Habari Mbaya kwa wanaotafuta kazi- Hakuna ajira mpya mwaka huu ila kwa Walimu na Madaktari

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Jana jioni nilikuwa kijijini kwetu. Nikiwa namshauri mdogo wangu alihitimu kidato cha sita nini akasome Chuo kikuu mara ujumbe unaingia kwenye simu yangu
"HAKUNA AJIRA MPYA WALA KUPANDA VYEO MWAKA HUU, AJIRA ZILIZOPO NI UALIMU NA UDAKTARI TU".
Ujumbe ulitoka kwa rafiki yangu ambaye yupo kwenye reliable source of news.
Sababu ni zilezile, ukata ulioikumba serikali. Hali ni mbaya kuliko tunavyofikiri. Kwa watakaoshindwa kupanda vyeo mwaka huu inaweza isiwe tatizo ila waombaji wapya wa kazi.... Sijui!
 
Mshauri akasome kuondoa ujinga ili aweze kuja kumudu maisha yake baada ya ku graduate na si kutegemea ajira ya mshahara toka serikali au kwingine kokote..........kilimo kwanza!!
 
Nadhani hizo zitakua ni hbari za kweli kwakua mimi pia nilipewa hizo habari tangu mwanzo wa mwezi huu wa 5.Na pia aliynipatia huu ujumbe anaaminika.
 
Hutuendi shule ili tuje kuajiriwa bali kuelimika.

Mtu aliyeelimika hawezi kubabaika na ajira kwasababu anajua
ataweza kutumia ujuzi wake kujitafutia riziki.

Dunia ya sasa inarudi kule tuliko toka (kujiajiri) haya mambo ya
kufanya kazi kwenye makampuni makubwa kidogo kidogo yana
ondoka kwasababu vitu vingi vinarahisishwa kwa kutumia mashine.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Hayayayaya!kudaaadeki!wanaandaa (wezi,wapiga debe,wala unga,machinga,vibaka,machangu,n.k)kwa maana nyepesi hili kundi ni bomu la squad ambalo timing yake linalipuka mwaka huu,it marks the end of rotting ccm,ntahakikisha naifikisha taharifa hii kwa wahusika(wahitimu)ili waanze harakati za kulipua Abbotabad mpaka nduli adui (ccm)anatekwa nyara,gud nyuuuzi!
 
jana jioni nilikuwa kijijini kwetu. Nikiwa namshauri mdogo wangu alihitimu kidato cha sita nini akasome chuo kikuu mara ujumbe unaingia kwenye simu yangu
"hakuna ajira mpya wala kupanda vyeo mwaka huu, ajira zilizopo ni ualimu na udaktari tu".
Ujumbe ulitoka kwa rafiki yangu ambaye yupo kwenye reliable source of news.
Sababu ni zilezile, ukata ulioikumba serikali. Hali ni mbaya kuliko tunavyofikiri. Kwa watakaoshindwa kupanda vyeo mwaka huu inaweza isiwe tatizo ila waombaji wapya wa kazi.... Sijui!

bali anayemtumaini BWANA ni jasiri kama simba hataogopa habari mbaya.
 
Jana jioni nilikuwa kijijini kwetu. Nikiwa namshauri mdogo wangu alihitimu kidato cha sita nini akasome Chuo kikuu mara ujumbe unaingia kwenye simu yangu
"HAKUNA AJIRA MPYA WALA KUPANDA VYEO MWAKA HUU, AJIRA ZILIZOPO NI UALIMU NA UDAKTARI TU".
Ujumbe ulitoka kwa rafiki yangu ambaye yupo kwenye reliable source of news.
Sababu ni zilezile, ukata ulioikumba serikali. Hali ni mbaya kuliko tunavyofikiri. Kwa watakaoshindwa kupanda vyeo mwaka huu inaweza isiwe tatizo ila waombaji wapya wa kazi.... Sijui!
Unazungumzia ajira ya serikali au hata AKINA ZANTEL NA MANYAMONGO.............????
 
Hata za hazina tulizohaidiwa tangu octoba2010 zimeyeyuka? Sasa mkuu unaleta msiba kwenye sherehe!
 
Mimi naona si habari baya bali njema kwa namna moja au nyingine. Mimi Agrodealer naumwa kuhudumia wakulima bila malipo. Juzi kati nimeona watoto wanasema mimi nikimaliza chuo nitafanyia kazi career yang na hawajui kama wa2 tunatafuta kila sector juu chini bila mafanikio. Nishaweka career pembeni mpaka sasa ctak tabu. Kusoma miaka hii ni kupata elimu na kujua life style mbalimbali si kuajiriwa. Wa2 laki moja wana degree bila ajira ni sawa uanzishe shule bila learning environment huu c wizi huu.
 
Hata za hazina tulizohaidiwa tangu octoba2010 zimeyeyuka? Sasa mkuu unaleta msiba kwenye sherehe!

hazina wameajiri kimya kimya na NSSF wanafanyisha watu usaili jumamosi hii kwenye chuo cha IFM , mashirika mengine kama MSD,TBA, NAO, kama mnataka ajira jaribuni kufuatilia magazeti ya muhimu sio mnasoma magazeti yale ya stori
 
Hata za hazina tulizohaidiwa tangu octoba2010 zimeyeyuka? Sasa mkuu unaleta msiba kwenye sherehe!

Ha ha ha sio mimi Mkuu ni serikali ya watu, iliyowekwa na watu kwa manufaa ya watu
 
Unazungumzia ajira ya serikali au hata AKINA ZANTEL NA MANYAMONGO.............????

you are a great thinker man!

au umeuliza kwa lengo la kumkosoa muanzisha uzi huu kuwa hiyo ni sahihi kwa sirikalini tu.....:biggrin1:
 
Kwa mantiki hiyo, kwani ajira zipo serikalini tu? Mbona "private sector" ndio muajiri mkubwa zaidi ya Serikali.
 
Maisha bora kwa kila Mtanzania!!!!!!!!!!! Aaaaggrrrrrrrrh Hasira sana Walimu na Madaktari..watoto wao wanasoma mbali wanatibiwa mbali sisi tunaotegemea shule zetu za magoma kitakita tumikwisha..Ualimu ni wito kama udaktari siheri zingekuwepo nafasi za Jeshi Tukajifunze mbinu zetu zile tuje tujikomboe maskini maana huku tunakoenda sio kabisa itafikia wakati tutaomba hata VITA VYA SHILINGI MOJA TU ili tubadili mfumo huu maana kila kitu usanii .. KATIBA usanii kila kitu usanii Tumechoka bwana tupeni nafasi nasisi tupate walau nafasi ya kujenga nchi yetu ..sisi tupo shule tunasoma ili tuje tupate ajira nanyi mnasema ajira hamna wakisema kina Dr Slaa mnasema wanataka kuchafua AMANI!!!:pound:

TUBADILIKE JAMANI WAKATI UNAPITA TUACHE LONGO LONGO......Maendeleo yanakuja kwa mipangilio mizuri inayopangwa na viongozi na wasomi wenye mapenzi na nchi yao. TUPENI NAFASI JESHINI NASISI TUNAWEZA:mod::mod:
 
kaka!hakuna afadhali hata kidogo.sema wote tumechoshwa na hii hali hope 2015 mambo yatabadilika.
 
zitto kabwe akisema serikali imefulia .....wanasema ametukana serikali haya sasa habari ndiyo hiyo ..serikali ya kikwete ni kiwete ..matumizi makubwa ya srikali yake ..kakuta mkapa kaacha pesa nyingi yeye badala ya kukusanya anatumia tu ..uchaguzi ccm imetumia garama ngapi ..mimi nasema ...hii nchi angekabidjiwa kagame tu kwa contract ..mabadiliko tungeyaona siku huyo ****** hamna kitu hapo tuliingia choo cha kike
 
Hapa ndipo utakapojua aina za elimu tunazosoma. Makelele meengi na "degree" zetu. Degree kwenye makaratasi, kichwani hakuna independence. Viingereza viiingi vya kutazamia tamthilia na kuwatisha makonda.
 
zitto kabwe akisema serikali imefulia .....wanasema ametukana serikali haya sasa habari ndiyo hiyo ..serikali ya kikwete ni kiwete ..matumizi makubwa ya srikali yake ..kakuta mkapa kaacha pesa nyingi yeye badala ya kukusanya anatumia tu ..uchaguzi ccm imetumia garama ngapi ..mimi nasema ...hii nchi angekabidjiwa kagame tu kwa contract ..mabadiliko tungeyaona siku huyo ****** hamna kitu hapo tuliingia choo cha kike
Mkapa aliacha pesa wapi fisadi mkubwa yule.Mabomu yote ya mikataba feki aliifanya yeye kipindi cha mwisho anaondoka,richmond,rada,meremeta na mengine mengi.Leo unampaka asali eti ameacha hela?Au binamu ako?
 
Back
Top Bottom