Guterres alaani vita dhidi ya corona kutumika kuwalenga wakosoaji wa Serikali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,008
9,873
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezikosoa vikali nchi ambazo zinatumia kisingizio cha janga la COVID-19 kuwakandamiza wapinzani, vyombo vya habari na wakosoaji wa serikali.

Akizungumza kwenye kikao kikuu cha kila mwaka cha Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja huo mjini Geneva hivi leo, Guterres amesema kwamba serikali za mataifa kadhaa zimetumia vikwazo ambavyo viliwekwa kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona kudhoofisha upinzani wa kisiasa.Bila ya kuzitaja nchi kwa majina.

Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema baadhi ya wakati vikosi vyenye silaha kali vimetumwa kwa wapinzani, huku uhuru wa kujieleza ukigeuzwa kuwa ni tendo la kihalifu, na wakati huo waandishi na jumuiya za kiraia zikizuiwa kuripoti juu ya maradhi ya COVID-19. Guterres amewakosoa vikali viongozi wakuu wa nchi wanaotumia upotoshaji kulielezea janga hilo.
 
Back
Top Bottom