Habari Leo Lina Wahariri Wasomi Kweli?


frema120

frema120

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2012
Messages
5,102
Likes
35
Points
135
frema120

frema120

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2012
5,102 35 135
Wakuu salama?

Kwanini gazeti hili swala la zitto na chadema limekuwa likikazania sanaaaaaaa na wakati mwingine kuandika habari za uongo uongo tuu sanaaaaaaaaaaaaaaa kwanini lakini???!!!

check mbele ya habari leo


  • asongeza mbele ziara yake - wakati chini kabisa kuna taarifa ya ziara hipo palepale
  • zapigwa kiberiti - kweli statement hii mbona kali sanaaaa
hivi hili gazeti lina wahariri makini kweli au wanafata lumumba wanasema nini, kwani wandishi mzuri kabla ya kuchapa habari utafuta ufafanuzi pande mbili.


check na huyu naye.sijui habari leo habari hii hawakuipata.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa ataanza ziara ya siku 20 katika mikoa ya Shinyanga na Kigoma, kuanzia Desemba 4-23, mwaka huu.

Lengo la ziara hiyo ambayo imetokana na maombi ya muda mrefu ya viongozi wa chama katika maeneo husika, ni kuimarisha na kukagua uhai wa chama katika majimbo ya mikoa hiyo.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakutana na wananchi katika mikutano ya hadhara ambapo atazungumzia masuala

ya kitaifa na eneo husika, kisha atafanya vikao vya ndani na viongozi pamoja na wanachama.

Siku ya Jumatano Desemba 4, mwaka huu Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Wilaya ya Kahama, siku inayofuata Desemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo la Muhambwe.

Ratiba ya siku zinazofuata itaendelea kutolewa kwa vyombo vya habari.

Imetolewa leo Jumanne, Desemba 3, 2013, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA


================================================
NB:
Kuna mtu kaja nalo ofisini hapa nimelichana nakutupa kwenye kidust bin, gazeti la serikari badala ya kuandika vitu vywa msingi kwa taifa na watanzania mjini, vijijini na mikoani huko kama wakulima kuzulumiwa mauzo yao, migogoro ya wakulima na mifugo plus ardhi, manyanyaso ya wazawa kwenye migodi n.k, wizi wa halmashauri n.k wao ni masiasa tuuuuuuuuuu kwani wasiachie uhuru, mzalendo na tazama haya ndio ya siasa.
 

Forum statistics

Threads 1,252,079
Members 481,989
Posts 29,794,899