Habari mbaya: Uwanja wa Uhuru Dar, Watu 45 wapoteza maisha kutoka na msongamano

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Salaam Wakuu,

Kuna habari mbaya ya watu wengi kufariki wakati wakiaga mwili wa hayati Magufuli.

Inadaiwa baadhi ya watu wamepelekwa Hospitali ya Temeke wengine wakiwa wamepoteza maisha na wengine kuzimia.

Nmempigia Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke kumuuliza juu ya vifo hivi, baada ya kujitambulisha tu, akanikatia simu. Hivyo nmeshindwa kujua Idadi kamili.

Hapa chini ni baadhi ya watu waliotajwa kupoteza maisha kenye msongamano Uwanja wa Uhuru Temeke Dar es Salaam.

TANZIA!
TUNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MWALIMU JANE NGONDE (MWALIMU MKUU WA S.M MGEULE) KILICHOTOKEA LEO MCHANA UWANJA WA BENJAMIN MKAPA ALIPOKUWA AKISHIRIKI KUTOA SALAMU ZA MWISHO. TARATIBU ZA MAZISHI ZINAFANYIKA NA TUTAENDELEA KUJULISHANA. AIDHA TUNAITAARIFU KAMATI YA MAAFA- UVEMI KUENDELEA NA TARATIBU ZETU. R. I.P

Nyingine:

TANZIA: Mboka Nsobi Minga amefiwa na mkewe Lidia Shomari Minga ambaye leo tarehe 21/3/2021 asubuhi akiwa mzima wa afya alikwenda uwanjani kuaga mwili wa Hayati John Joseph Pombe Makufuli. Kifo chake kimesababishwa na kukanyagwa na umati wa watu uwanjani hapo. Mwili wake umehifadhiwa hospitali ya Temeke. Msiba upo Kilwa road Barracks.

IMG-20210321-WA0002.jpg

Lidia Shomari

Mashuhuda wengine wamesema;

"Nilikuwa temeke hosp ninamgonjwa mama yangu mdogo, ambulance zilizoleta maiti pale ni zaid ya watu 40 aisee, kuna mama mjamzito kafa na watoto wake 2"

"Yan nilikuwa natetemeka tu ambulance zinaleta watu watatu watatu wengine mahututi wengine wamekufa Yan kweli magufuli tulimpenda Sana"

"Jamani pale Taifa umetokea mkanyagano wakati wa kuaga mwili wa JPM, watu wengi wamepoteza maisha..including two of my relatives.

Im worried hata kule Dodoma the crowd is not well managed, tutapoteza wengi."

"Sijui tuna kwama wapi.Kuna jirani yangu hapa ndugu yake kafiwa na mke na watoto wawili.Watoto wa nini kwenye crowd kama ile?🤷🏾‍♂️🙆🏾‍♂️🙆🏾‍♂️"

"Nina Rafiki yangu kafiwa na Mke na watoto wake 2 huko uwanjani"
susan.JPG



PIA SOMA>>Familia moja yapoteza watu 5 waliokufa uwanja Uhuru, kamanda Mambosasa kutoa taarifa Jumanne!

 
Hao ni physical victims wa msongamano. Sijui viral victims wa msongamano itakuwaje maana barakoa hazikupewa nafasi yake kabisa.

Mungu aliponye hili taifa liondokane na usukule wa hii miaka 5 iliyopita na awarudishie waja wake fahamu zao wajitambue kuwa wao ni binadamu hai wanaoishi!
 
Duh!

Viongozi wetu wa usalama wanakosea sana. Hadi kwenye misiba wanataka kutuaminisha kuwa wingi wa watu ndio upendo!

Anyway, naiombea familia ya Hayati Dr. JPM pamoja na Watanzania wenzangu faraja. Tusisahau kuwa kila aliyeumbwa na Mungu na kuwepo duniani anaumuhimu wake. Tuzidi kuombeana kila iitwapo leo.
 
Back
Top Bottom