Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,885
- 6,885
Rushwa ya ngono imekithiri vyuo vikuu
LEO wazalendo wenzangu nina mada ambayo imejificha kidogo, ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya taifa kwa namna moja. Kama macho yako yatakuwa yametazama kichwa cha habari hapo juu, utakuwa pamoja nami na kufahamu nini nataka kuzungumzia.
Jana katika harakati za shughuli zangu za kila siku niliweza kutembelea moja ya chuo cha elimu ya juu hapa nchini. Mandhari ya chuo hicho ni mazuri yanayovutia sana, binafsi nimevutiwa na hali ya usafi wa mazingira ya chuo hicho. Nilikuta wanafunzi wakijisomea makundi kwa makundi, wanawake na wanaume.
Kuna malalamiko kuwa eti baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu huwa wanataka wapewe rushwa ya ngono ili watoe majibu ya mitihani kwa wanafunzi wanawake! Hili ndilo lililopelekea mimi kufanya uchunguzi ili niweze kugundua ukweli wa mambo. Najua yawezekana kama wewe ni mwanafunzi mwanamke umewahi kukutana na tatizo hili!
Naamini kabisa wapo baadhi ya wanafunzi wanaokubali kutoa rushwa ya ngono ili waweze kufaulu lakini wengi wao hawapendi kitendo hicho cha udhalilishaji.
Nikafika chini ya mti mmoja ambao walikuwa wameketi wanafunzi wanawake na kuwasabahi kabla ya kuanza uchunguzi wangu juu ya jambo hilo. Wakanieleza kuwa tatizo la rushwa ya ngono lipo na wahadhiri wanalitumia kama silaha pekee kufanikisha jambo hilo.
Mmoja wa wale wanafunzi alisema, "yaani hata ukiwa na rafiki yako wa kiume ni tatizo, mnaweza kufelishwa mitihani yenu kwa sababu eti umekataa kutembea na mhadhiri!" Tatizo la rushwa ya ngono lipo karibu vyuo vingi vya elimu ya juu hapo nchini, lakini hebu tujiulize ni hatua gani zimechukuliwa mpaka sasa!
Kuna malalamiko mengi katika vyuo kuwa baadhi ya wahadhiri wana tabia ya kuwataka kimapenzi wanafunzi wa kike ili waweze kuwapa majibu ya mtihani. Malalamiko ya wanachuo ambao wanatakiwa kutoa rushwa ya ngono yanapopelekwa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi ya hao, hilo ni tatizo ambalo linapaswa kutafutiwa dawa. .....
Habari Leo