Haaoo: Watimuliwa kwa kutafuta kuomba uwaziri kwa JK

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
251
11
Akataa kuteta na wabunge

*Ni mpaka atangaze Baraza la Mawaziri

* Walikwenda kumwona warudi patupu

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

RAIS Jakaya Kikwete jana amekataa kukutana na wabunge na baadhi ya waliokuwa mawaziri hadi hapo atakapotangaza Baraza jipya leo.

Habari za kuaminika kutoka Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma, zinasema kwamba Rais Kikwete jana aliwaambia wasaidizi wake kuwa hataki kukutana na wabunge wala mawaziri waliopita hadi leo baada ya kutangaza kwa Baraza jipya.

"Rais amekataa miadi ya aina yoyote na wabunge na waliokuwa mawaziri mpaka Jumatatu baada ya kutangazwa kwa Baraza la Mawaziri," kilisema chanzo cha habari kutoka Ikulu ya Chamwino.

Habari zaidi zinasema kwamba jana kuna mbunge ambaye alikuwa waziri kamili alikwenda kwa lengo la kuonana na Rais, lakini alikataliwa kwa maelezo kuwa kiongozi huyo wa nchi ametoa maagizo kwamba ataonana na watu baada ya kutangazwa kwa mawaziri wapya.

"Huyu alikuwa waziri kamili, ni rafiki yake Rais, lakini amekataliwa kumuona na hii ni ishara kwamba hataki kuteua watu ambao ni rafiki zake," alisema.

Jana mchana Rais, Makamu wa Rais Dk Mohammed Shein walikuwa na kikao kwa ajili ya kuchambua majina ya watakaokuwa mawaziri.

Rais Kikwete alivunja Baraza la Mawaziri juzi baada ya kuridhia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na anatarajiwa kutangaza jingine leo na kuwaapisha Jumatano.

Katika maeneo mengi ya mji wa Dodoma, wabunge wamekuwa wakiuliza kuhusiana na majina yatakayokuwako katika baraza hilo.
 
Ina Maana watu wanajiendea ikulu bila ya kuomba appointment kwanza? kwani ikulu ni Supermarket? au ndiyo strategy za biashara hizo
 
kiele hele, walienda kumkumbushia JK jinsi walivyo mpigia kampeni na kuchangia pesa katika uchaguzi uliopita.
watoseeeee JK
waswahili usema, ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni asilani!!!
 
The Prezido yupo kwenye Conclave ? Poa wacha apike lakini we are working on pre empting him na majina ya mawaziri .Stay tune
 
Mkuu heshima.
naomba unifafanulie kuhusu post yako. ina maana vyombo vya habari na bunge vilitudanganya?? au muungwana kapiga chenga ya mwili??? Nipo njia panda mkuu

Kwa mujibu wa katiba Baraza la Mawaziri linavunjika by default Waziri Mkuu anapojiuzulu.Unless kama unasema rais kukubali resignation ndiyo indirectly anavunja baraza.Lakini ukiondoa indirect kick kilichovunja baraza ni kujiuzulu kwa PM.

Mimi nilifikiri anayemshauri rais kuhusu uteuzi wa mawaziri ni premier, sasa hawa mbona wanamhighlight makamu wa rais.
 
Back
Top Bottom