Gunia 1,515 za Korosho zenye thamani ya Tsh Milioni 160 zaibwa mkoani Mtwara

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,886
141,817
Mkuu wa mkoa wa Mtwara amesema korosho yenye thamani ya sh milioni 160 imeibwa katika ghala la kampuni moja mkoani humo katika mazingira yaliyojaa utata.

Upelelezi wa kina unaendelea.

Chanzo: ITV habari!

======

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linawashikilia watuhumiwa 14 kwa makosa mawili tofauti ikiwemo, tuhuma za kula njama, kuvunja ghala la korosho na kuiba gunia za korosho 1,515 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni miamoja na sitini mali ya Yalin Cashewnut Company. LTD.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Mark Njera amesema watuhumiwa tisa tayari wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kuvunja ghala na kuiba korosho, huku watuhumiwa watano wanashikiliwa na jeshi hilo kwa kosa la kupatikana na korosho zisizo na ubora.

Akizungumzia wizi wa korosho Kamanda Njera amesema kabla ya watuhumiwa kufikishwa mahakamani walikiri kufanya kosa hilo eneo la maghalani manispaa ya Mtwara.

Amesema kabla ya kubainika kwa tukio hilo walinzi wawili wa Kampuni ya Fumwa Security Campany Limited waliacha kazi ghafla bila kutoa taarifa yoyote kwa viongozi wao huku wakijua makosa waliyoyafanya kwa kushirikiana na wenzao.

Hata hivyo walinzi hao wamekamatwa na kuhojiwa na kukiri kula njama na kushiriki kuiba korosho kwenye lindo walilokuwa na dhamana ya kulilinda kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yao.

katika tukio la pili kamanda Njera amesema wanawashikilia watu watano wakiwemo viongozi wa chama cha msingi cha Mwembe Tongwa kwa kosa la kukutwa wakiwa na korosho zisizo na ubora gunia miamoja na ishirini na nne.

kufuatia tukio hilo amesema upelelezi bado unaendelea na ukikamilika watuhumiwa wote watano watafikishwa kwenye vyombo vya sheria na ametumia fursa hiyo kuomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kukomesha matukio ya namna hiyo.
 
Tunasubiri wenye kulipanua hili jambo ili tuweze kulielewa kimapana maana korosho sio kama madini kwamba kuna mtu kameza na kukimbia nayo panahusika makontena au malori
 
Naona sasa zile Bongo movie za utawala wa Meko zimeanza tena?

Bado nakumbuka vichwa vya treni vilivyookotwa bandarini, mamia ya magari yaliyookotwa bandarini nk.
 
Back
Top Bottom