Habari hii inaniuma sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari hii inaniuma sana

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by KakaJambazi, Jun 8, 2009.

 1. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  MWANAFUNZI mmoja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Dar es Salaam (Duce), ameuawa kwa kuchomwa kisu mara nne na mwanafunzi mwenzake kwa madai ya wivu wa mapenzi.

  Inadaiwa mwanafunzi huyo, Bertha Mwarabu, 23, wa mwaka wa pili, alitofautiana na mpenzi wake, Masamba Musiba, 27, katika masuala ya mapenzi wakiwa katika hosteli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu iliyopo Mabibo.

  Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 2:30 usiku kwenye varanda ya Jengo 'C' la hosteli hiyo linalotumiwa na wanafunzi wa kike na kiume, lakini mauaji yalifanyika katika upande wa wanawake.

  Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Bertha alifariki njiani wakati akipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Mwananyamala.

  Kalunguyeye alisema baada ya tukio hilo, Musiba alijeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na wanafunzi wengine na hivyo kukimbizwa katika hospitali hiyo hiyo kwa matibabu.

  "Musiba anashikiliwa na polisi katika kituo kidogo cha polisi, Mbezi jijini hapa," alisema Kalunguyeye.

  Inadaiwa Musiba alifanya tukio hilo baada ya marehemu Bertha kuvunja uhusiano wao wa kimapenzi.

  Kwa mujibu wa habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo, Musiba alichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa Bertha ameanzisha uhusiano mpya wa kimapenzi na mwanamume mwingine.

  "Baada ya Musiba kubaini hilo, aliamua kumwadhibu. Alimchoma kisu mara nne, kimoja katika ziwa la upande wa kushoto, mara mbili tumboni na kusababisha utumbo kutokeza nje na kingine alimchoma kifuani. Kisu hicho kilipinda na mpini wake ukaanguka chini," alisema shuhuda huyo ambaye alikataa jina lake kuandikwa gazetini.

  Habari zaidi zinasema wakati tukio linatokea, wanafunzi wengi walikuwa nje ya hosteli na hasa kwenye kiwanja cha mpira kilichopo eneo hilo wakiangalia tamasha la muziki.

  Habari zinasema kabla ya kumshambulia kwa kisu msichana huyo, Musiba alimwita Bertha kwa ajili ya maongezi ambayo alitaka yafanyike ndani ya chumba ambacho msichana huyo alikuwa akiishi na wenzake watatu. Ilikuwa majira ya saa 2:00 usiku.

  Wakati huo, Bertha alikuwa ametoka kujiandaa kwenda kuimba kwaya kwa ajili ya mazoezi ya Jumapili. Alikuwa ni mwanakwaya ya kanisa moja la Roma lililopo Bunju wilayani Kinondoni.

  "Ndipo akaitikia wito na wakakutana chumbani humo. Waliyoyazungumza hatukuweza kuyajua, lakini ghafla tulisikia kelele za mwanamke na tulipofika tulimkuta Bertha akiwa amejiegemeza kwenye ukuta na damu nyingi zikiwa zimetapakaa koridoni huku akiwa ameshikilia sehemu ya utumbo ambao ulikuwa umejitokeza nje," alisema.

  Mpashaji habari huyo alisema, Bertha alifanikiwa kuchoropoka chumbani mara baada ya kuonyeshwa kisu na alidondoka kwenye korido hiyo na ndipo zahama yote ikamkuta.

  "Kuna dada mmoja alikuwa chumba kingine ambaye alisikia purukushani na alipochungulia akamwona Bertha anagaragara chini, ndipo alipoanza kupiga kelele za kuomba msaada," alisema.

  Baada ya kufanya tukio hilo, Musiba alitokea kwenye moja ya dirisha na kuanza kukimbia, lakini baadhi ya wanafunzi waliokuwa chini ya ghorofa hilo walidhani kuwa ni mwizi na wakamkamata na kumpa kipigo.

  Inaelezwa kuwa matatizo ya kutoelewana kati ya wawili hao yalianza baada ya Bertha kubaini Musiba anatumia vilevi vya pombe, bangi na sigara.

  Inadaiwa kuwa Bertha alimkataza kuendelea kutumia vilevi hiyo kama alikuwa na nia ya kuendelea kuwa mpenzi wake, lakini hakujirekebisha.

  "Bertha alimpa miezi mitatu ili jamaa aache kuvuta sigara, bangi na kunywa pombe, lakini jamaa alishindwa masharti hayo na ndipo uhusiano wao ukavunjika," alidai mpashaji huyo.

  Taarifa tulizozipata kutoka kwa mtu wa karibu na Musiba zilidai kuwa, kabla ya kufanya tukio hilo, alinunua kisu kipya na alikusanya vitu vyake ikiwemo nguo.

  "Juzi alinunua kisu kipya na alipakia vitu vyake kwenye mfuko aina ya 'Volcano'. Wakati huo mimi nilikuwa sijui ana lengo gani" alisema mtu huyo bila kutaja jina lake.
  Uchunguzi unaonyesha kuwa, Musiba ni mwenyeji wa wilaya ya Musoma mkoani Mara, wakati Bertha ni mwenyeji wa Mkoa wa Morogoro.

  Source: Mwananchi Read News
  MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA,AMEN
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Poleni wafiwa.
  Haya ndo madhara ya mapenzi vyuoni ukipigwa kibuti lolote linaweza tokea mabrazameni msifie sana ukitoswa ndo unyofoe roho ya mwenzio?
  Poleni wote.
   
 3. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Poleni wafiwa,
  Hilo livulana lina usahamba,ujinga na mambo mengine mengi ndiyo yamemsumbua, kuachwa kitu gani bwana! wana wanakimbiwa na wake wa ndoa wanauchuna tu na maisha yanaendelea kama kawaida. Imethibitisha msemo wa wahenga kuwa "Mpumbavu akienda shule, anakuwa mpumbavu zaidi!" Apewe adhabu kali liwefundisho kwa wengine>
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,325
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Poleni wafiwa. Haukuwa uamuzi wa kiume kumchoma dada huyo kisu.Kama hakumuoa, alikuwa free kuanzisha relationship nyingine pale alipoona shaka na huyo jamaa.Suala la kuwa na mpenzi chuoni linataka umakini mkubwa maana presha zinaweza kupanda na kushuka bila utaratibu kama una roho ndogo.Pengine sasa anajuta kumfahamu marehemu maana msala alionao mkubwa
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mungu anajua zaidi yaliyowasibu watu hao wawili... Poleni wafiwa na has kwa Bertha kwani maisha yake na mtu aliyempenda.

  Simuonei huruma kabisa Musiba, ni upeo mfupi na siajabu ni matunda ya vilevi na hasa bangi

  Love stinks!!
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  imeniuma sana,
  sina la kusema juu ya hili.
   
 7. M

  Msindima JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  nawapa pole wafiwa,hii imenikumbusha nilipokuwa A level jamaa mmoja alikataliwa na mdada akaenda kunywa vidonge vya chloroquin,wanaume wenzake huko bwenini wakamkimbiza hospital,kwa hiyo hivi vitu vipo sana tu ila nachoona mimi ni kutokujiamini na kukubali matokeo,jamaa alipaswa kuyakubali matokeo na kuendelea na masomo kama kawaida,hapo alipo sasa anajuta na tayari mwelekeo wa maisha ndo umeishia hapo,uko mlango uko wazi kumkaribisha.
   
 8. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
   
 9. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  RIP Bertha.
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  musiba?

  wajita hawa jamani,au?
   
 11. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Its very bad kwa kweli....
  Unatoa roho ya mtu wakati si mke wako kabisa na hakuna ukweli kama mtaoana......
  SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE TU....

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI ... AMEN.
   
 12. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka mwaka fulani jamaa mmoja yeye baada ya kutemwa na demu ghafla akaenda kukumata line ya umeme ili afe bahati yake umeme ulikuwa haupo saa hizo. lakini baada ya miezi kadhaa akafa kwa heart attach. mambo ya mapenzi ni mazito ni kila mtu ana uwezo wake wa kuhimili. Sasa huyu bwana mdogo ukichanganya na bangi zake, pombe (na inawezekana gongo) pamoja na sigara. Wacha akanyee debe Segerea.
   
 13. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Akina dada, ni mambo ya mkoa wa Mara hayo!!!! Samahani sijaleta u-regionalisation hapa!!!! Kaeni chonjo. Ila ndiyo ukweli wenyewe kwa wanaume/wanawake 90% wana hasira/wakali hata kwa jambo la kutumia busara tu. Kwa bahati nimesoma nao, ni majirani, co-workers, halafu huwa wanajitapa kabisa mimi bwana...... ikiwa hivi....R.I.P Bertha binti mchamungu, alikuwa anasali Bunju Charismatic. Kwa mwana-charismatic wa kweli tabia kama zilivyoandikwa hapa huwa ni mwiko.
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  So bad indeed, ama kweli Mpumabavu akienda shule basi huwa mpumbavu zaidi....! Mungu Amrehemu Bertha
   
 15. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,800
  Likes Received: 2,480
  Trophy Points: 280
  Hawa jama wa musoma kweli kiboko yaani mpenzi tu unamchoma kisu na mahali hajalipa je angelipa mahali si angeunguza familia nzima ya marehemu Bertha?
  Dada zetu mnatakiwa kuwa makani na hawa watu sijawahi ona wala sikia.
   
 16. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Kuna tabia imezuka kwa vijana wa ki-.com. Wanaiga mambo ya kwenye movies.
  Siku hizi ukigombana na mpenzi wako, unaenda kuongea na rafiki yake ili mfanye "uhusiano fake" wa kumpa jelous. Isije ikawa dada huyu naye alifanya hivyo jamani. Wapenzi wengine hawaangalii tamthilia.
   
 17. GP

  GP JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  nasikia huyo Musiba nae ni msiba!
  yaani hivi tunavyoongea amefariki kutokana na kipigo alichokipata toka kwa wanafunzi wenzake akiwa anakimbia, ambapo walidhani ni mwizi wakamshushia kipigo cha haja, kafia hospitali.
  Mungu aziweke ahali pema peponi roho za marehemu
   
 18. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  mkuu omba radhi tafadhali.....jani hata siku moja halimfanyi kuw na akili za kihayawani namna hio.....pia ukila mjani huwezi kuwaza mashori.....mjani una hsshima yake mkuu.....tutake radhi..
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hehehe mkuu ndo maana mimi nahit na kurun tu maswala ya kufall in love noma mzee angalia sasa jamaa anakalia debe atajuuta kupenda. Hapo mpaka kesi yake ianze kusikilizwa ni kama baada ya miaka 2 atajuuta.
   
 20. GP

  GP JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mshkaji AMEKUFA!
   
Loading...