MHANGA WA BOMU: Afya ya mtoto Wema Kigenda (12) aliyeumizwa na bomu Ngara Okt. yazidi kudorora, vidonda vyaozea hospitali ya wilaya. Aomba serikali imsaidie.

21. NDEGE YAKWAMA ARUSHA: Ethiopian Airlines ilitua Arusha kwa dharura, kisha ikashindwa kupaa shauri ya barabara (runway) fupi. Abiria 213 wakwama.

Ndege ya Ethiopian Airlines iliyokwama kwenye tope Arusha ilipaswa kutua Moshi, ikashindwa kisa ndege nyingine mbovu imeziba njia uwanja wa KIA.

22. MAAFA MBEYA: Mvua kali yaleta maafa wilayani Mbarali, hivi sasa raia wanahaha baada ya nyumba 73 kuharibiwa vibaya. Wanadai hawajapata msaada.

23. MASHITAKA YA MORSI: Rais wa Misri aliyepinduliwa, Mohamed Morsi sasa atashitakiwa kwa makosa ya uhaini na kushirikiana na kundi la Hamas la Palestina.

24. JELA MIAKA 120: Mahakama wilayani Nzega, Tabora imewahukumu watu 4 kifungo cha jumla ya miaka 120 baada ya kutiwa hatiani kwa unyang'anyi wa kutumia silaha.

25. BALAA LA TINDIKALI: 5 waburuzwa kortini, 17 wahojiwa Bara na Z'bar kwa matukio 11 yaliyotokea. Serikali yaliambia bunge, upo udhaifu kukabili matukio hayo.

26. VIWANGO FIFA: Tanzania imepaa toka nafasi ya 124 hadi 120 katika viwango duniani vilivyotolewa punde. Spain, Germany na Argentina tatu bora, Uingereza ya 13.

27. MAUAJI PADRE MUSHI: Mahakama Kuu Z'bar yamuachia kwa dhamana Omar Mussa Makame anayetuhumiwa kumuua E. Mushi. Wadhamini 2 wasaini dhamana ya laki 5 kila mmoja.

28. UVAMIZI SUDAN: Vifo zaidi vyahofiwa Sudan Kusini baada ya kambi ya Umoja wa Mataifa kuvamiwa usiku. Hadi sasa, kambi za UN Juba zishapokea wakimbizi 20,000.

29. NGONO MARUFUKU: Bunge Uganda lapitisha sheria inayokataza vipindi, uandishi, mavazi na muonekano unaochochea ngono. Museveni akiisaini, sketi fupi marufuku.

30. MAAFA LONDON: Sehemu ya paa katika jumba la maonyesho la Apollo jijini London imeanguka maonesho yakiendelea, idadi ya watu waliokuwepo ndani haijafahamika.

Zaidi ya watu 700 walikuwepo kwenye jumba la maonyesho la Apollo jijini London lililoanguka sehemu ya paa, watu 80 wajeruhiwa, 7 wako mahututi.

31. MAUAJI UFILIPINO:Watu wenye silaha wamewaua 4 akiwemo meya, mke wake na mtoto katika shambulio lililotokea hivi punde uwanja wa ndege wa Manila, mamlaka yasema.

32. DODOMA - OPERESHENI TOKOMEZA: Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli anawasilisha ripoti ya zoezi hilo bungeni muda huu, yabaini madudu.
KAMATI YA LEMBELI: Yabaini kushamiri kwa rushwa, udhalilishaji, mateso na upotevu wa mali na fedha, akisoma ripoti hiyo asema haki za binadamu zilikiukwa.


KAMATI YA LEMBELI: Yashauri kuwajibishwa wasaidizi wa waziri wa Maliasili, mkurugenzi wanyamapori, maofisa vyombo vya ulinzi, usalama. Waathirika kulipwa fidia.


PINDA AANDAMWA: Atakiwa kujiuzulu kutokana na vifo na mateso yaliyoainishwa na Kamati ya Lembeli. Mh Zitto ashauri asipofuata ushauri huo, bunge limwajibishe.

MOTO BUNGENI: Wabunge waijadili ripoti ya Lembeli, washauri majina ya mawaziri, wabunge na vyama vilivyohujumu operesheni hiyo yafichuliwe na kuchukuliwa hatua.


KAGASHEKI LAWAMANI: Wabunge walia na Waziri K. Kagasheki, wasema matatizo ya Operesheni Tokomeza aliyajua akakaa kimya, wataka ajiengue mwenyewe.

WABUNGE WASUTWA: Serikali, wabunge wote wana makosa kwa kushindwa kurekebisha madudu yaliyojitokeza Operesheni Tokomeza, asema Anne Kilango.


SHUTUMA ZAIDI BUNGENI: Tundu Lissu (MP) ahoji uhalali wa kutumia jeshi, mahakama kuminya haki za raia wakati wa Op. Tokomeza hivi punde, asema inakiuka katiba.

33. AJALI YAUA TABORA: Watu 4 wamekufa, 5 wamejeruhiwa vibaya eneo la Mnadani baada ya lori walilokuwa wanasafiria kupinduka, mamlaka zimethibitisha.

34. MAUAJI MBEYA: Watoto 2 (miaka 6 na 17) wauawa kikatili nyumbani kwa diwani wa Tunduma, Kaimu RPC wa Mbeya B. Masaki athibitisha. Miili yatelekezwa sebuleni.

35. ....







mcl
 
Back
Top Bottom