Uchaguzi 2020 Gwamaka: RPC Sweetbert Njewike mpuuzeni, Alex Jonas ni Katibu wa Jimbo la Manyoni Mashariki tangu Oktoba 2019

ABC ZA 2025

JF-Expert Member
May 2, 2018
1,156
701
Salaam,

RPC Njewike anapaswa kufahamu kwamba Alex Jonas ni Katibu wa Jimbo la Manyoni Mashariki na kwamba nafasi hii haikatazi yeye kufanya kazi ya Bodaboda.

RPC Njawike anapswa kujua kuwa katiba ya CHADEMA inaeleza wazi kuwa mwanachama wa chama chetu anapaswa kuwa na kazi halali ya kufanya mbali ya kuwa kiongozi au mwanachama wa CHADEMA.

Mbali ya kuwa kiongozi wa CHADEMA Alex Jonas alikua BODA BODA & Fundi cherehani na kwamba hii ndio ilikua kazi yake halali wakati wote.

Mbali na hilo hata ingekuwa kweli kwamba Alex Jonas ni boda boda tu na sio kiongozi wa CHADEMA bado haiondoi HAKI yake ya kuishi.

Tunalitaka jeshi la Polisi liendele kufanya uchunguzi wa kina kuliko kujiingiza katika siasa wakati huu tukisubiri taratibu za mazishi,


Gwamaka Mbughi.
Katibu CHADEMA kanda ya kati
Leo trh 27/02/2020

Pia soma: https://www.jamiiforums.com/threads...-bodaboda-na-sio-kiongozi-wa-chadema.1695825/

2) https://www.jamiiforums.com/threads...jonas-auawa-kwa-kukatwakatwa-mapanga.1695330/
 
Hawa jamaa ni wajinga sana sasa Kama ni dereva wa bodaboda ndio auwawe na jeshi lisichukuwe hatuwa, nimeamini hawamu ya tano ni janga la taifa
Hata wale wauaji wakati wa utawala wa Idi Amin hawangethubutu kutoa tamko la kishenzi kama hili lililotolewa na huyu msemaji wa hiki kikosi cha mauaji kinachosimamiwa na polisi na kulindwa na serikali ya awamu ya tano.
 
Back
Top Bottom