H. MOHAMMED G.DEWJI (MO) Amwaga Msaada wa Zaidi ya SHILINGI MILIONI 127

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,727
2,000

Mbunge wa Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na viongozi wa Mahakama ya Qadhi wakati alipotembelea Mahakama hiyo kuona namna inavyohudumia waumini wa Dini ya Kiislamu katika kutatua migogoro ya ndoa.

Sheikh wa Mahakama ya Qadhi, Ramadhani Kaoja akimweleza Mheshimiwa Mbunge shughuli za Mahakama hiyo pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili, Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Singida Mjini , Hamis Nguli, wa pili kulia ni Katibu wa Mahakama ya Qadhi, Alhajj B. Mlau.

Mbunge wa jimbo la Singida Mjini MO akisalimiana na waumini wa Msikiti wa Kata ya Mtipa wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Msikiti huo, ambapo mara baada ya kuona hatua zilizofikia za ujenzi huo aliahidi kutoa Mabati 50 pamoja na mifuko 50 ya Saraji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.

MO akitoka kukagua ujenzi wa Msikiti wa kijiji cha Mangwanjuki kata ya Mtipa.

Waumini wa Msikiti wa kijiji ch Mangwanjuki wakimsikiliza Mbunge wao Mheshimiwa MO.

Baadhi ya wapiga kura wa kijiji cha Mangwanjuki wakipeana mikono ya Kheri na Mbunge wao.

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Mwankonko darajani wakimsikiliza Mbunge wao (hayupo pichani) wakati alipoendelea na zoezi la kutembelea nyumba za kuabudu zilizopo jimboni kwake.

Jengo la wa Mwankonko darajani likiwa kwenye hatua Lenta, ambapo baada ya Mbunge kuona hatua hiyo ya nguvu za wananchi aliahidi Bati 50 na Mifuko ya Saruji 50.

Mheshimiwa Mohammed Dewji na baaadhi ya viongozi wa Msikiti wa kijiji cha Kisasida.

Mbunge MO akizungumza na waumini wa Msikiti wa Kisasida, ambapo ameahidi kutoa msaada wa Mabati 100 na Mbao 100 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Msikiti huo.

MNEC wa Manispaa ya Singida, Hassan Mazala akitoa hamasa kwa wakazi wa Kisasida kushiriki Mkutano wa hadhara ambao umeitishwa kwa ajili ya Katibu Mkuu CCM Taifa, Abdulrahman Kinana wa kuongea na wakazi wa jimbo la Singida Mjini utakaofanyika viwanja vya People’s Club.

Mheshimiwa Mohammed Dewji akielekea kukagua ujenzi wa Msikiti wa Minga mjini Singida.

Watoto wa Madrasa ya Msikiti wa Mwankoko Darajani wakimpokea Mbunge wao kwa mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati alipotembelea ujenzi wa Msikiti huo.

Mheshimiwa Mohammed Dewji akifurahia jumbe zilizoandikwa na watoto wa Madrasa ya Mskiti wa Mwankoko Darajani.

Hivi Kumbe mahakama za Kadhi zipo na zimeishaanza kufanya kazi?
 

peri

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
2,582
1,225
Mashaalah kazi nzuri ila isijekuwa ni gia ya kisiasa kwaajili ya 2015.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,707
2,000
..hii Mahakama ya Kadhi ndiyo kwanza naisikia.

..all this time nilikuwa najua suala hili lipo ktk majadiliano baina ya serikali na wawakilishi wa Waislamu.

..nini kinaendelea?
cc Ritz, Kadogoo, THE BIG SHOW
 
Last edited by a moderator:

Kashishi yetu

JF-Expert Member
Mar 22, 2014
2,371
2,000
Hakuwa Kwenye Ziara Ya Kuwatembelea Wananchi Wote Bali Ni Baadhi Ya Wananchi Wa Dini Ya Kiislam Ila Wapagani Na Wakristo Hawana Mbunge Wao Hvy Nao Waamke Watoe Mbunge Wao Atakaewapa Misaada Kama Wenzao Waislam Walivyopata Misaada Hy.
 

Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,649
1,225
Hizo pesa wataishia kudhulumiana na ndio utakuwa mwisho wa mahakama ya kadhi! Watu wenyewe wanaonekana, njaa kibao!
 

Mabulangati

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
792
250
Anafunika sukari na bidhaa nyingine feki anazosambaza hapa nchini. Hawa jamaaa bana daaaa!!!! Eeee baba Mungu uturehemu
 

Ruaha

Member
May 30, 2012
28
20
Kashishi uwe unafanya utafiti kwanza. Mo alitoa misaada kwenye makanisa, miskiti, shule na zahanati. Sasa udini upo wap hapo?
 
Last edited by a moderator:

swissme

JF-Expert Member
Aug 15, 2013
13,661
2,000
Pesa za kodi ya watanzania sio msaada warudishiwe wananchi pesa zao.muhindi huyo na si mtanzania.
 

Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,726
1,500
mkuu mchango wako umekaa kichuki zaidi. mbona tunaona viongozi wengi wanapita makanisani na kuchangia mamilioni ya hela mbona hamuongei? kuwa mstaarabu bhana. da!

Hakuwa Kwenye Ziara Ya Kuwatembelea Wananchi Wote Bali Ni Baadhi Ya Wananchi Wa Dini Ya Kiislam Ila Wapagani Na Wakristo Hawana Mbunge Wao Hvy Nao Waamke Watoe Mbunge Wao Atakaewapa Misaada Kama Wenzao Waislam Walivyopata Misaada Hy.
 

Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,726
1,500
mkuu ruaha watu wengine wanaishi kwa chuki. hawataki kusikia watu wa imani nyingine. ni chuki tu. hivi huyu mtu kweli ukimkuta ofisi ya umma atakuhudumia kweli japokuwa analipwa na kodi zako? badilikeni achaneni na vya kunyonga aka dhulma.

Kashishi uwe unafanya utafiti kwanza. Mo alitoa misaada kwenye makanisa, miskiti, shule na zahanati. Sasa udini upo wap hapo?

Mbona misikiti tu aende na makanisani aweke usawa.

Hakuwa Kwenye Ziara Ya Kuwatembelea Wananchi Wote Bali Ni Baadhi Ya Wananchi Wa Dini Ya Kiislam Ila Wapagani Na Wakristo Hawana Mbunge Wao Hvy Nao Waamke Watoe Mbunge Wao Atakaewapa Misaada Kama Wenzao Waislam Walivyopata Misaada Hy.
 

Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,726
1,500
Pesa za kodi ya watanzania sio msaada warudishiwe wananchi pesa zao.muhindi huyo na si mtanzania.
mkuu huyo anatoa hiyo hela lakini anajua pakuzipata. wengi wao hao ni wezi tu wa mali zetu ikiwemo kukwepa kodi.
kumbuka na hapo uchaguzi umekaribia halafu wanajifanya kupita kwenye madhabahu ili 2015 wapate pa kutokea.
nchi hii tuna safari ndefu sana.
 

Ruaha

Member
May 30, 2012
28
20
Sio watu wote wenye hela wana roho nzuri, wakarimu, wanahuruma na waelewa.
Ila kiukweli Mohammed dewji ni mfano wa kuigwa kwa wanaopenda maendeleo. Huyu mtu namkubali sana. Si rahisi ku-deal na biashara za kimataifa, kiwa mwanasiasa + chuki za siasa, kuwa social na kuinteract na watu wa aina zote, katika umri mdogo, sio rahis. WaTZ tuache kuangalia mabaya ya watu tu pale mtunanapofanya jema tumsifie. Hata ile kuwahamasisha vijana kujituma ni mfano mzuri. Kuna watu kazi yao kitukana kulaani na kuchukua umaarufu bar kwa kulewa, kwenda club, n kuwa na michepuko. Na bado watatukana na hapa.
Mo dewji 👊
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom