Grudge: Tanzania Tomorrow and CCM era Today .....Take note

Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,169
10,785
Kuwa hali hii ambayo watu wanawaona watanzania kuwa ni wapole, sio wachukuaji hatua, si wasikivu, wanafanya uchaguzi m'baya, wako goigoi n.k si kweli?!!

Watanzania hawa hawatazionyesha hasira hizi leo, watanzania hawa wameumizwa, wametumikishwa, watanzania hawana raha, hata wanaoonekana wana magari ya kifahari, bado sura zao zinaonyesha ukiwa na upweke! Watanzania wamedharauliwa, wamenyimwa haki ndani ya nchi yao. Watanzania wameuawa kwa makusudi , watanzania hawajui kesho, kesho yao ni juu yao.

Viongozi waliowaamini wamewauza. Watanzania hawa wana gubu, wana uchungu, akina mama wanajifungulia barabarani huku wengine wakiponyeshwa mafua Malaysia. Watu wanakufa na wataendela kufa kwa uzembe wa serikali. Mgao wa umeme unapandisha maisha juu, mgao wa umeme unaturidisha miaka ya 60! Mgao wa umeme ni laana.

Maumivu haya yamejificha, imekuwa kama jua linaloweza kuonekana saa kumi alfajiri. Maumivu haya yanatibiwa juu juu, wafariji wakubwa wa watanzania ni magazeti , yaliyoachiwa huru kama njugu kusema lolote, ikiwa ghiriba ya watawala kufanya hivyo ili kuonyesha dunia kuna demokrasia Tanzania! Faraja ya watanzania ni nakala za magazetini, faraja za watanzania ni michezo, shughuli za kijamii na nyumba za ibada na mitandao ya kijamii kama FB, blogs ns sie JF!, si maneno ya faraja, ya hekima, ya kimapinduzi na ya kuongeza motivationa makazini na mashambani. Hatuna viongozi ambazo tuanweza kuyatumia maneno yao katika kuamsha vipaji na kufanikisha malengo yetu. Hatuna akina Nyeyere type ambao wanaweza kukuliza na kukuchekesha at the same time, yet ukijivunia kuwa mtanzaniaTaifa la Tanzania halipo kwa sasa, hatuna sura ya utaifa tunao wanyang'nyi na wanaowaza matumbo

Kidonda hiki kisipopona haya yanatatokea na yatatokea!

1. Watu wataendelea kutoaminiana na kuzushiana

2. Ufisadi na utaendelea

3. Wenye malengo mema watashukiwa kuwa wana ajenda zao za siri hivyo kutofanya lolote lile

4. Utaifa utapotea na hali ya shamba la bibi litaendelea

5. Kukata tama kwa watu kutaongezeka hivyo matumizi ya madawa ya kulevya, kujiuza-umalaya, kutaendelea

6. Watu wa hali za binadamu watakuja kwa sura nyingine, ushoga na abortion vitaruhusiwa na serikali kama njia ya kuwafurahisha minority kwa sababu wameshindwa kuwatumikia majority.

7. Matajiri watachukiwa hata kama fedha wamepata kihalali

8. Social gaps yataongezeka, wengi watakata tama ya kufanikiwa!

9. Watu hawatajitokeza kupiga kura..kwani kura will be a wastage of time as it is now!

10. Any slight force may result into a war of its kind

11. Kutokana na poor system ya elimu watu watageuka watumwa ndani ya nchi yao

Kumbuka hali hii itatokea hata kama CCM itaondoka madarakani, endapo chama kitakachokuja kitashindwa kuwaponya watanzania, hali hizo hapo juu zitaendelea.Mwezi mmoja baada ya kushika nchi, lisipofanyika jambo la kuwaponya watanzania, wengi wataendelea kuumwa ugonjwa huu wa hatari.

TIBA

1. Kuwakamata woote waliohusika kufanya grand corruption, kuwafungulia mshtaka na warudishe fedha za wananchi

2. Kufuta mikataba yote mibovu ambayo serikali iliingia

3. Kuwapa wananchi katiba ambayo inawapa mamlaka makubwa wao waamue hatima ya nchi yao

4. Kufanya jambo au kitu kuleta utaifa na hivyo kila mmoja kujivunia taifa lakeHaya manne makubwa yasipofanyika hakuna chama
chochote kiwe CCM au upinzani watakaoweza kutawala Tanzania kwa amani.

Tunakidonda , tumeumizwa!
 
Kumbe una akili heee.Mwanzoni ulikuja kututibua na huku unajua CCM ni majambawazi wakubwa .Umesamehewa uliyo ropoka kule na hapa umesema mimi nakubaliana nawe .
 
This are the things we want to hear from great thinkers, and not Personal affairs of a person
 
Acha kueneza uchochezi wewe, amani ya hii nchi imegharamiwa na ni mpumbavu tu ndiye atathubutu kuipima uimara wake. Matatizo ya hii nchi kama ugumu wa maisha ni ya Dunia nzima na hakuna sababu ya msingi ya kumlaumu Kikwete na Serikali. Kitu muhimu ni kuendelea kumpa muda na mabadiliko yatakuja tu yenyewe.
 
Nyie ndio mnaomzidishia mzigo Kikwete kwa kudhani mnamsaidia.
 
Umeandika kwa hisia na uchungu na hii ni ishara ya uzalendo ulio nao.mawazo yako ni ya kimapinduzi zaidi.

Sishangai kuona wewe ni mhandisi, maana hayo unayoyapendekeza katika ulingo wa siasa wala hayana nafasi.
Labda kwa mitutu ya bunduki..

Lakini pia kisheria na kikatiba huwezi kufuta mikataba au kukamata watu kama unavyodhani..
Ila angalizo ulilotoa juu ya muelekeo wa haya matatizo ni la kuzingatia.
 
Kumbe una akili heee.Mwanzoni ulikuja kututibua na huku unajua CCM ni majambawazi wakubwa .Umesamehewa uliyo ropoka kule na hapa umesema mimi nakubaliana nawe .

Hivoo...mkuu tangu nimejiunga JF i feel more comfortble kuwa huru , na kuamini ninachokiamini, na kusema ninavyowaza, sidhani kama nimemkosea mtu!
 
Acha kueneza uchochezi wewe, amani ya hii nchi imegharamiwa na ni mpumbavu tu ndiye atathubutu kuipima uimara wake. Matatizo ya hii nchi kama ugumu wa maisha ni ya Dunia nzima na hakuna sababu ya msingi ya kumlaumu Kikwete na Serikali. Kitu muhimu ni kuendelea kumpa muda na mabadiliko yatakuja tu yenyewe.
you better stick to what you do best - womanizing!!!
 
Acha kueneza uchochezi wewe, amani ya hii nchi imegharamiwa na ni mpumbavu tu ndiye atathubutu kuipima uimara wake. Matatizo ya hii nchi kama ugumu wa maisha ni ya Dunia nzima na hakuna sababu ya msingi ya kumlaumu Kikwete na Serikali. Kitu muhimu ni kuendelea kumpa muda na mabadiliko yatakuja tu yenyewe.

Masikini we! Unadhani dunia nzima ina matatizo kama ya Tanzania? Huo umeme na maji mnakosa nyie, sio dunia nzima. Toka kidogo ufungue macho.
 
Wabongo kama kunawatu tunatakiwa tuwalaumu na tuachane na mahela yao ya mkopo ni IMF na world bank hawa ndio mafisadi wakubwa tokea tupate uhuru wamekuwa wanatuendesha na remot contole na malimbikizo ya madeni. Yaani haya mashirika mawili na washenga wake hutupaga kama milioni kumi alafu ukiangalia kwaundani zaidi ni wanatoa kwa kifungu kifungu kwa miaka kama kumi. Alafu watatuletea yale malandcruser ya hard top alafu yote yatahesabiwa kwenye hiyo hela ya mkopo. Alafu watawaleta wale watu wanaowaita expart wao na wawalipe kama tsh200,000,000 for only few months work in bongo kila mwaka. Haya siye twabakia kulalamikia serikali, tutafika kweli. Mtu yoyote anayejua mambo ya mahesabu ataelewa milioni kumi ya leo ni tofauti na ukipewa kidogokidogo kwa miaka kumi. Alafu siye tutalipia riba ya milioni kumi wakati ela tuliyopata siyo sawa na milioni kumi.
 
Back
Top Bottom