radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,427
- 32,191
KUNDI la wafanyabiashara ndogo maarufu machinga na lile la waendesha pikipiki maarufu bodaboda katika wilaya ya Ilala, wamemuomba Rais John Magufuli kutosikiliza kelele za wanaopinga jitihada zake, kwani hawana uzalendo kwa taifa lao.
Makundi hayo yalitoa ujumbe huo jana katika risala iliyosomwa na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara ndogo, Namoto Namoto mbele ya mgeni rasmi, Waziri wa Madini, Angella Kairuki walipokusanyika kumpongeza Rais Magufuli katika jitihada zake mbalimbali alizozifanya tangu aingie madarakani miaka miwili iliyopita.
“Tunamuomba Rais asisikilize kelele za watu wanaombeza kwani wengi wao hawana uchungu na uzalendo kwa taifa lao, sisi wananchi wanyonge daima tuko pamoja naye bega kwa bega,” alisema. Walisema Rais Magufuli ni mzalendo namba moja katika kupigania maslahi ya wanyonge na taifa kwa ujumla.
“Sisi wananchi wanyonge tumeamua kupaza sauti kama ishara ya kuunga mkono jitihada zote ulizozifanya katika nchi yetu katika sekta mbalimbali,” alisema. Alitaja baadhi ya jitihada zilizofanywa na Rais kuwa ni pamoja na kubaini madudu yaliyokuwa yakitendeka katika sakata la makinikia na pia Kampuni ya uchimbaji ya Barrick Gold Mining kukukubali kuilipa serikali ya Tanzania Sh bilioni 700 kwa udanganyifu walioufanya kwenye mchanga wa madini.
Chanzo habari leo.