Gwajima Unakumbuka hii? Ngoja nawe Ukerwe utie akili

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
GWAJIMA UNAIKUMBUKA HII? NGOJA NAWE UKERWE

Na, Robert Heriel

Wewe uliwakera wenzako, uliwanyima mate kooni. Uliwachachafya mimbarini mbele ya waumini wako. Ulijisikia raha bila karaha. Tena kwa mdomo mpana hukuwa na simile wala machale ya kuwa nawe siku moja utaingia kwenye kumi na nane za unaowakera.

Ati ulisema ukweli, Ukweli?

Gwajima nitakukumbusha kidogo kidogo kero ulizowafanyia watu. Hii ni kero ya tatu.

Naomba ninukuu kukukumbusha;

"Dini ya kiislamu ni ya majini na niya mpinga Mkristo; Dini ya Kikatoliki niya kwenye nchi na niya nabii wa uongo. Shauri yako kama utakerwa, ila natakiwa nikusaidie"

Hata kama dini yetu iwe ya mashetani wewe inakuhusu nini?
Hata tuabudu majini na mizimu, wewe unapungua wapi?
Hata kama tuabudu mpinga Kristo inakukera nini?
Tukiabudu dini ya Nabii wa uongo inakuwasha washa nini?
Nani alihitaji msaada wako?

Unaita dini za wenzako ni za majini kwani walikuja kusalia kanisani kwako? Au walikuja nyumbani kwako kufanya ibada zao? Nini kinakukera?

Tunakubali sisi dini zetu ni za majini na mpinga Kristo, ya kwako ndio ya malaika na Yesu Kristo.
Tunakubali dini zetu niza nabii wa uongo ila ya kwako ndio ya nabii wa kweli.

Sasa kama ulitaka kutukera utasubiri sana.

Muda wa Kukerana umefika, wewe si ulijisikia raha kuongea na kupata sifa. Sawa. Subiri nasi tutajibu mapigo october.

Jambo moja nikupongeze, hongera Sana nilikuona na Mzee Pengo juzi juzi, Bila shaka ulimuomba msamaha.

Sasa unakazi ya kuomba msamaha wenye dini za majini na mpinga Kristo, wenye dini za Nabii ya uongo ambao umewataja wewe mwenyewe kwa jina kabisa.

Hivi huko Kawe hakuna wenye hizo dini ulizozitaja hapo juu? Kama wapo basi subiri Kukerwa.

Tumekubali sisi tunaabudu majini
Tumekubali dini yetu niya nabii wa uongo

Tukikuchagua ujue tumekubali kuwa dini zetu ndivyo ulivyozitaja

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mbona hapa bado kama ni ugoro basi upo puani mwendo wa chafya tuu infact the bygones will always be bygones we are talking of the present nt
 
Una jipya la jana au leo maana hii tumeshazoea ni bora ungetafuta kitu kipya in short mwambie huyo aliyekutuma kuwa sisi wanakawe wala hatuangalii mambo aliyoyasema kipindi hcho cha msingi n kuwa anaweza kutuwakilisha vema bungeni na kutuletea maendeleo hvyo hzi porojo zako hazitasadia kitu
 
Mkerekwa umepanik Sana inaonekana umevumilia vya kutosha ,sema umefeli ungeseka tangu alivyo wakera umekaa nayo mpka umepata uhakika wa kuwa mbunge ndo una kerekwa ! Mtuachie mbunge wetu tuna muelewa vibaya mnoo atusikii la kuambiwa apa tulipo tuna sikiliza mazuri yake tu ayo mabaya kaa nayo ndo kwanza nimesikia kwako Ayo mambo
 
Sasa kwa taarifa yako hao hao waislamu unao wasema wewe na hao wakatoliki ndiyo watamchagua kwa kura nyingi kuliko unavyodhani wewe.
Gwajima anakubalika kuliko akili yako inavyowaza.
 
Mkerekwa umepanik Sana inaonekana umevumilia vya kutosha ,sema umefeli ungeseka tangu alivyo wakera umekaa nayo mpka umepata uwakika wa kuwa mbunge ndo una kerekwa ! Mtuachie mbunge wetu tuna muelewa vibaya mnoo atusikii la kuambiwa apa tulipo tuna sikiliza mazuri yake tu ayo mabaya kaa nayo ndo kwanza nimesikia kwako Ayo mambo


Yeye mwenyewe anajua hatashinda, sasa inashangaza kwa wewe mpambe wake.

Subiri siku ya uchaguzi ndio utaelewa.

Hatupo kanisani hapa mpaka tutazame mazuri tuu.
 
Waislamu wenyewe wanaita wakristu makafiri kila mmoja anapohubiri kwake huwa anavutia mpande wake hivyo uache uchonganishi kwanza tumegundua kuwa hauishi Kawe na wala hauna mapenzi na Kawe lengo lako ni kutimiza ulichotumwa ili upate posho yako na sio kuwaonea huruma wanakawe ila umeshindwa maana Gwajima atashindaaaa kwa kishindooo kikuu
 
Gwajima hagombei ubunge wa dini, Hii ni siasa usiingizie mambo ya dini. Ya kale yameshapita tugange yajayo, Siwezi kufanya kosa tena la kumchagua Halima, tunataka maendeleo kwenye Jimbo letu la Kawe hivyo kura yangu nampa Gwajima.
 
Nikwambie tu ukweli kama ulikuwa hujui Askofu Gwajima anakubalika na wana Kawe na dini zote na atapita kwa kishindo hadi utashangaa na baada ya October 28 urudi tena na hii post yako tutakujibu tena.
 
Wachungaji wa zamani walikuwa muda wao wanautumia kwenda mahospialini kuombea wagonjwa na kuwapa chakula wasiojiweza kutoka kwenye sadaka, kwenda gerezani kuwapa injili wafungwa na walionewa kuwasaidia kutetea haki, kutembelea waumini wao kuwajulia hali, kutenga muda wa kukaa kwenye maombi kanisani, ila Sasa imegeuka wachungaji wanamuda mwingi wa kupoteza mpaka wanatafuta majukumu mengine ya kushinda bungeni.
 
Yeye mwenyewe anajua hatashinda, sasa inashangaza kwa wewe mpambe wake.

Subiri siku ya uchaguzi ndio utaelewa.

Hatupo kanisani hapa mpaka tutazame mazuri tuu.
Wewe n mtu mzima lakin hautumii akili yako vzurii hakika kama ungekuwa na akili za kukutosha usinge kaa na kuandika maneno kama haya mtu anayejielewa huwa hapigi kelele nyingi anasubiri tu siku akishindwa sasa wewe hizi kelele zako zinaashiria kuwa ameshashinda ndo maana Unaumia roho yako inatapatapa kama unataka kukata roho tulia wewe dawa iingie vizuri tumeshachoma shindano tunasubiri tu dozi ifanye kazi kawe mpya na Gwajima
 
Wachungaji wa zamani walikuwa muda wao wanautumia kwenda mahospialini kuombea wagonjwa na kuwapa chakula wasiojiweza kutoka kwenye sadaka, kwenda gerezani kuwapa injili wafungwa na walionewa kuwasaidia kutetea haki, kutembelea waumini wao kuwajulia hali, kutenga muda wa kukaa kwenye maombi kanisani, ila Sasa imegeuka wachungaji wanamuda mwingi wa kupoteza mpaka wanatafuta majukumu mengine ya kushinda bungeni.
Kila kanisa linautaratibu wake hyo huduma hata Gwajima anafanyaga na msichojua n kwamba yule n Askofu mkuu yuma yake kuna wachungaji wengi sana na wanafanya hyo kazi na hata yeye amefanya hyo kazi Mara nyingi sana
 
Back
Top Bottom