TANZIA Gregory Teu aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Viwanda, Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Mbunge wa Mpwapwa, afariki dunia

Mimi ndio maana sikuwa naenda kukusanyika kwenye ile mikutano ya kampeni, mtu anakwambia et Corona ilipungua sasa kama Corona ikipungua ndio mkusanyikane vile bila hata barakoa? usikute zile nyomi za Magufuli na Lissu walizokuwa wanashindana ndio zimeleta nimonia.
 
Mbunge wa zamani wa Mpwapwa mkoani Dodoma nchini Tanzania Gregory Teu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo (Januari 25, 2020) baada ya kujisikia vibaya akiwa katika cha Bodi ya Kampuni ya Maendeleo ya Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO).
Gregory Teu

GREGORY TEU​


Tanzanian politician
Mpwapwa. Mbunge wa zamani wa Mpwapwa mkoani Dodoma nchini Tanzania, Gregory Teu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kujisikia vibaya akiwa kikaoni.

Akizungumza leo Jumatatu Januari 25 2020, Msemaji ukoo wa Teu Stanley Mbijili amesema Teu alikuwa kwenye kikao cha bodi ya Kampuni ya Maendeleo ya Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO) New Board Chairman appointed for Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO). ambacho yeye ni mwenyekiti wake.

Mbijili amesema marehemu alifariki saa 9.00 alfajiri usiku wa kuamkia leo wakati akiendelea na matibabu katika hospitali ambayo bado haijafahamika.

“Tunajua kuwa marehemu alienda Arusha kwenye kikao cha Bodi kwa sababu yeye alikuwa ni Mwenyekiti wa bodi hiyo ila hatujajua alikufa katika hospitali gani,”amesema.

Amesema utaratibu wa kusafirisha mwili wake utafanyika Januari 27 (kesho kutwa ) kutoka Arusha kwenda Wilayani Mpwapwa na kwamba mazishi yatafanyika Jumatano (Januari 28) katika makuburi yaliopo katika viwanja vya Kanisa la Watakatifu Wote Vighawe.
Amesema kuwa Teu alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na sukari mara kwa mara.

Teu aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Mpwapwa (CCM) kati ya mwaka 2010 hadi 2015 na kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na baadaye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.

Pia Teu aliwahi kuwa Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Mpwapwa katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.

Aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo Oktoba 17 mwaka 2017 baada ya Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi Hassan Kibelloh.

Source : www.mwananchi.co.tz
 
Hospitali ambayo bado haijafahamika and the same story hapo tunapewa source ya kifo ????
 
Back
Top Bottom