Green na Brown cards za Bima ya Afya (NHIF) mnazielewa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Green na Brown cards za Bima ya Afya (NHIF) mnazielewa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mmaroroi, Aug 31, 2011.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Matumizi ya Green na Brown cards za NHIF zinabagua wanachama na zinasababisha matibabu hafifu kwa wala wanaotumia Brown card.Je hii ni sahihi hasa kwa maana kuweka baadhi ya Hospitali kubwa kutibu tu wale wa Green card?WanaJF na wanachama wa NHIF mnasemaje kuhusu hili?
   
 2. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,447
  Likes Received: 7,187
  Trophy Points: 280
  Poleni njooni AAR.Tulikuwa strategis hakuna matabaka japokuwa tumeamua kuhamia AAR
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ugumu ni namna ya kuachana na NHIF kwa kuwa mashirika ya umma na taasisi za serikali zinalazimika kuwasajili wafanyakazi wao NHIF.Wangeweka utaratibu wa kuweza kuondoka kwenda AAR ingekuwa safi kabisa maana NHIF wangebaki na wale wanaokubaliana na ubaguzi huo.
   
 4. S

  Sebali Member

  #4
  Aug 31, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />Hili suala linatengeneza matabaka miongoni mwa wagonjwa. Ni vizuri wanachama wote tungekuwa tunatumia cards za rangi moja.
   
 5. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Hii bima ya afya inatuhusu sie makabwela wauza matunda wa huku soko la Mbagala Yakhem? Au ni kwa wenye anuwani tu?
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  ingekua jambo zuri kama bima ya afya ingekuwa moja itasaidia sana kuondoa matabaka kwani kila mtz anapaswa kutibiwa vizuri.
   
 7. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wapendwa,

  binafsi nalifahamu vizuri na kwa kina suala hili. tatizo sio NHIF, bali ni hospitali kubwa za dar kama agakhan, regency, MNH (fast track) nk. hospitali hizi katika kuingia mkataba na NHIF zilihofu kuwa kwa kuwa huduma zao hutolewa katika mazingira bora zaidi, basi kuna hatari ya kila mwanachama wa NHIF kukimbilia kwao na kuongeza msongamano na hatimaye kuzorotesha huduma zao kama ilivyo kwenye hospitali za serikali. kwa msingi huo waliwapa NHIF sharti la kuchagua ni wanachama gani watakuwa wanaenda huko na kama hawatachagua na kuruhusu wote waende kwenye hospitali hizo basi, hawatasign mkataba ili kulinda quality ya huduma zao.

  NHIF walipotafakai kwa kina waliamua kutengeneza kadi za aina mbili, kijani na brown na wanachama wake hupewa kulingana na mishahara yao. kijani hutolewa kwa wenye mishahara kama Tsh. 820,000/= hivi (sikumbuki exact figure), kwenda juu kwa mujibu wa mishahara ya mwaka wa fedha 2007/08 na brown hutolewa kwa wenye mishahara ya chni ya hapo. kwa hiyo hospitali hizo kubwa hupokea wagonjwa wa green card tu kwa primary treatment pamoja na referals. wale wa brown cards, hupokelewa kama wana referals tu zilizowaelekea huko. mfano kuna wakati agakhan ndio pekee waliokuwa na kipimo cha MRI hapa nchini, so mgonjwa mwenye brown card alikuwa akipokelewa pale bila usumbufu wowote kama ana makaratasi yanayoonyesha kuwa daktari wake ameagiza afanye kipimo hicho.

  vilevile, tofauti hizo za green na brown huzingatiwa kwa hospitali za dar tu, ukitoka nje ya dar, hakuna masharti kama hayo niliyoyasema. mimi na familia yangu tuna green cards na tunapata huduma bila tatizo lolote hospitali yoyote tunayotaka wenyewe 24 hrs bila usumbufu wowote

  kwa hilo nawatetea NHIF, tatizo si lao, ni la hospitali husika

  natumanini mmeelewa sasa,

  mbarikiwe sana na Bwana

  eid mubarak
   
 8. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  Sasa kama tatizo sio NHIF na Serikali kwanini wasiruhusu mashirika ya umma na taasisi za serikali kujiunga mfano na AAR au taasisi nyingine yoyote ya matibabu wanayokubaliana nayo.Walifanye suala hili liwe huria kama ni kweli hawaendekezi ubaguzi.Utasema pia suala la matibabu ya Bima kutotolewa Weekends na sikukuu ni tatizo la hospitali wakati Hospitali hizohizo zinatibu wagonjwa wengine katika siku hizo.Geen na Brown card zitamchagulia mtu ugonjwa NHIF na Serikali iondoe ubaguzi huu.Mbona haukuwepo kabla ya kuanzishwa kwa NHIF, wakati waajiri ndio wanaogharamia matribabu hakukuwaa na ubaguzi lakini NHIF imeanzishwa kimatabaka.
   
 9. HOYANGA

  HOYANGA Senior Member

  #9
  Sep 1, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ikumbukwe pia kiwango cha kuchangia kinatofautiana sana kati ya wanachama wenye green card na brown card!!!
   
 10. HOYANGA

  HOYANGA Senior Member

  #10
  Sep 1, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  una mshahara mzuri sana kumbe!!!!
   
 11. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mpendwa,

  ondoa mawazo kuwa NHIF imeanzishwa kimatabaka, wao wanakata 3% tu kwenye mshahara wako, kama ni mdogo, sio wao waliokupa, huyo aliyekuajiri ndiye wa kumuuliza kwa nini anawapa watu mishahara kwa kutengeneza matabaka? nimeeleza hapo juu kuwa green na brown groups zilisababishwa na mahospitali ya kibiashara na sio NHIF. kwa kweli hapo mi sioni lawama ya NHIF inakujaje

  halafu naomba tuzungumzie uhalisia na sio nadharia. siujui mshahara wako, ila kiukweli kama ni wa kima cha chini, hutaweza mashirika binafsi kama AAR, strategis nk! kwa NHIF unachangia 3% na mwajiri anakuchangia 3%, niambie ni shirika gani zaidi ya NHIF amabalo serikali itakuchangia ada ya bima ya kila mwezi? fanya vizuri utafiti hapo na utakubaliana nami.

  kwa maoni yangu, NHIF inafaa sana kwa watu wenye mishahara ya kati na midogo, una uhuru wa kutibiwa hospitali yoyote na hata kupata daw katika maduka ya dawa yaliyo na mkataba na NHIF amabayo kwa dar ni mengi sana! nimeishasema kuwa na mimi natibiwa kwa kadi za NHIF na natibiwa 24/7 na sijawahi kuona usumbufu wowote, tena hata nikisahau kadi nyumbani huacha kitambulisho cha kazini mapokezi nanatibiwa naondoka bila kudaiwa hata senti na nikileta kadi narudishiwa kitambulisho changu, maisha yanaendelea! hayo ya kutotolewa huduma siku za weekend na sikukuu ndio kwanza nayasikia kwako. lakini hata kama ni taratibu za hopitali moja moja, kwa nini usiende hospitali nyingine yenye mkataba na NHIF? kwani wewe mwenzetu kadi yako imandikwa jina la hiyo hospitali yako inayokataa kukuhudumia siku za sikukuu na weekend?

  kuwa flexible mpendwa, u-enjoy huduma!

  NB: hao waajiri unaowasema kama ni mashirika ya umma, basi ndiyo serikali yenyewe!

  ubarikiwe sana!
   
 12. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ni kweli mpendwa,

  nina kazi nzuri sana, cheo kikubwa sana, mshahara mkubwa sana na maisha yangu ni mazuri sana! amani tele, furaha yangu ni ya kipimo cha kujazwa, kushindiliwa, kusukwasukwa hadi kumwagika! ooh, asante Yesu wangu!

  sifa na utukufu apewe Bwana wa Mabwana!

  NB: hata wewe mwenzetu unaweza kumshukuru Mungu kwa chochote alichokujaalia, hata kama ni afya! tuwe wenye kushukuru kwa kila jambo kwani hayo ni mapenzi ya Mungu katika Kristo Yesu (1 Thesalonike 5:16-18)

  amani iwe nawe, ubarikiwe sana mpendwa!
   
 13. D

  Danniair JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mh! kazi ipo.
   
 14. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2011
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  thanks a lot @ Miss Judith kwa maelezo ya kina na ya kujitosheleza.......Ukweli ni kwamba hili shirika lilipoanzishwa kulikua na changamoto nyingi na hali ya kukatisha tamaa, mfano mteja anaweza kuwa kajiandikisha na mshahara unakatwa halafu kadi hapewi na hivyo matibabu hapati, lakini with time walibadilika sana na mimi ni mmoja wanaoamini kuwa huduma zitolewazo na NHIF ni nzuri na za kuigwa mfano.........kudos sana NHIF, hakika ni mkombozi wa wengi!
   
 15. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ni kweli mpendwa,

  mwanzoni ilikuwa kazi kwelikweli, lakini si mnajua wapendwa kuwa mwanzo mgumu? kwa hali ilivyo sasa kwa wakazi wa dar, michango na fomu zilizojazwa kikamilifu zikifika na kupokelewa NHIF, hata wiki moja haiishi kadi huwa zimeishatoka! kuna watu ni wavivu kufuatilia, au maafisa wanaohusika huko maofisini kwao ni wavivu kufuatilia.

  nakumbuka niliwahi kumkuta mama mmoja analipa pesa kaunta ya agakhan eti kadi ya mwane haijatoka, nikamzuia na kumwambia awapigie NHIF simu kuwaambia kuwa anauguliwa na mchango na fomu yake imeishafika NHIF. akasema hana no ya simu ya NHIF, tukaiomba pale kwenye ofisi za aghakhan ikatafutwa ikapatikana ya meneja wao, unajua kilichotokea? NHIF walipothibitisha kuwa fomu imejazwa inavyotakiwa na mchango umeishawasilishwa kikamilifu, walipiga simu kwa wahusika aghakhan na yule mama alirudishiwa hela zake na kuambiwa aache kitambulisho cha kazini, akimaliza matibabu afuatilie kadi yake makao makuu kule kurasini awapelekee agakhana na atarudishiwa kitambulisho chake!

  wapendwa, ili huduma iwe nzuri mnataka iweje?
   
 16. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  Ndugu yangu matatizo haya hayakuwepo wakati waajira wanawalipia waajiriwa matibabu.Mbona sasa?Ugonjwa unachagua Mtu kwa kiwango cha mshahara?Wewe kama una mshahara mkubwa usijiangalie wewe binafsi wajali na hao wengine.Je wafe kwa kuwa wana mishahara midogo,ila wamepatwa na maginjwa makubwa?Tatizo letu watanzania tunajali ubinafsi tuangalie na wengine kuwa ni binadamu kama sisi.Sasa kama ni hivyo watu binafsi watakaojiunga na NHIF watatibiwa vizuri kweli bila kuondoa ubaguzi huu?
   
 17. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mpendwa,

  matatizo yako wapi? mnona mimi siyaoni? naona hujanielewa.

  1. kadi ya kijani na brown hazihusiani na magonjwa yanayotibiwa, bali zinahusiana na masharti yaliyotolewa na hospitali za kibiashara!

  2. ukiwa na kadi ya brown unatibiwa ugonjwa wowote utakaougua na kama itahitajika rufaa kwenye hospitali kubwa zaidi, hutaulizwa rangi ya kadi yako!

  3. wakati waajiri wanalipa, walikuwa wanaingia mkataba na hospitali chache na wengi walikuwa waningia mkataba na hospitali moja tu. sasa hapo kama unakaa ukonga na mwajiri ana mkataba na TMJ, basi ni lazima uje TMJ (msasani) hata kama unaumwa kikohozi tiu ambacho kingeweza kutibiwa hata hospitali ile ya wakatoliki pale ukonga madafu au ile ya akiba ya wafanyakazi pale RTD au hata ya wilaya temekke ambazo zote ziko karibu zaidi! lakini kwa kadi za NHIf uko flexible kutibiwa popote ili mradi hiyo hospitali ina mkataba na NHIF. hujaona faida hapo?

  4. pia kama mwajiri anataka wafanyakazi wake wote wawe na kadi za green, anaruhusiwa ku-top up michango yao ilingane na michango ya wenye mishahara mikubwa na michango hiyo ikifika NHIF, watapewa wote green cards! so unaweza kutoa wazo hilo kwa mwajiri wako na akiridhia basi mtabadilishiwa wote kadi zenu

  5. siangalii mshahara wangu bali naangalia unafuu, urahisi, na ubora wa huduma za NHIF pamoja na kufafanua kuhusu hizi kadi mbili za green na brown kwa kadiri ya ufahamu na uzoefu wangu na kwa mujibu wa swali lako wewe muanzisha thread. hayo ya mshahara unayaleta wewe sasa!

  natumaini umenielewa mpendwa,

  ubarikiwe sana
   
Loading...