Habari Mbaya kwa Watu Wote kama ilivyoandikwa na 'Raia Fulani'

we mkaree, nimeipenda makala makala yako. Umeiandika kwa ubunifu mkubwa na japo ni ndefu lakini inavutia kuisoma. Hongera sana.
 
Hii kitu imekaa vema sana, shukrani kwa ku-link hicho kisa cha kale enzi za tawala za kimabavu na hiki cha kimagamba.

Tunashukuru umetuongezea wigo wa kutafakari na kujipanga upya, kumbe bado tunatawaliwa kimabavu!!

Thumb up mkuu!!
 
Well said. Viongozi wa majeshi ndio kikwazo cha mapinduzi nchini. Wanajeshi wa kawaida wanataka sana kuipindua serikali ila viongozi wao ndio stumbling blocks.

Kuna mtu nilimsikia akisema "Mwamnyange hafai kabisa, nchi hii kwa uongozi hovyo hovyo uliopo, ilitakiwa ichukuliwe na jeshi wanyoshe mambo kisha wawakabidhi raia wema watawale".
 
Asanteni sana wandugu kwa pongezi hizi. Yote haya ni katika kuona ni jinsi gani na sisi tulio pembezoni (marginalized) tuna hamu ya kuona mabadiliko katika mfumo uliopo
 
kuna waandishi wa habari wavivu wa kufikiri ..hii makala utaikuta kwenye magazeti yao ya jumapili....wamekopy na kupaste..



hongera kwa uandish mahiri

Usiwe mchoyo ,kuna watu hawana access ya kuingia humu nayo ni jamii inastahili kupata hiki ambacho unaona waandishi kama wa vivu usiwe na mawazo membamba huo ni ubinafsi .
 
Duh Mkuu.. Mara ya mwisho kusoma mpangilio wa kifasihi kama huu ni abt 2 decades ago..! Toka kwenye vitabu vya Kuli.. Kusadikika na vingine..! Ahsante Mkuu Raia Fulani kwa kuweka makala iliosanifiwa kwa kiswahili chenyewe..
 
unajua hapa kwetu watu watapiga keleleeeee mwisho yatapita kama alivosema UPEPO UTAPITA !

Huu ni ukweli mchungu kwa kweli.
Sijui kwanini sisi watanzania tunaitikia tofauti na matakwa ya historia!
Wengi wetu hatutaamini kitakachotokea hapo 2015 kama hatutafanya kitu sasahivi
 
Hongera Ndugu kwa makala iliyotulia yenye mvuto na hisia kali inayoumiza wapenda haki.Inatupasa mkuu wa baraza ajue kuwa hata maandiko ya mMwenyeezi yanasema "Kiungo kimoja kikikukosesha, Heri ukitoe ili ukifa ufe ikiwa na viungo vichache kuliko uwe na viongo vyote ukaingia motoni" Sasa Rais aliyesema huu ni upepo acha upite, naye Mr Sugu alisema kile ni kimbunga kisipobomoa Nyumba kitatoka na Bati "Mwana wa Mkulima akiwa ndo Bati", sasa nimuunge mkono Mr. Sugu kuwa kimbunga kisipobomoa nyumba kinapotoka na Bati "Mwana wa Mkulima" kinaweza kutoka na Nguzo za nyuma JK yenyewe. Lazima wakati ujao yeye JK ndiyo apigiwe Kura ya kutokuwa na Imana naye" ili aone huo siyo upepo wa kupita bali ni Tsunami inayosomba kila kitu.
Nawasilisha
 
Usiwe mchoyo ,kuna watu hawana access ya kuingia humu nayo ni jamii inastahili kupata hiki ambacho unaona waandishi kama wa vivu usiwe na mawazo membamba huo ni ubinafsi .

hao waandishi wa habri wangekuwa wanaomba au hata wanapooandika wawe wanasema habari wameitowa wapi...habari nyingi huwa wanatoa humu na kuweka kwenye magazeti yao halafu wanasema imetoka kwa ''wan bidii'' hao kitu ambacho ni uongo
 
Makala nzuri sana, ukiisoma kwa kweli inaingia akilini na moyoni pia.

Unaweza ukapata hamasa hata za kuingia barabarani kutafuta ukombozi.

Hongera sana Raia Fulani
 
Back
Top Bottom