#COVID19 Askofu Gwajima anawapumbaza kondoo wake, muda si mrefu atachoma chanjo

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Gwajima leo nimemfatilia nimegundua hapa hakuna mtafiti ni utopolo na ujinga na sifa mdio vinamsumbua

Ibada nzima ilikua ni sifa kwa Rais samia tu, means ameshashtuka kuona ibada ilivyopita alimdhihaki sana lakini samia kapiga kimya

Mchungaji kaanza kupiga u-turn taratibu, ibada iliyopita aliuliza kwanini korona ije magufuli alipoondoka, sasahivi anakubali kua ipo na ameshaanza kuchukua tahadhari kwa kuweka mambomba ya maji kanisani kwake, anakili uwepo wa korona, hataki watu wachome chanjo ya JJ lakini hawambii watumie nn ili kuepuka korona isiwadhuru

Gwajima ameendelea kutuhumu kwamba chanjo ya JJ haifai kwa hali hiyo kumbe kuna chanjo zingine anazikubali tofauti na JJ

Tafiti za Gwajima hazijulikanagi anakozitoa mara ya kwanza kabisa aliwahi kusema corona inahusiana na 5G.

Sasahivi anasema waliochanja wapo sahihi ila yeye anawashauri kondoo wake wasichanje

Kondoo kazi wanayo.


Screenshot_20210731-084315.png
 
We ndo mshamba, jumapili iliyopita aliuliza chanjo wanayochoma wazungu ni Sawa na chanjo unayochomwa wewe ??? Akaongeza kama ni tofauti, hii tunayoletewa Sisi Una uhakika gani wa usalama wetu au kuna watu wamekula percent Kwa billgate?

Badala ya kujibu hoja mnakimbilia kumchonganisha na Raisi Wajinga kweli nyie
 
Gwajima hajabadilisha chochote kwenye maelezo yake, ninaweza ni si Support anachoamini, ila Hakuna mtu wa kujibu hoja zake!
 
Je, kajima ni mtumishi wa Mungu jibu ndiyo, ni Mungu yupi, ndio kuna mtihani hapo.
 
Gwajima ameshika akili za waumini wake. Hawana tena uwezo wowote wa kutafakari na kila anachosema wanapiga makofi. Wajinga ndiyo waliwao! Sidhani kama kuna muumini mwenye akili timamu pale kanisani.

Hizi ndizo technics wanazotumia watu sampuli ya akina Kibwetere. Kwanza wanachota akili za wafuasi wao zote na kinachofuta ni kuwa-manipulate kama wanavyopenda.
 
Mkuu sisupport ya Gwaji boy, ila leo amesema watu wafanye nn ili waepuke na Corona.
 
Gwajima ameshika akili za waumini wake. Hawana tena uwezo wowote wa kutafakari na kila anachosema wanapiga makofi. Wajinga ndiyo waliwao! Sidhani kama kuna muumini mwenye akili timamu pale kanisani. Hizi ndizo technics wanazotumia watu sampuli ya akina Kibwetere. Kwanza wanachota akili za wafuasi wao zote na kinachofuta ni kuwa-manipulate kama wanavyopenda.
ww umechanja??
 
Hata asipochanja, hawa Mazuzu wake wanatakiwa kufahamu jambo moja tu.

Leo hii Askofu Rasheed akifikia hatua ya kupumulia mashine, atapelekwa hata Ujerumani kutibiwa, wakati hao mazuzu watakuwa wanasubiria uwepo wa mitungi ya gas pale Mwananyamala Hospital
 
Mimi nilimtoa thamani kwa kuihusisha teknolojia ya 5G na covid-19. Huyu ni mhuni na tapeli kama wahuni wengine tu.
 
Back
Top Bottom