Gwajima amvaa 'nabii' Bushiri kwa kutabiri maovu juu ya Tanzania

Mie nilitegemea aje na neno la faraja kwa wahanga wa ajali ya huko Karatu , matokeo yake yeye anakuja na sizitaki hizi mbichi zake...Je nayeye wakitafutwa wale Nasema waliokuwa wanajifanya misukule na kulishwa unga wa ndele, atakuwa na la kusema kujitetea?
Mchungaji huyo alitabiroi kuwa Lowassa atafariki dunia na Uchumi wa Tanzania utakuwa na hali mbaya miaka ijayo, Gwajima amempelekea ujumbe akimtaka akae kimya upesi

Gwajima naye ni ngenga njaa tu kama Bushiri amesahau alivyotoa unabii Kuwa EL atashinda urais WA JMT na akatumia andiko la Biblia 'mene mene tekeli na pelesi'.
 
Mie nilitegemea aje na neno la faraja kwa wahanga wa ajali ya huko Karatu , matokeo yake yeye anakuja na sizitaki hizi mbichi zake...Je nayeye wakitafutwa wale Nasema waliokuwa wanajifanya misukule na kulishwa unga wa ndele, atakuwa na la kusema kujitetea?
Alitoa pia neno la faraja mkuu
 
Gwajima Amvaa Nabii aliyetabiri Kifo cha Lowassa, Atishia Kuwataja Hadharani Wanaopanga Kumuua

Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo amemvaa muhibiri maarufu wa Malawi anayefahamika kwa jina la Nabii Bushiri aliyedaiwa kutabiri kuhusu hatma ya uhai waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Katika moja kati ya mahubiri yake, Nabii Bushiri ambaye ni mzaliwa wa Malawi anayefanya kazi zake nchini Afrika Kusini, alidai kuwa ameona hali ya umauti ikimnyemelea Lowassa na kuwataka waumini wake kuomba ili awe na maisha marefu.

Akizungumza leo katika ibada kanisani kwake, Gwajima alilaani utabiri wa Nabii Bushiri, akidai kuwa amekodiwa na watu wenye nia mbaya ili atabiri ubaya kuhusu waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ili kufanikisha mpango wao wa kufanya tukio baya.

Gwajima alidai kuwa kwa uwezo wa kiroho, amewafahamu watu waliopanga kutekeleza njama dhidi ya Lowassa na viongozi wengine wa Serikali huku wakimtumia nabii huyo kuwaandaa watu kisaikolojia.

“Nataka nimueleze Nabii Bashiri kuwa nafahamu watu waliomkodi kufanya hivyo, na utabiri wake hautawezekana kamwe. Hakuna kiongozi yoyote wa serikali wala wa upinzani atakayekufa kwa utabiri huo. Wote wataishi kwa jila la Yesu,” alisema Gwajima ambaye leo alikuwa akihubiri kwa lugha ya kiingereza na kufasiriwa kwa lugha ya kiswahili.

Hata hivyo, Askofu huyo anayefahamika kwa kauli zake tata alieleza kuwa kwa uwezo wa kiroho amewafahamu watu waliopanga njama hizo na namna walivyoenda Afrika Kusini kukutana na mhubiri huyo kwa lengo la kumkodi atoe utabiri huo.

“Wanaweza kujiuliza nimewafahamu vipi. Roho yangu ilisafiri nao hadi Afrika Kusini, walivyokutana na Nabii Bashiri nilikuwa naye, yote waliyozungumza naye nayafahamu na hata walichompa ninakifahamu,”
alisema.

“Ninawafahamu kwa majina na walipo na ninawataka wakome mara moja kuendelea na mpango wao. Wasipositisha mpango wao huo, Jumapili ijayo nitawataja hapa wote kwa majina,”
alisikika Gwajima.

Gwajima alidai kuwa hamaanishi kuwa Bushiri sio mtumishi wa Mungu, lakini utabiri wake juu ya viongozi wa Tanzania ni wa kukodiwa.

Nabii Bushiri ambaye amekuwa akizua mijadala na hata kuingia katika mgogoro na baadhi ya nchi za Afrika, pia aliwahi kutabiri kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu Tanzania pamoja na tukio la tetemeko la ardhi nchini.
 
Nani hatakufa huko mbeleni maana kufa ni wajibu wa kila anaeishi mjinga huyo atuache tuage watoto wetu na walimu huko arusha na tz nzima kupitia clouds tv
 
Hivi inakuwaje mtu unadiriki kutaka kutoa roho ya binadam mwenzako simply kwa sababu ya ushindani wa kisiasa!!?

Kutabiri ni kutambua mambo ya ghaibu kitu ambacho binadam yeyote hana huwezo nacho hisipokuwa kutumia nguvu ya giza.

Hata siku moja sitoamini utabiri wa yeyote anayeitwa binadam.
 
Gwajima bana,kama anawafahamu si awataje bila ya simile?
Anachofanya Gwajima ni kurukia hoja na kuiweka kwenye hali tete ili kujaza wafuasi.
Alisema akikasirika atatoa vyeti vya makonda,akapiga pesa weee,mwishoni akaja na karatasi ya kufungia maandazi eti ni cheti
 
Gwajima bana,kama anawafahamu si awataje bila ya simile?
Anachofanya Gwajima ni kurukia hoja na kiweka kwenye hali tete ili kujaza wafuasi.
Alisema akikasirika atatoa vyeti vya makonda,akapiga pesa weee,mwishoni akaja na karatasi ya kufungia maandazi eti ni cheti
 
Gwajima Amvaa Nabii aliyetabiri Kifo cha Lowassa, Atishia Kuwataja Hadharani Wanaopanga Kumuua

Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo amemvaa muhibiri maarufu wa Malawi anayefahamika kwa jina la Nabii Bushiri aliyedaiwa kutabiri kuhusu hatma ya uhai waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Katika moja kati ya mahubiri yake, Nabii Bushiri ambaye ni mzaliwa wa Malawi anayefanya kazi zake nchini Afrika Kusini, alidai kuwa ameona hali ya umauti ikimnyemelea Lowassa na kuwataka waumini wake kuomba ili awe na maisha marefu.

Akizungumza leo katika ibada kanisani kwake, Gwajima alilaani utabiri wa Nabii Bushiri, akidai kuwa amekodiwa na watu wenye nia mbaya ili atabiri ubaya kuhusu waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ili kufanikisha mpango wao wa kufanya tukio baya.

Gwajima alidai kuwa kwa uwezo wa kiroho, amewafahamu watu waliopanga kutekeleza njama dhidi ya Lowassa na viongozi wengine wa Serikali huku wakimtumia nabii huyo kuwaandaa watu kisaikolojia.

“Nataka nimueleze Nabii Bashiri kuwa nafahamu watu waliomkodi kufanya hivyo, na utabiri wake hautawezekana kamwe. Hakuna kiongozi yoyote wa serikali wala wa upinzani atakayekufa kwa utabiri huo. Wote wataishi kwa jila la Yesu,” alisema Gwajima ambaye leo alikuwa akihubiri kwa lugha ya kiingereza na kufasiriwa kwa lugha ya kiswahili.

Hata hivyo, Askofu huyo anayefahamika kwa kauli zake tata alieleza kuwa kwa uwezo wa kiroho amewafahamu watu waliopanga njama hizo na namna walivyoenda Afrika Kusini kukutana na mhubiri huyo kwa lengo la kumkodi atoe utabiri huo.

“Wanaweza kujiuliza nimewafahamu vipi. Roho yangu ilisafiri nao hadi Afrika Kusini, walivyokutana na Nabii Bashiri nilikuwa naye, yote waliyozungumza naye nayafahamu na hata walichompa ninakifahamu,”
alisema.

“Ninawafahamu kwa majina na walipo na ninawataka wakome mara moja kuendelea na mpango wao. Wasipositisha mpango wao huo, Jumapili ijayo nitawataja hapa wote kwa majina,”
alisikika Gwajima.

Gwajima alidai kuwa hamaanishi kuwa Bushiri sio mtumishi wa Mungu, lakini utabiri wake juu ya viongozi wa Tanzania ni wa kukodiwa.

Nabii Bushiri ambaye amekuwa akizua mijadala na hata kuingia katika mgogoro na baadhi ya nchi za Afrika, pia aliwahi kutabiri kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu Tanzania pamoja na tukio la tetemeko la ardhi nchini.
Huyu Lowasa naona bado ana mapenzi makubwa sana na CCM. Angalia kitambaa mkononi kama bendera ya CCM. Kweli Fisi siku zote ni fisi habadiliki kuwa Mbwa.
 
Biblia inatufundisha kuwa mtawajua kwa matendo yao. Kwa hiyo hawa jamaa huwa wanalipwa? Sasa yeye kalipwa na nani?

Na washawasha!
 
Back
Top Bottom