Gubu linavowatafuna wapinzani wa Liverpool

hii kauli klopp hakuisema 2015..aliisema mwanzo wa msimu wake mpya akiwa anaongezewa mkataba akasaini miaka 6 huku akiwa amekaa Liverpool kwa miezi kadhaa tu...alivyosign mwaka 2016 ndio akaahidi miaka 4 ya kujenga tim na atakua ameshinda taji ndani ya miaka hio

Aliisema kwenye interview yake ya kwanza kabla hata hajaanza mazoezi.

Rudi YouTube utazame.
 
Nimeangalia kweli alisema mwanzoni nilikosea...lakini pia nimenotice hakusema premier league au ikiwa title inaulazima wa kua PL?

I doubt hujaisikia interview vizuri, swali liliulizwa specific for premier league.

Kama umesikia kuna mahali ilitajwa long wait ya PL ndo akajibu vile.
 
Mengine yote yanaweza kuwa kweli, lakini pakikosewa popote the whole story inakuwa fake. Wachezaji aliowakuta Klopp na bado wapo ni zaidi ya wanne uliowataja.

1. Firmino 2. Lalana 3. Henderson 4. Origi 5. Milner 6. Joe Gomez 7. Lovren 8. Bila kuweka walioko kwa mkopo
Katika hao 7 wote wanaweza kuanza kikosi cha kwanza kwenye mechi yoyote.
 
Mugosha! Origi, Lallana, Lovren hao ni sub tena wanahusishwa kuondoka!!!
Origi hapana,wanaohusishwa na kuondoka ni lallana, Loren ambao mikataba yao ipo ukingoni na klopp anataka apate watu sahihi maana Jan next year salah na Mane watarudi kwenye afcon so watakosa game 5 mpaka 6 za epl kwa Jan-feb so anataka apate pesa kidogo then alete watu sahihi na target kubwa ni timor Werner.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndani ya misimu minne ntashinda taji moja. Ndivyo Klopp alivowaambia waandishi wa habari misimu mitatu na nusu iliyopita. Jamier Ghalagher alimuonya Klopp kuwa siyo rahisi kihivyo na ni kosa kubwa sana kuahidi taji ndani ya misimu minne.

Alianza na mfumo wake wa gegen pressing kwa wachezaji plastic kama Sturidge alishindwa kabisa, wazito kama Benteke walikoma! Maumivu ya misuli yalishamiri ndani ya kikosi na madaktari wa viungo walimponda sana Klopp hata Ferguson alidiriki kusema hajawahi kuona tim ina press muda wote. Klopp alijibu kirahisi kuwa anahitaji msimu mmoja kuweka msingi wa utimamu wa mwili wa wachezaji wake.

Hakukurupuka kusajili kwa bei bali alianza kuingiza falsafa yake pole pole kwa wachezaji aliowakuta huku akiwauza wale walioshindwa na kuwaingiza wapya pole pole ndani ya timu. Hadi sasa ni wachezaji wanne tu wa kikosi cha kwanza aliowakuta wamebaki ndani ya kikosi na hata hivyo hawana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza. Adam Lallana, Jordan Henderson, Firmino na Origi ndiyo pekee waliobaki katika kikosi cha Klopp.

Ninapoandika huu ni msimu wa tatu na nusu kwa Klopp na ameshatwaa mataji makubwa matatu yaani UCL, FIFA CLUB W.CUP na UEFA SUPER CUP amezidi matarajio ya mashabiki wa Liverpool na sasa anaongoza ligi kwa point 13 akiwa na mchezo moja wa kiporo dhidi ya Westham.

Huyo ndiyo Klopp alietaka kuwageuza wasio na imani wawe na imani na timu yao, wakati sherehe zikishamiri mashabiki pinzani wamebaki na gubu mioyoni mwao huku wakisingizia teknolojia ya video eti inawabeba Liverpool. Wamesahau kuwa TAA amebadilishwa kuwa Kevin Debruyne, Robertson kawa Marcel Henderson kwa makelele n.k. Unathubutu vipi kusema liva inabebwa kwa VAR? hamuoni MANE, SALAH na FIRMINO wanavyofanya kazi yao? Hamuona Gini na Hendo wanavyokaba?

Hamuoni Origi alivo super sub? Acheni uchawi, Furahieni angalau mmebahatika kuona kikosi bora zaidi katika historia ya EPL. Liver hii inaenda kutawala EPL kwa miaka kumi.

Mashabiki pinzani mjilaumu wenyewe kwa tim zenu kufanya maamuzi ya hovyo!kwa mfano eti leo Ancelotti yupo Everton halafu man utd wamemkumbatia Ole wakati Massimiliano hana timu nyie mnampa Arteta timu, wakati Mourinho yupo Spurs. Chelsea eti ina Lampard. Huo ni uhuni ambao hata Masau Bwire hawezi kuufanya hapa Bongo.

Nawashauri furahieni maisha ya soka kwa kuishangilia Liverpool hii ya mabingwa ya Mjerumani JURGEN NOBERT KLOPP.

Hajasajili wachezaji wa bei?
Pengine hajasajili kuliko Man U na Man City ila Mpunga nao wametoa mrefu sana wamevunja Record za dunia mara 2.
1. Van Djik kama Beki ghali zaidi duniani
2. Allison kama GK ghali zaidi Duniani.

Ya Van Djik imevunjwa na Maguire ila bado Ni namba 2.

Ongezeka na Salah, Fabinho, Keita Etc. Kifupi wamespend kama 300M hivi kwa wachezaji kama 6 kwa muda mfupi.
 
Hajasajili wachezaji wa bei?
Pengine hajasajili kuliko Man U na Man City ila Mpunga nao wametoa mrefu sana wamevunja Record za dunia mara 2.
1. Van Djik kama Beki ghali zaidi duniani
2. Allison kama GK ghali zaidi Duniani.

Ya Van Djik imevunjwa na Maguire ila bado Ni namba 2.

Ongezeka na Salah, Fabinho, Keita Etc. Kifupi wamespend kama 300M hivi kwa wachezaji kama 6 kwa muda mfupi.
MKUU

Baada ya kumuza coutinho KWA paundi million 142 ndio van dyke 75 milion na Allison 65 milion jumla 140 milion!tunauza kwanza ndio tunanunua pia Benteke 32.5,One 15 million na wengineo tuliuza ndio mane na salah KWA paundi 30 plus KILA MMOJA!!
 
MKUU

Baada ya kumuza coutinho KWA paundi million 142 ndio van dyke 75 milion na Allison 65 milion jumla 140 milion!tunauza kwanza ndio tunanunua pia Benteke 32.5,One 15 million na wengineo tuliuza ndio mane na salah KWA paundi 30 plus KILA MMOJA!!
ila mlivunja record za dunia mkuu, na hata sasa hivi mumemsajili Nunez kwa hela ndefu na addons ambazo zinalipika kirahisi kabisa. nakumbuka 2016 wakati tunamsajili pogba Klop alisema hatafundisha ikiwa timu yake inasajili mchezaji kwa 100m kama Pogba.

FVD2dvtWUAAwSh2.jpg
 
Back
Top Bottom