Habari maelezo wajibu Propaganda na upotoshaji wa Tundu Lissu

Kweli Lissu kiboko serikali nzima inacheza mziki wake, kuna memba jana alisema baada ya vigongo vya jana vicheche vyote vya Lumumba vitatoka na kweli, tunamsubiri mkuu wao naye amjibu Lissu.
Wanakiu nae haasa lkn hawana namna
Kwa waliomsikiliza Lissu huenda wakawa na kuongeza,je amejibiwa yale aloyasema JANA?

May Allah bless Me and You


Sent from Calculator Phone vesion007
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Majibu ya kina dhidi ya propaganda na upotoshaji wa Mbunge wa Singida Mashariki Ndug Tundu Lissu.

View attachment 545237
View attachment 545238
Bora kukaa kimya !! Mmejibu nn hapa...??

Tueleze huko wizara ya fweza ni urongo ?
Tueleze ukanda na ukabila...!
Tueleze demokrasia gani mtu ahojiwe polisi kisa eti fulan kaja kufuturu kwake !
Tueleze kamata kamata ya hawa ma DC na RC kwa sababu za kipuuzi ni urongo !!

Inatia aibu na kichefuchefu. Kama kuna kitu cha kujifunza, basi jifunzeni kwa JMK...!! Mnajenga misingi mibaya ya kubaguana na kufanya siasa ni vita. Waacheni nao wafanye siasa zao sababu mwisho wa siku wananchi ndo watapima. Kuwakandamiza bila sababu tena kwa kauli za hadharani kuwa wabanwe na kutimuliwa bngeni halaf eti nyie mtawashughulikia nje ya bunge ni kujenga uhasama husio na msingi kabisa. Baba wa Taifa mnaejifanya kumuenzi hakuwa hivyo!
 
Aliyeandika hapo ni Doctor ? a PhD holder ? Mbona kaandika taarabu na mipasho badala ya kujibu hoja? Nielekezeni na mimi nikachukue huo udoctor mwepesi kama huo
 
Siku moja nilikuwa na rafiki zangu katika 'kiwanja' kimoja maarufu hapa jijini tukipata vinywaji. Ghafla sauti ya muziki ikabadilika na kuwa kubwa mno, na baadaye tukatangaziwa kwamba kuna 'promosheni' ya sigara fulani. Wadada warembo wakawa wanapita mezani kwa wateja kutushawishi tununue na tuvute sigara zile kwa bei ya 'promosheni'. Pamoja na urembo wa wale akidada ilikuwa zoezi gumu sana kutushawishi wateja wengi kununua na hatimaye kuvuta sigara zile. Mmoja wa wateja aliyekaa mezani kwetu alimuuliza mmoja wa warembo kama amewahi kuvuta sigara zile anazozifanyia 'promosheni', binti mrembo yule, alikataa kwamba havuti, hajawahi kuvuta na hatakuja kuvuta sigara maishani mwake. Tulimpa changa moto kwamba sote tulikuwa katika meza ile hatujawahi kuvuta sigara tangu kuzaliwa, na atupe sababu za msingi kwanini leo, tuanze kuvuta sigara, wakati tunajua kwamba ina madhara, hata juu ya ganda lake imeandikwa tahadhari kwamba 'Sigara Ni Hatarai Kwa Afya Yako'. Wengi wetu tuliishia kupiga soga na warembo wale na kuendelea kuusikiliza muziki ule mkubwa. Lakini sigara zilidoda.

Katika maafisa wa masoko walio jasiri ni wale wanaofanya kazi za masoko katika makampuni ya sigara. Ni majasiri kwasababu katika nafsi zao wanaamini kabisa kwamba sigara ni sumu, na wao wenyewe hawaipendi sigara, na kwamba ni hatari kwa wavutaji na hata walio jirani na wavutaji. Ni majasiri kwasababu inabidi watangaze na wauze bidhaa ambayo wao wenyewe hawaiamini na wala hawaikubali. Lakini wanaendelea kuitetetea kwasababu wana njaa, hawana ajira hivyo inabidi wagange njaa kwa kuitangaza sigara kwamba ni kiburudisho bora.

Utawala huu wa awamu ya tano umefanya mambo kadhaa mazuri yanayostahili kupigiwa makofi. Mfano, kuongeza uwajibikaji na nidhamu makazini, kupunguza wafanyakazi hewa, kupunguza kwa kiwango kikubwa uhaba wa madawati shuleni, kuboresha ukusanyaji kodi, kupiga vita ufisadi na kadhalika. Lakini pia kuna maeneo utawala huu umefanya vibaya sana. Maeneo ambayo inafanya vibaya ni, utawala bora, kusimamia utawala wa sheria, haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari, diplomasia, mahusiano ya kisiasa n,k.

Ni rahisi sana kwa watendaji na maafisa wa serikali kuyatangaza na kuyatetea yale mazuri yanayoendelea kufanyika.

Lakini niwaase watendaji na maafisa wa serikali kwamba itakuwa vigumu sana kwao kutetea masuala ambayo serikali inafanya vibaya tayari, mfano; utawala bora, kusimamia utawala wa sheria, haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari, diplomasia, mahusiano ya kisiasa.

Ugumu wa kuyatetea masuala haya, naufananisha na kazi ngumu waliyonayo maafisa masoko wa kampuni za sigara.
 
Wadau ni muda umepita tokea Rais wa TLS mh Lissu kutoa tuhuma kwa serikali na kwa Rais wa Tanganyika kuwa anaendesha nchi kwa misingi ya udini, ukabila,ukanda na undugu pia anavunja sheria za nchi ambazo yeye ameapa kuzilinda. Mh lissu alitaja vielelezo kadhaa dhidi ya hizo tuhuma lakini jambo la kushangaza kesho yake msemaji wa ikulu akaja na majibu mepesi na kwa ujumla mimi kama mwalimu naweza kusema hayakuwa majibu sahihi ya kujibu hoja za Lissu na hii ni kituko kingine kwa serikali cha kushindwa kutoa najibu sahihi. Lissu alitaja mpaka vyeo vya watu vyeo ambavyo kwa kawaida vinapokaliwa na watu wa sehemu moja lazima hofu iibuke, je serikali mnaweza kuidhibitishia mahakama kuwa kitu alichokiongea Lissu ni uongo IGP, Mkuu wa majeshi, AG, na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali pia na kuhusu tuhuma dhidi ya uongozi wa wizara ya fedha ni uongo? Mimi kama mwananchi was kawaida naomba kutoa wito kwa serikali kurudi tena wajibu hoja za Mh Lissu na siyo kukalia vitisho.
By Kamanda wa Musoma kwa sasa Arusha
 
Hoja gani hasa ulitaka ijibiwe? hujui kuwa kesi iko mahakamani? Hoja zote zitajibiwa mahakamani.
 
Back
Top Bottom