Guninita

Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,754
7,536
Sijui kama nimeandika jial hilo inavyopaswa, basi tuseme tu kuwa linafanana na jina la mtu anyeitwa John Guninita. Habari njema ni kwamba Ameamua kuanza masomo ya secondary. Wengi wamempongeza kwa maamuzi ya kijasiri.

Lakini watanzania sasa wamejua kuwa kiwango cha elimu yake kinaweza kuwa ndo sababu ya kuzungumza hovyo kuunga mkono ufisadi kwa kuwatetea mafisadi na kujaribu kuwakandamiza wanaoupinga ufisadi. Saa imefika kwa uongozi wa CCM kufanya uchunguzi (take stock) uwezo wa makada na viongozi wa CCM ktk ngazi mbali mbali. Haiingii akilini katika zama hizi kuwa na mwenyekiti wa CCM katika mkoa kuwa amekomea darasa la saba.

Vyama vyote viangalie visije vikaweka watu wenye elimu duni na upeo mfinyu, tusije tukaipeleka nchi pabaya.
 
watu dizaini ya gininita wako wengi, bunge la kenya limepitisha sheria ya kuwa waziri awe na angalau elimu ya shahada ya kwanza, sasa kwenye akina siye sijui tunafikiri nini
 
Saa imefika kwa uongozi wa CCM kufanya uchunguzi (take stock) uwezo wa makada na viongozi wa CCM ktk ngazi mbali mbali. Haiingii akilini katika zama hizi kuwa na mwenyekiti wa CCM katika mkoa kuwa amekomea darasa la saba.
Huko CCM kwani elimu ni kitu muhimu! Hivi hujasikia kisa cha mbunge anaitwa Chitalilo... si tu kuwa hana elimu ya kutosha, bali uchunguzi wa polisi ulithibitisha kuwa jamaa alighushi vyeti. lakini hadi hii leo ni mbunge na hakuna dalili kuwa atashughulikiwa
 
Tatizo la vyama vyetu mtu huwa mbaya pale anapoachana na chama. Habari ya elimu ya Guninita ilitolewa na Malecela miaka mingi iliyopita baada ya Guninita kuhamia CHADEMA. Nakumbuka mzee Malecela akisema wazi kuwa Guninita hakuwa mwaminifu kwani alidanganya hata kuhusu elimu yake. Ni Guninita huyuhuyu na elimu yake hiyohiyo aliyeonekana lulu huko CHADEMA na kutwishwa ukatibu mwenezi.
Cha kushangaza zaidi, karudi CCM na elimu yake hiyohiyo na kuukwaa uenyekiti wa mkoa.
 
Huko CCM kwani elimu ni kitu muhimu! Hivi hujasikia kisa cha mbunge anaitwa Chitalilo... si tu kuwa hana elimu ya kutosha, bali uchunguzi wa polisi ulithibitisha kuwa jamaa alighushi vyeti. lakini hadi hii leo ni mbunge na hakuna dalili kuwa atashughulikiwa

Mkuu Mpita Njia
Chitalilo ana kiburi kwa kuwa najua alitumwa kufanya ugaidi kwa watu na serikali ya CCM ndio iliyomchongea hivyo vyeti kumfunika awafanyie kazi vizuri. Sasa unataka CCM ijikamate yenyewe?
 
Nimesoma kichwa cha habari kwenye gazeti la HOJA kwamba Guninita anataka kulipwa shilingi bilioni 3 na IPP, nadhani inaweza kuwa inahusiana na habari hii kwa kuwa magazeti ya "umbea" ya IPP Media ndiyo ambayo yaliibua hizi habari. Mwenye details na hiyo kesi naomba atumwagie hapa ili tujue jamaa anadai bilioni 3 za nini.
 
Ugaidi gani? Hivi lakini CCM kwanini wanacheza na akili za watu? Chitalilo hana tofauti na mtu aliyeishia darasa la 7.

Au ndio maana JK aliwahi kusema kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba kulala usingizi? Maana maneno hayo aliyasema akiwa Jimboni kwa Chitalilo.
 
Raisi wa Jamuhuri ya Muungano: Guninita
Waziri Mkuu: Chitalilo
Waziri wa mambo ya nje: John Komba
waziri wa mambo ya ndani: Makamba
Waziri wa viwanda na biashara: hadija Kopa
 
Raisi wa Jamuhuri ya Muungano: Guninita
Waziri Mkuu: Chitalilo
Waziri wa mambo ya nje: John Komba
waziri wa mambo ya ndani: Makamba
Waziri wa viwanda na biashara: hadija Kopa
Waziri wa fedha na mipango: Richard Tambwe Hiza
 
Nimesoma kichwa cha habari kwenye gazeti la HOJA kwamba Guninita anataka kulipwa shilingi bilioni 3 na IPP, nadhani inaweza kuwa inahusiana na habari hii kwa kuwa magazeti ya "umbea" ya IPP Media ndiyo ambayo yaliibua hizi habari. Mwenye details na hiyo kesi naomba atumwagie hapa ili tujue jamaa anadai bilioni 3 za nini.

Mkuu Guninita anatafuta magunia ya kitita.Tatizo tu ni kuwa sina uhakika kama anafahamu kuwa katika bilioni moja kuna sifuri ngapi!!
 
Back
Top Bottom