CRI Swahili
Member
- Dec 21, 2013
- 19
- 42
Habari wana JF,
Sisi China Radio International, Idhaa ya Kiswahili (CRI Swahili), tungependa kupata maoni yako juu ya habari ambayo unaamini ilikuwa habari kubwa kwa mwaka 2013. Aidha, habari 10 zitakazopigiwa kura/pendekezwa ndizo tutazitangaza kuwa habari 10 kubwa zilizopendekezwa na watanzania kupitia mitandao ya kijamii (JamiiForums ukiwa mmojawapo).
Wale watakaotoa maoni ambayo yanashawishi kuwa habari flani ilikuwa kubwa kwa mwaka 2013 na sababu zilizojitosheleza kuonyesha ukubwa wa habari yenyewe watazawadiwa na majina yao yatatangazwa kupitia chaneli yetu ya Kiswahili (CRI Kiswahili). Kuna zawadi takribani 15 na tumewasiliana na Uongozi wa JF ili ufanikishe utoaji wa zawadi hizo kwa washindi.
Tumependekeza habari 15, yawezekana hizi tulizopendekeza zikawa hazitoshi na kuna habari mnaona ingepeswa kuwekwa kwenye orodha, tutaikubali endapo utaambatanisha na sababu za kwanini habari hiyo iwekwe kwenye orodha na huenda ikashinda pia.
Habari 15 tulizopendekeza ni hizi:
1. Shambulizi la kigaidi kwenye jengo la Westgate mjini Nairobi
2. Kimbunga cha Haiyan nchini Philippines kilichosababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 6
3. Umoja wa Afrika kujadili uwezekano wa kujitoa ICC
4. Kifo cha aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela
5. Makubaliano kuhusu suala la nyuklia kati ya Iran na nchi tano wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama
6. Mgogoro wa Syria na tishio la Marekani kushambulia nchi hiyo baada ya kudaiwa kutumia silaha za kemikali
7. Kuondolewa madarakani kwa Rais Mohamed Morsi wa Misri na mgogoro uliofuata
8. Sakata la Edward Snowden na mpango wa upelelezi wa mawasiliano wa Idara ya Usalama ya Marekani (NSA)
9. Kufungwa kwa shughuli za serikali ya Marekani baada ya bunge kukataa kupitisha bajeti
10. Kupinduliwa kwa Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na mgogoro uliofuata
11. Kurushwa chombo cha anga ya juu cha China Change 3 na kutua kwenye mwezi
12. Kufikiwa kwa makubaliano ya biashara ya raundi ya Doha
13. Kupungua kwa tatizo la uharamia katika pwani ya Somalia na Ghuba ya Aden
14. Tukio la ubakaji nchini India lilisababisha kifo cha msichana mwanafunzi
15. Kufichuka kwa siri ya kutumia dawa za kuongeza nguvu kwa mwendesha baiskeli Lance Armstrong
Karibuni..
*Tembelea ukurasa wetu wa Facebook kila siku ili kuhabarika kuhusu hali ya China kwa dunia kwa lugha ya Kiswahili | Bofya =>> CRI Kiswahili