Nimeufuatilia huu mjadala unafurahisha sana. Napenda kuchangia nami kidogo. Kwanza siwezi kukataa kuwa walimu wa vyuo wanaweza kuwa na mahusiano na wanafunzi wao. Kwa hali ya kawaida hakuna sheria inayokataza kuwa na mahusiano na mwanafunzi. Wanafunzi wengine ni wake za waalimu wa chuo. Kuwa na mahusiano ambayo yanaenda kinyume na utaribu za kazi kama kupendelea mwanafunzi kwa sababu mnauhusiano naye wa kimapenzi ni 'moral decay' ambayo huwezi kuitumia kuonyesha kuwa walimu wote wa chuo kikuu wameoza. Moral decay kwa sasa ni national crisis, ndiyo maana leo hii unaweza kununua kura! Kila siku tunasikia watu tuliowaamini wanaiba mali ya umma! Kwa hili kama taifa tuna tatizo.
Pili, Mwandishi wa makala hii nafikiri ameandika hisia zake, maana mimi nimekaa 'university' kwa miaka 13 sijaona hiyo hali kama mwandishi alivyowasilisha. Nikiwa kama mwanafunzi wakati nasoma UDSM, hii 'rumours' ilikuwepo kuwa fulani kapewa mtihani! lakini matokeo ya huyo anayesemekana amepewa mtihani unakuta amefaulu kwa margin ya 'D'.
Tatu, Uzoefu wangu unaonyesha kuwa msichana akiwa 'smart' darasani na amekuwa anafulu vizuri kuliko wanaume hisi kuwa anapewa mtihani ndipo inakoanza na kupata kasi! Hili tunahitaji kulifanyia utafiti/nitalifanyia utafiti zaidi. Mimi nina rafiki yangu mwanamke nimesoma naye Chemistry darasa moja UDSM, yule dada alikuwa na uwezo wa hali ya juu sana, mimi binafsi sijawahi kukutana na binadamu mwenye akili kama yeye! Sasa hivi anamalizia PhD yake ya chemistry huko Uholanzi. Wakati tunasoma kulikuwa na hisia kuwa anapewa mtihani. Lakini huyo dada alikuwa anapata 'A' kila somo.
Nne, hawa watu au wanafunzi wanaolalamika kuwa wasichana wanapewa mtihani wamechukua hatu gani kuzuia hilo tatizo?Nauliza hivi kwa sababu chuo kikuu watu wanafundishwa 'critical thinking' and beyond'! Chuo kikuu ni sehemu ya kukuza maarifa na kuleta mabadiliko! ya kifikra na kimatendo!Kama mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kuwa mtumwa kiasi hicho hapaswi kuwa chuo kikuu akatafute mahali pengine pa kusoma maana hatasaidia jamii akimaliza chuo
Tano, Chuo kikuu haiwezekani mwalimu akamfelisha mwanafunzi mtihani ambaye ameandika majibu sahihi. Kuna utaratibu ambao unamlinda mwanafunzi na mwalimu. Mwanafunzi akiona kuwa anaonewa anaweza kukata rufaa. Hili la kuwa professor anaweza kukufelisha kwa sababu umetembea na binti yake au na mpenzi wake sio kweli. Mwandishi nafikiri ameaandika hisia zake kwa sababu hajui mitihani ya chu kikuu inavyoendeshwa.
6. Sasa hivi kuna 'mfumuko' wa vyuo hapa Tanzania, vingine huwezi kuamini kuwa ni vyuo! vinafanana na high schools! labda huko hiyo biashara inakofanyika! ingawa sina uhakika maana sijafanya utafiti.
Kama hayo mambo yapo popote tuchukue hatua sote.