HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,413
- 6,134
Askofu wa makanisa ya ufufuo na uzima dunia Josephat Gwajima amwaga cheche. Amesema "Tanzania Mpya inakuja" Amesema alikuwa anajua Magufuli ni Mchapa kazi lakini anaichukia CCM, kwani hili dude hata kama malaika akiingia, anabadilika kuwa shetani.
Rais ameanza Vizuri, siku 60 za mwanzoni alikundua mambo mengi ikiwemo flow meter, Makontena. Inawezekanaje makontena yaingie Polisi wapo, Usalama wa taifa upo wasijue. Walijua sema walijua ni ya yule mzee.
Sasa amepata taarifa zake za kiufufuo kwamba wale watu waliokuwa wanaosafirisha Pembe za ndovu na kuingiza makontena bila kulipa ushuru, na wale walioruhusu Watumishi hewa, na wale walioharibu flow meter, Sasa wanazunguka Nchi nzima Kuwaambia watu wasimpe uwenyekiti wa CCM rais Magufuli sababu anatumbua sana.
Amesema wanataka wabadili utaratibu kwamba sio lazima rais awe Mwenyekiti wa Chama, kwani wanahofia kuharibiwa mambo yao.
Askofu Gwajima kamshauri rais kwamba, kama watafanya hivyo yaani kumnyima Uwenyekiti wa chama akubari, ila awape sharti moja la kupeleka Mswada Bungeni ili katiba ifanyiwe marekebisho Marais nao washitakiwe kwa yale makosa waliyotenda wakiwa madarakani.
Unafanya vizuri hata sisi ambao tulikuwa hatukupendi tunakupenda, sasa peleka mswada ili rais aondelewe kinga. Wapinzani watakubali.
Uanze na tembo, watuambie illikuaje Tembo wasafirishwe na rais yupo ilikuwaje, au makontena hayakulipiwa ushuru na rais yupo ilikuwaje.
Vilevile amemshauri kama wataendelea Kumsumbua, abadilishe chama, ahame chama na urais wake ahamie chama kingine kwani hata Malawi yalishawahi kutokea ambapo rais alihama na urais wake. Ahame tu kwani kanisa la Ufufuo na Uzima linamuunga Mkono.
Gwajima kasema ukisahau jina lake muite Mr. Tanzania.
Hatari sana leo. Ngoja nitafute namna ya kuweka clip