Habari leo: Vilaza 1,194 wachaguliwa Sekondari Ukerewe


M

Mantombazane

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2014
Messages
461
Likes
157
Points
60
M

Mantombazane

JF-Expert Member
Joined Sep 7, 2014
461 157 60
Gazeti la Serikali Habari leo la 25/10/2017 limeandika habari ya kusikitisha katika mfumo wetu wa elimu ambapo wanafunzi 1,194 walichaguliwa Sekondari 2015 lakini wakiwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.

Kilicho nileta jukwaani sio hasa hiyo habari kwani ni matukio ya kawaida katika mfumo wetu wa elimu. Kilichonileta hasa ni matumizi ya hilo neno "Vilaza" ambalo kwa siku za hivi karibuni limekua kwa haraka sana ingawa ni neno la kawaida vyuoni lakini baada ya rais Magufuli kulitumia alipokuwa akizungumzia wanafunzi waliokuwa wanasoma Udom. Pamoja na kuwa ni neno linalotumika kuelezea mtu au watu wenye uwezo mdogo katika mambo mbali mbali mfano elimu au ujuzi wa mambo.

Kinachonishangaza ni kuwa imekuwa neno hilo hilo alilolitumia rais kuelezea kuhusu wananchi wake lakini lilipotumika kumwelezea yeye limesababisha mtu akapelekwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo au faini ambapo muathirika alilipa faini. Sasa kama vyombo vya umma kama hilo gazeti vinatumia hilo neno ikiwa ni pamoja na rais mwenyewe inakuwaje mwananchi huyu akatiwa hatiani? Mimi nashauri mamlaka husika kumrudishia faini aliyolipa kwani ni kumwonea sheria haipaswi kuwabagua raia wa nchi moja.

Mimi namshauri mhusika akate rufaa au idara ya mahakama kufikiria kumrudishia mhusika pesa yake kwani neno hilo halina madhara yoyote sawa na Kihiyo au hilo jingine lilillo kua kwa kasi sana la bashite. Kihiyo linatumika kumwelezea mtu anayejidai kuwa na elimu au uwezo fulani wakati hana ambalo kwa sasa linaweza kuwa na maana inayokaribiana sana na kilaza wakati bashite sasa hivi linatumika kumwelezea mtu aliyefoji vyeti kwa kuimpersonate yaani kutumia cheti cha mtu mwingine kujipatia masomo au kazi. Hakuna matusi yoyote hapo na maneno hayo yana asili zake ambazo zinajulikana wazi. Ukienda kwenye fasihi maneno hayo tunaweza kuyaita kuwa ni metaphor kwa kiingereza au Sitiari kwa kiswahili.

Hii ndiyo habari yenyewe:

WANAFUNZI 1,194 wasio na sifa wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, walichaguliwa kwenda sekondari mwaka 2015 wakati hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Frank Bahati. Amesema uchunguzi unaendelea dhidi ya walimu wote waliohusika kuvujisha mtihani wa darasa la saba mwaka 2015.

Kwamba uchunguzi utakapokamilika, watachukuliwa hatua za kisheria. Alisema hayo katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika jana mjini Nansio, kujadili na kuweka mikakati kukabili tatizo la wilaya hiyo kuendelea kufanya vibaya kitaaluma.

Bahati alisema hatakuwa na huruma kwa walimu wanaokiuka maadili ya kazi. Alieleza kuwa katika uchunguzi aliofanya, amebaini walimu wakuu 72 wa shule za msingi na waratibu elimu kata 18, walihusika kufanya udanganyifu katika mtihani wa darasa la saba mwaka 2015, hivyo kusababisha wanafunzi 1,194 wasio na sifa wachaguliwe na kwenda sekondari wakati hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.

Mwaka 2015 Ukerewe ilikuwa ya kwanza mkoani Mwanza kwenye wilaya za Buchosa, Magu, Misungwi, Sengerema, Ilemelana Nyamagana wakati kitaifa ilishika nafasi ya tano kati ya shule za msingi 186.

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Estomiah Chang’ah aliitisha kikao hicho kujadili na kuweka mipango ya kuikwamua kitaaluma, baada kuwa ya mwisho kati ya wilaya saba za mkoa wa Mwanza kwa mara ya pili mfululizo katika matokeo ya darasa la saba, yaliyotangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ofisa Elimu Msingi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Reonard Richard alisema jumla ya wanafunzi 10,042 walifanya mtihani huo mwaka huu, lakini waliofaulu ni asilimia 50.7, hivyo kushuka kwa asilimia 12 ikilinganishwa na ufaulu wa asilimia 62.1 wa mwaka uliopita.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kakerege, Deus Tibalemwa alisema udanganyifu wa mitihani uliofanyika huko nyuma, ndio sababu ya walimu kufanya kazi kwa mazoea na kuacha kujituma, hivyo kusababisha anguko la kitaaluma linalotokea sasa, baada ya kuwepo usimamizi mzuri wa mitihani. Mkuu wa Wilaya, Chang’ah aliahidi kuunda tume ya uchunguzi kubaini sababu za tatizo hilo.
 

Forum statistics

Threads 1,251,863
Members 481,917
Posts 29,788,114