Habari hizi ni kweli kuhusu matrafiki?

Igangilonga

Senior Member
Mar 11, 2006
133
27
Jana jioni wakati narudi home kutokea Mwenge nilikuta foleni ya ubungo mataa kuelekea Mwenge imepitiliza njiapanda ya sinza makaburini inaelekea Mlimani City na matrafiki na mapolisi wa kawaida wamejaa kibaao wamekamata magari mengi yanayopita service road.... katika ongea ongea ndani ya daladala ikazuka hoja kuwa hiyo ni mbinu wanayoitumia trafiki siku hizi kujipatia hela especially wikend.... yaani wanamwambia mwenzao anaeongoza mataa asiruhusu njia fulani kwa muda mrefu wakijua kuwa watu wengi watapita service road halafu wao wanawapiga bao wanakula hela yao then baadae wanamkatia na mwenzao (anaeongoza magari)....mnalionaje hili, lina ukweli?
 
Back
Top Bottom