Habari Mbaya kwa Watu Wote kama ilivyoandikwa na 'Raia Fulani'

Yani hapa nilipo bado kuna watu wanasikitikia yaliyotokea jana bungeni. Kwamba walikaa kitako wakisubiria kile Pinda alichosema atazungumzia Jumatatu wala wasisikie hizo habari njema. Wanalaani sana.
 
Yani hapa nilipo bado kuna watu wanasikitikia yaliyotokea jana bungeni. Kwamba walikaa kitako wakisubiria kile Pinda alichosema atazungumzia Jumatatu wala wasisikie hizo habari njema. Wanalaani sana.
Hata mwanamke akidengua sana wakati wavulana wengi wanamfukuzia, Pindi ashukapo thamani ndio anakuwa mrahisi.
Na Mizengwe Pinda atakaposhuka thamani, hata afanye action gani? watu hawatashtuka.
Kipindi hiki watu bado wana shauku ya kusikia lolote kutoka kwake, baba Mwanaasha akimtosa..... hata aende ukumbi wa habari(maelezo) sana sana atakuta waandishi walio kwenye mafunzo ndio waandike habari zake!
 
Yani hapa nilipo bado kuna watu wanasikitikia yaliyotokea jana bungeni. Kwamba walikaa kitako wakisubiria kile Pinda alichosema atazungumzia Jumatatu wala wasisikie hizo habari njema. Wanalaani sana.

Wanalaani sababu waziri mkubwa alibeba "ahueni" sasa ahueni yenyewe kagoma kuiweka kwenye hatma!
Sisi watz tunajichukulia kuwa watu wa "ahueni", watu tunaostahili kidogo, watu wa afadhali, watu tunaoendeshwa na misemo ya "sasa utafanyaje?, ndiyo nchi yetu ilivyo"

Ukitoa wazo kubwa (rejea uzi wa Mwanakijiji wa no half revolution),
ukitoa mawazo makubwa (rejea makala za jenerali juu ya katiba mpya)
Ukitoa mawazo makubwa (rejea andiko la Shivji juu ya ardhi )
hamna anayejali, na ndio maana hata kipindi kile cha mgomo wa madaktari wale wanaharakati walipoitisha maandamano baada ya kuona wiki nzima nchi ipo kimya huku watu wakifa, unakumbuka nini kiliwapata??
Walitukanwa na kuonwa wakorofi na wahatarishi wa amani yetu!

Ndio maana hata leo tunaomshukuru waziri mkubwa kwa kutuepushia ile "ahueni" kwamba ni kweli hii nchi hapa ilipo inataka shari kamili sio tena nusu shari.
Hapa Waziri mkubwa ametupa pa kuanzia!

Nani aanzishe?
Tunaangaliana.... Lol
 
Well said. Viongozi wa majeshi ndio kikwazo cha mapinduzi nchini. Wanajeshi wa kawaida wanataka sana kuipindua serikali ila viongozi wao ndio stumbling blocks.
Unaweza ukatakiwa kutoa ushahidi juu ya hili. Hata hivyo sidhani kama mapinduzi huwa yanafanywa na viongozi wa juu. Kama kuna mapinduzi yaliyowahi kufanywa na mkuu wa majeshi wa majeshi wa nchi nafikiri yatakuwa ni machache sana. maana hao wakuu wa majeshi siku zote huwa ni wafuasi wa uovu.
 
Wanalaani sababu waziri mkubwa alibeba "ahueni" sasa ahueni yenyewe kagoma kuiweka kwenye hatma!
Sisi watz tunajichukulia kuwa watu wa "ahueni", watu tunaostahili kidogo, watu wa afadhali, watu tunaoendeshwa na misemo ya "sasa utafanyaje?, ndiyo nchi yetu ilivyo"

Ukitoa wazo kubwa (rejea uzi wa Mwanakijiji wa no half revolution),
ukitoa mawazo makubwa (rejea makala za jenerali juu ya katiba mpya)
Ukitoa mawazo makubwa (rejea andiko la Shivji juu ya ardhi )
hamna anayejali, na ndio maana hata kipindi kile cha mgomo wa madaktari wale wanaharakati walipoitisha maandamano baada ya kuona wiki nzima nchi ipo kimya huku watu wakifa, unakumbuka nini kiliwapata??
Walitukanwa na kuonwa wakorofi na wahatarishi wa amani yetu!

Ndio maana hata leo tunaomshukuru waziri mkubwa kwa kutuepushia ile "ahueni" kwamba ni kweli hii nchi hapa ilipo inataka shari kamili sio tena nusu shari.
Hapa Waziri mkubwa ametupa pa kuanzia!

Nani aanzishe?
Tunaangaliana.... Lol

Nadhani dhana ya 'punje ya ngano' imetupitia mbali sana. Ngugi aliandika kuhusu A Grain of Wheat akielezea ni kwa namna gani wachache wajitoe kwa ajili ya wengi. Mataifa ya wenzetu wako mstari wa mbele sana katika kuhakikisha haki zao zinapatikana. Kwa wenzetu bei ya mkate tu ikipanda, kesho wako barabarani kuhoji.

Tatizo jingine hapa kwetu ni uelewa wa vyombo vyetu vya Dola hasa Polisi. Wanalishwa sana nidhamu ya utii wa woga hadi wanashindwa kuelewa wamtumikiaje mwananchi na Bosi wake. Polisi wetu ni tatizo sana.
 
Umejitahidi sana kutengeneza hiyo habari' tutakutunuku stashahada ya uzamili kwanza ukionyesha maendeleo mazur zaidi tutakupa ya uzamivu. ''CONGRAT'S"
 
1. Mkuu,Heshima! hii jumbe iko makini sana!natamani gazeti moja liichapishe kesho wananchi wengi waisome.mana kutokuwa widely read itakuwa sawa na uchoyo!

Hivi mtu kama Mh.MfutaKamba kabla ya kusema huo ***** wake huwa anafikiria kama kuna watanzania wenye brain, kama huyu jamaa?!

2. Wanabodi, halafu nimegundua kuwa hawa jamaa wa serikali wao hawajioni kama ni waovu, labda tutafute kuwaongelesha katika lugha ambayo wao wanajiona wanafanana nayo! - wajinga/wazembe/immature au...? Ndo tutaelewana nao na hatimaye watupishe.
 
Back
Top Bottom