Habari hii - Itawasaidia zaidi wale waliokata tamaa ya maisha......................! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari hii - Itawasaidia zaidi wale waliokata tamaa ya maisha......................!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mtambuzi, Apr 4, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Alikuwa akisafiri kwenye barabara kuu akiwa juu ya pikipiki yake. Alikuwa akiendesha kwa wastani wa kilimeta 65 kwa saa. Jambo lenyewe lilitokea ghafla sana. Aligeuka kutazama pembeni mwa barabara na aliporudisha macho barabarani, gari kubwa la mizigo lililokuwa mbele yake lilikuwa limesimama ghafla.

  Ilikuwa ni ghafla mno kiasi kwamba hata akili kufikiri ilikuwa ngumu sana. Kwa kutaka tu kuokoa maisha yake mawazo ya nguvu za mwisho yalimjia ambapo aliangusha pikipiki na kuburuzika chini ya gari hilo. Wakati akiburuzika, kifuniko cha tangi la mafuta la pikipiki yake kilifunuka na jambo baya lilitokea.

  Moto ulilipuka akiwa bado anaburuzika chini ya gari hilo. Anachokumbuka baada ya hapo ni kupata fahamu wakati akiwa hospitalini. Alikuwa ameungua karibu mwili wote kwa kiwango ambacho hata kupona ilionekana ni suala la Mungu mwenyewe. Lakini yeye hakukata tamaa katu. Alisema kwamba anataka kupona na kwamba ni lazima angepona.

  Alipona na kuanza shughuli zake za biashara kama vile hakuwa amepatikana na ajali ile mbaya. Lakini haikuchukua muda kabla hajapambana na kisirani kingine cha maisha. Ilikuwa ni wakati wa safari zake za kibiashara, ambapo ndege aliyokuwa akisafiri nayo ilianguka naye akaponea chupuchupu. Lakini akalemaa kuanzia kiuno kwenda chini. Hakukata tamaa. Alisema anataka kuishi na siyo kuishi tu bali kuishi kwa mafanikio. Alipopona alirudi katika biashara zake kama vile hakukuwa kumetokea jambo lolote baya au la kuvunja nguvu.

  Huyu siye mwingine bali ni mfanyabiashara maarufu sana kule Colorado nchini Marekani, William Mitchel, ambaye baada ya mitihani hii mikubwa ya kimaisha alipata ari mpya ya kutafuta mafanikio maishani. Aliendelea kufanya biashara huku akiwa na makovu na ulemavu hadi akafanikiwa kuingia kwenye orodha ya mamilionea wa Marekani.

  Bila shaka unafahamu kwamba kwenye maisha huwa tunapitia hatua mbalimbali za mabadiliko kutoka mafanikio kwenda maanguko au kinyume chake na kutoka faraja kwenda visirani au kinyume chake. Kila mmoja wetu ana njia ambayo huchukulia mabadiliko haya. Kuna wakati ambapo huwa tunasema tunajaribiwa, tunapewa mitihani na mungu. Hali hii iko duniani kote na kwa kila binadamu kutegemea tu mazingira ya mitihani hiyo. Wakati huu ni ule ambapo kila tulicho nacho kama ulinzi wetu hujaribiwa. Huu ni wakati ambapo huwa tunayatazama maisha kama yasiyo na haki na yanayoonea au kutazama upande mmoja.

  Hiki ni kipindi ambapo imani zetu, thamani ya utu wetu, viwango vya subira zetu na uwezo wa kujizatiti hufikishwa kwenye ukomo, ambao tunadhani hatuwezi tena kuwa na vitu hivyo. Kwa baadhi ya watu, hutumia vipindi kama hivi vya mitihani ya maisha kuwa watu bora zaidi, wakati wengine hutumia vipindi hivi kukata tamaa na kuharibu kabisa maisha yao. Je umeshawahi kujiuliza maishani mwako ni kwa nini baadhi ya watu hutumia mitihani ya maisha kufanikiwa na wengine huitumia kwa kuanguka kabisa maishani?
  Ukweli ni kwamba siyo kuwa watu walifanikiwa hawana au hawakupitia mitihani katika maisha, tena huenda wamepitia mitihani mizito kuliko wale ambao hawana mafanikio maishani mwao. Mahali ambapo hakuna matatizo ni kaburini tu, lakini kwenye maisha matatizo ni lazima kwa yeyote.

  Kama Mitchel alivyoungua mwili mzima, ilikuwa ni juu yake kuamua kuhusu tukio hilo. Kama angeamua kwamba kuungua kule ulikuwa mwisho wa maisha , mwisho wa kutafuta mafanikio, bila shaka angefia hospitalini au hata kama angepona, angebaki mtaani kuombaomba. Lakini kwake kuungua kule kulikuwa ni changamoto katika kutafuta maana halisi ya maisha. Alijiambia kwamba, mtihani ule wa kuungua haukuwa umempata tu kwa sababu ya kumpata, bali kulikuwa na maana kubwa, kusudi maalum kubwa. Kusudi ambalo linalenga kwenye kubadili maisha yake kwa mafanikio makubwa zaidi.

  Ni wangapi kati yetu ambao wanapopambana na mitihani ya maisha huchukulia mitihani hiyo kama mwisho wa maisha yao. Huanza kuchanganyikiwa na hata kuamua kujiuwa? Ni wangapi ambao wanapopambana na mitihani ya maisha huanza kuwanyooshea kidole wengine kwamba ndio wamewasababishia matatizo hayo kwa kuwaloga au kwa njia nyingine? Ni wangapi ambao wanapopambana na mitihani ya maisha huamua kuingia katika ulevi ili kupoteza mawazo? Bila shaka ni wengi, wengi, wengi sana, pengine ukiwemo na wewe…………….

  Waweza kusoma zaidi habari hiyo hapa:

  http://en.wikipedia.org/wiki/W_Mitchell


   
 2. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa-haya maisha haya!
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Huwa nikiwaangalia wale omba omba mitaani najiuliza maswali mengi..................Maana kuna wengine wana uwezo kabisa wa kujishughulisha na biashara ndogo ndogo na kujiingizia kipato, Kwa mfano kazi kama ya Shoes Shine au Shoes Maker kuna wale ambao wana ulemavu wa miguu tu, hawa wana uwezo mkubwa wa kujiingizia kipato kwa kazi hiyo kama wakiamu.
  Mtu anaweza kusema Serikali haijawawezesha, lakini kama wao wenyewe wakiamua wanaweza..........
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Asante sana Mtambuzi..ni kweli hatutakiwi kukata tamaa katika maisha ..
  Tunatakiwa kusonga mbele hata kama tumekutana na mikasa mingi
   
 5. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante baba kwa somo hili,

  Maisha ni safari ndefu,yenye mikwamo na misuko suko mingi,
  Ni kweli inatubidi tusikate tamaa bali ni kupambana na kusonga mbele.
   
 6. K

  Kimberley Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kweli maisha ni kusonga mbele na sio kukata tamaa katika hali yoyote ile na kwa uwezo wa Mungu tutafika!
   
 7. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hakika usemayo! Bila kupambana na mitihani ktk maisha daima mafanikio hugeuka kuwa ndoto! Ahsante kwa kuniongezea ujasiri wa kuthubutu!
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,089
  Likes Received: 6,555
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu kwa hilo somo,
  kwani unanisema ni mimi mama au kuna na wengine.
   
Loading...