Guilty until proven innocent | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Guilty until proven innocent

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by ruby, Jun 14, 2009.

 1. r

  ruby Member

  #1
  Jun 14, 2009
  Joined: Jun 13, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwenye nchi za wenzetu, it is true that a person is innocent until proven guilty, kwenye nchi zetu it is the opposite. Ni lini tutafika? Kwa nchi kama marekani mtu hawezi kukamatwa akawekwa ndani mpaka wawe na ushahidi wote, kwetu wakikuhisi tu ndani, ukipelekwa mahakamani kila siku ushahidi haujakamika. Bado nauliza tena hivi lini tutafikaaaaaa?
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  You are innocent until proven guilty in the court's of law.

  With mentality za kiafrika, sio rahisi. USA Mtu kusema kuwa navuta bangi au kula madawa sio kosa, kosa ni kukamatwa na hizo controlled substance. Bongo ukionekana una-rasta tu, ujuwe lupango ni kwako.

  There are so many laws which needs amendments, lakini labda mazingira na utamaduni unazuia hizo amendments kufanywa na/au Serikali haioni umuhimu wa kufanya hizo amendments na/au serikali za afrika hazijali watu wake.
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Position ni kuwa hata hapa kwetu ni hivyo. Katiba yetu ya mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa ina kitu kinaitwa presumption of innocence. See Article 13 ( 6 ) (b).

  Tatizo liko kwenye vyombo vya upelelezi eg polisi, takukuru etc, bunge, mawakili na mahakama.

  Tatizo lililopo ni jinsi gani wapelelezi wa kesi wako mahiri katika kupeleleza kesi zao. Sheria zetu zinaruhusu dhamana wakati wa upelelezi ( police Bail), hii inasaidia mshukiwa pupewa dhamana wakati upelelezi unaendelea vile vile dahamana wakati kesi inaletwa mahakamani( bail pending trial) na hata dhamana endapo utapatikana na hatia ( bail pending appeal).

  Tatizo lingine ni bunge, awali makosa amabayo yalikuwa hayana dhamana yalikuwa mauaji na uhaini lakini sasa hivi tunaona wigo wa makosa yasioyo dhamana umeongozeka kamavile wizi wa kutumia silaha, makosa ya kujamiiana, wizi wa fedha ambapo ili kupata dhamana lazima uweke nusu ya hela ambayo imedhaniwa imeibiwa.

  Tukiangaliana sana vifungu vinavyozuia dhamana vinakinzana na katiba na sheria inatamka wazi kuwa katiba ni sheria mama, hivyo ni juu yetu kuiomba mahakama kutengua vifungu ambavyo vinakinzana na katiba. Mpaka leo ni watu wachache wamekuwa na ujasiri wa kufanya hivyo.
   
Loading...