Gwiji la mauaji ya kimbari Theoneste Bagosora afariki gerezani

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,466
20,212
Kanali katika jeshi la zamani la Rwanda aliyepatikana na hatia kutokana na nafasi yake katika mauaji ya kimbali ya mwaka 1994 ambapo watu zaidi ya 800,000 waliuawa, amefariki gerezani nchini Mali ambako alikuwa akitumikia kifungo.

Théoneste Bagosora, mwenye umri wa miaka 80, alikuwa afisa wa ngazi ya juu katika wizara ya ulinzi ya Rwanda wakati mauaji hayo yalipofanyika.

Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya uhalifu kwa ajili ya mauaji ya Rwanda ilimpata na hatia na kumfunga kifungo cha maisha, lakini hukumu hiyo baadaye ilipunguzwa hadi kifungo cha miaka 35 jela.

Mtoto wake wa kiume Achille ameiambia BBC kuwa baba yake alifariki katika hospitali mjini Bamako, ambako alikuwa akipewa matibabu kutokana na matatizo ya moyo.

Watu zaidi ya 800,000 - wengi wao wakiwa ni kutoka jamii ya watutsi -waliuawa kikatili katika kipindi cha siku 100 ya mauaji ya kimbari.

Mauaji yalianza baada ya ndege iliyokuwa imembeba rais wa Rwanda wakati huo Juvenal Habyarimana kudunguliwa tarehe 6 Aprili 1994, na kuwauwa watu wote waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.

Bagosora alikamatwa miaka miwili baadaye Cameroon, ambako alikuwa ametorokea baada ya chma cha Paul Kagame cha Rwandan Patriotic Front kuchukua mamlaka.

Juni 1994: Wanajeshi w Ufaransa wakiwa katika doria wakipita kwenye umati wa wanamgambo wa Kihutu nchini Rwanda. Wanamgambo hao walitumika katika utekelezaji wa mauaji ya kimbari

CHANZO CHA PICHA,AFP
Maelezo ya picha,
Juni 1994: Wanajeshi w Ufaransa wakiwa katika doria wakipita kwenye umati wa wanamgambo wa Kihutu nchini Rwanda. Wanamgambo hao walitumika katika utekelezaji wa mauaji ya kimbari
Mnamo mwaka 2008, Mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Rwanda ICTR ilimpata na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu , na kupanga mauaji ya wanasiasa kadhaa , akiwemo aliyekuwa Waziri mkuu Agathe Uwilingiyimana.
Katika kesi yake, Bagosora alisisitiza kuwa alikuwa muathiriwa wa propaganda za serikali ya sasa ya Rwanda.
Jenerali Mcanada Romeo Dallaire, aliyekuwa Mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa kilichokuwa Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari, alimuelezea Bw Bagosora kama ''mfalme'' wa mauaji na akasema kuwa kanali huyo wa zamani alitishia.
Awali Bagosora alihukumiwa kifungo cha maisha, lakini miaka mitatu baadaye mashitaka yaligeuzwa na hukumu yake ikapunguzwa hadi kifungo cha miaka 35 gerezani.
Mapema mwaka huu ombi lake la kutaka aachiliwe mapema lilikataliwa, na alitakiwa kumaliza hukumu yake akiwa na umri wa miaka 89.
Alikuwa akitumikia kifungo chake katika gereza la Koulikoro nchini Mali pamoja na wafungwa wengine wengi kutokkana na mchango wao katika mauji ya kimba
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom