Guninita: Bila Kikwete CCM Ingekuwa imezama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Guninita: Bila Kikwete CCM Ingekuwa imezama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzito Kabwela, Aug 20, 2012.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  [h=3][/h]
  [​IMG]


  MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita amesema kama siyo busara za Rais Jakaya Kikwete kukiongoza chama hicho, tayari kingekuwa kimesambaratika.


  Pia, Guninita ameonya kuwapo watu wanaotumia vibaya jina Rais Kikwete katika uchaguzi wa CCM unaoendelea nchini. Akizungumza Dar es Salaam na viongozi wa CCM Kata ya Mbezi Juu mwishoni mwa wiki iliyopita,Guninita alisema kuwapo kwa chama hicho licha ya wengine kudai kuwa kimepoteza mvuto na haiba mbele ya umma, kumetokana na busara za Rais Kikwete.


  Guninita alisema tangu Rais Kikwete ashike usukani wa chama hicho, kimepita kwenye mawimbi makali ambayo kama siyo busara zake yalikuwa yanakizamisha.


  “Amekuwa (Rais Kikwete) akitumia vikao kumaliza misuguano inayotokea kwa baadhi ya wanachama… tangu ashike usukani wa chama mwaka 2006, CCM imekumbwa na mawimbi mazito lakini busara zake zimeokoa jahazi kuzama,” alisema Guninita.


  Kuhusu baadhi ya wanachama wanaopita pita wakitumia vibaya jina la Rais Kikwete, Guninita aliwaonya kuacha mara moja kwa sababu ana uhakika hakuna aliyetumwa zaidi ni kuchafua jina linalo heshimika kwa wananchi.


  Alisema hali hiyo imesababisha watu wengine wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi kuogopa kujitokeza kuchukua fomu na kuzua malalamiko.


  “Ni haki ya kila mwanachama na kila kiongozi kugombea,huyo anayesema ametumwa na JKni mnafiki mpuuzeni,hata kwenye nafasi yangu jitokezeni hiyo ndiyo demokrasia,”alisema Guninita.


  Alisema mtu anayetumia jina la viongozi wakubwa licha ya kuwatisha wanachama wenzake, anakiharibu chama na kudhalilisha demokrasia. Pia,aliwataka wanachama wa chama hicho kuchagua viongozi bora wanaopenda kushirikiana na wenzao,ambao watakisaidia chama kushinde chaguzi mbalimbali.


  Mwananchi
   
 2. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Walewale. Wapo bize kupulizia mavi perfume!!
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Yani hata sijui nicheke au nilie kwa pumba alizoongea huyo jamaa
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sasa wewe GUNINITA baada ya kucheza cheza na SIASA sasa umekuwa eh; unataka KIKWETE akupe JIMBO LA KUGOMBEA UBUNGE?
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Mkuu umeniacha hoi leo....
   
 6. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,102
  Likes Received: 1,492
  Trophy Points: 280
  Kabla ya Kikwete CCm kilikuwa chama chenye nguvu pamoja na mapungufu kiliyonayo.Baada ya kuingia madarakani kwa kutumia mtandao wake sasa hivi hiki chama kimemeguka vipande na ni swala la muda tu kwa ccm kuondoka madarakani.
  Ngome kubwa ya ccm ilikuwa vijijini lakini sasa hivi hata vijijini wananchi wameanza kuikataa.Na hii yote imesababishwa na watu kama Guninita na Makamba badala ya kufanya kazi ya kujenga chama walifanya kazi ya kumtukuza mtu.
  Huyo Guninita ndio alikikimbia chama akiwa mwenyekiti wa umoja wa vijana baada ya kujiingiza kupendekeza ni nani wanaona wanafaa kuwa marais[umoja wa vijana haukuanza kutumika leo]Pia yeye na kina Lukuvi ndio walioua mradi wa mabasi ya wanafunzi.
   
 7. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti wa Chama.
   
 8. a

  afwe JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160

  Hayo mawimbi na misuguano ndani ya chama kasababisha nani kama sio udhaifu wa uongozi wake?
   
 9. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  CCM ina wenyewe na wenyewe ndiyo......................
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee bana
   
 11. Jimmy Romio

  Jimmy Romio JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 253
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Duh! LOVELY COMMENT!
   
Loading...