Greta Thunberg: Mwanaharakati anayefuta maono ya JK Nyerere

Teknocrat

JF-Expert Member
Oct 20, 2018
3,816
8,452
Greta Thunberg ni Mwanaharakati mtoto wa mazingira na madiliko ya tabia nchi anayefuta maono ya yaliyozungumzwa na Raisi wa kwanza wa Tanzania JK Nyerere miaka zaidi ya ishirini iliyopita, na ni wakati hata Greta mwenyewe hajazaliwa.

Huyu mtoto mdogo anapigania utunzaji wa mazingira duniani na kulinda rasilimali asilia za dunia kuharibiwa na mataifa makubwa duniani yenye uchu wa kutumia rasilimali za asili kujitajirisha na kujilimbikizia maendeleo huku wakiacha uharibifu mkubwa wa mazingira na vyanzo vya rasilimali asilia.

Greta Thurberg hali nyama, na hapandi ndege na kuna wakati alisafiri na mashua ya upepo kutoka Sweden kwenda USA kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu kulinda mazingira ili kuepusha mabadiliko ya tabia nchi yanayo sababisha majanga ya kiasili zaidi kwenye nchi masikini dunia.

MW-HW738_GretaT_20191211105312_MG.jpg

10459202

Msikiliza JK Nyerere alisema nini zaidi ya miaka ishirini iliyopita
 
Hivi hakuna viongozi wa sasa wanasikiliza hizi hotuba? hivi sijawahi kusikia kiongozi yeyote anazungumzia tupande miti kwa wingi mpaka wahisani waje kutuletea kwahisani ya............nk.
Hapo tutaweka bonge la sherehe ya ufunguzi wa mradi kwahisani ya.............Mayo weeeeeeeeee!!!
 
Wanapiga hata hizo hela za misaada ndio maana wanashangilia...

Mimi nimeona huu ukweli wa mabadiliko ya tabia nchi mkoa wa Shinyanga ambao ulikuwa unaongoza kwa kilimo cha pamba, baada ya kumaliza miti yote sasa maeneo mengi ni nusu jangwa na ukame mbaya sana....
 
Aisee umenikumbusha kitu niliona Kishapu kaaaa!!!
 
Sasa mbona kichwa cha habari umeandika mwanaharakati anayefuta badala ya anayefuata maono ya Nyerere? Rekebisha kichwa cha habari.
 
Back
Top Bottom