Guinea yashumbaliwa kuchezesha madume Sauzi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Guinea yashumbaliwa kuchezesha madume Sauzi.

Discussion in 'Sports' started by Ehud, Nov 26, 2010.

 1. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Guinea yashumbaliwa kuchezesha madume Sauzi.

  Friday, 26 November 2010 09:39
  ABUJA, Nigeria

  SHIRIKISHO la Soka la Nigeria (NFF) limetoa malalamiko rasmi kwa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) ikidai kuwa timu ya wanawake ya Equatorial Guinea ilikuwa na wanaume wawili katika timu yake ya soka wakati wa mashindano ya Afrika yaliyomalizika Afrika Kusini hivi karibuni.

  "Malalamiko bado yapo. Tulituma malalamiko yetu CAF.Tunasubiri majibu," Msemaji wa NFF, Robinson Okosun aliliambia Shirika la Habari la Associated Press jana.

  Afisa aliyekuwa CAF hakutaka kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo.

  Equatorial Guinea ilikanusha tuhuma dhidi ya mshambuliaji na nahodha wake Genoveva Anonma na mshambuliaji Salimata Simpore, ikisema kuwa malalamiko hayo yametokana na kujisikia unyonge kwa wapinzani wao kutokana na mafanikio ya timu yao.

  Anonma, ambaye anacheza soka katika klabu ya Ujerumani aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza kuwa kwamba alishachunguzwa kuhusu jinsia yake, na anaona ni udhalilishaji.

  Equatorial Guinea imefunzu kucheza mashindano ya kombe la dunia kwa wanawake yatakayofanyika Ujerumaini mwakani baada ya kuwa mshindi wa pili katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika Afrika Kusini na kufungwa na Nigeria mabao 4-2 katika fainali.


  Ghana na Cameroon pia zilikuwa na mashaka kuhusu jinsia ya wachezaji hao lakini Shirikisho la Soka la Cameroon liliiambia AP kuwa halijatuma malalamiko

  "Hapana hatujafikiria kufungua kesi dhidi ya Equatorial Guinea," msemaji wa shirikisho hilo, alisema Junior Binyam.

  Equatorial Guinea ilitwaa ubingwa wa Afrika
  mwaka 2008 baada ya kuitoa Nigeria katika nusu fainali na kuwa nchi nyingine mbali na Nigeria kutwaa ubingwa huo.

  Baada ya kutwaa ubingwa huo timu hiyo pia ilituhumiwa kuchezesha wanaume katika mashindano hayo.

  " Tuhuma kuhusu kuwepo wachezaji wa kiume kwa ujumla hakuna ukweli," Shirikisho la Soka Equatorial Guinea lilisema kwenye taarifa yake Jumanne. "Tunachukulia habari hiyo kama ni ushahidi wa kujisikia unyonge.

  CAF inatarajia kuchukua hatua kwa kuliweka sawa suala hilo ili malalamiko kama hayo yasitokee wakati wa fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake.

  Malalamiko kama hayo, yaliikuta nchi ya Afrika Kusini baada ya mkimbiaji wake Caster Semenya kushinda mbio za meta 800.

  Semenya aliyetuhumiwa kuwa mwanaume, amekuwa akikimbia riadha na wanawake, alilalamika kufanyiwa uchunguzi wa jinsi yake na Shirikisho la Kimataifa la Riadha na Julai alisafishwa rasmi kutambulika kuwa ni mwanamke.
   
Loading...