Green guards waendeza vipigo kwa wanachama wa CHADEMA Arumeru Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Green guards waendeza vipigo kwa wanachama wa CHADEMA Arumeru Mashariki

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by KOMBAJR, Mar 19, 2012.

 1. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jana jioni wakati vijana wa CCM(Green Guards) wakitoka kwenye kampeni za mgombea wao katika kijiji cha kikatiti waliwavamia wananchi ambao inasemekana ni wanachama wa CDM katika eneo la Kwa Aloisi ambao inasemekana ni ngome kubwa ya CDM kwa eneo la tindigani na maji ya chai.Inasemekana vijana hao walikuwa wamejikusanyana wakifanya tasmini ya kampeni za mgombea wao zinavyoendelea ghafla ndipo Green Guard walipo tokea na kuanza kuwafanyia fujo. Huu si ungwana hata kidogo tusindane kwa sera jukwaani na siyo vujo katika makazi ya watu.
  Kwatasmini ambayo imefanyika ni kwamba hata wanakijiji wa vijiji vya milimani kama Sura,ulong`a,seela na maeneo mengine achini mbali vijiji au maeneo ambao yapo karibu na lami wameshashtuka hawataki kusikia kuhusu CCM na ukitaka kudhibitisha hilo angali mikutano yao pamoja na kuwa na watumbuizaji ya TOT Bado hawana mvuto wa watu na hata wanaokuja unaona kabisa kwamba hawana ushirikiano na mkutano.
  Sioi siyo mwanasiasa hana hata uwezo wa kujenga hoja, na kibaya zaidi hao makampeni meneja wake wote hawana sera kama kwenye mikutano ya jana badala ya kutoa sera wao wanazungumzia swala la urai wa mgombea wao.

  Agalizo wamekuwa na tabia ya kuwapa watu pesa ili wawapigie kura na pindi wanapogundua kuwa wananchi hawatawapa kura wanatishia kuwapasulia "chungu"watu wamestuka This time hakuna kitu kama hicho.

  CDM kuweni makini na shahada za kupigia kura nasikia kuna mchezo unaendelea.Ushindi upo kwa njia nyingi siyo tu
  kwa sanduku la kura.

  Mytake: Usichafue hali ya hewa kama una la maana,

  Source:Mashuuda wa matukio mbali mbali.
   
 2. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndiyo kazi yao Magamba wanapoona mambo yamekuwa magumu halafu wanakimbilia kulalamika wakati wao ndiyo wenye silaha zote na taasisi za ulinzi na usalama ziko chini yao, lakini kumbuka haki ya mtu haipotei bali hucheleweshwa tu
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,957
  Likes Received: 1,283
  Trophy Points: 280
  hawa ma*ga*mba wanaweza, kama lipipa lilimuua baba wa taifa sembuse kupiga tu. Kawaida yao
   
 4. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Hawa Chadema wawe makini sana ...tayari mkakati wa ccm wa IGunga unaendelea ...kwa kutumia genge la wahuni 200 waliosafirishwa toka Mara....vijana Hawa Wana silaha....bastola,mapanga,visu ,sime ,bisbisi ,acid etc...

  LENGo...

  1.kuchoma moto nyumba za wenyeji ambao ni wana ccm na kusingiZia ni Chadema.
  2.kuteka na kupora wana ccm ionekane ni Chadema
  3.kurushia mawe magari ya ccm wenzao na kusingiZia Chadema
  4.kuteka watu na kuwauwa...ie Hawa kule IGunga waliua zaidi ya watu 15..-ambao baada ya uchaguzi Maiti za watu walopotea ziliendelea kuonekana.
  5.kumwagia watu tindikali zionekane ni Chadema
  6.kufanya vurugu wakati matokeo ya awali yanaanZa kutoka ili ccm wapate Mwanya wakuite ffu .....warushe mabomu,ffu watakuja wakiwa na mabox tayari na wakati watu wanajifunika na moshi wa mabomu wao watabadili matokeo...

  NINI Kifanyike?

  Chadema wahubiri Amani mikutanoni..
  Wawasisitize vijana wao kuwa makini na watu wanaowachikoza au wanaovaaa Sare Zao sio wote ni Chadema ...wengine wapo kundi la "al shabaab"
  Wakazi wawe makini na wahamiaji ambao wapo kwenye kundi hii wanaosambazwa vijijini mwao........kwa kuwa wa wanafahamiana,itakuwa rahisi kutambua wageni miongoni mwao Wenye nia mbaya ...

  Onyo kwa Dola...

  Hatua ya ccm Kukodi mercenaries ni dalili mbaya .....Kama iliyokuwa ikifanywa na KAnu kuwakodi Mungiki....ni dalili za mwisho za chama kinachokufa...ie kutumia mamluki,kutumia siasa za majitaka...,kutumia dola ..etc..,....Hatua hizi hazitakuwa na faida kwa ccm zaidi zitaaharakisha kifo......kuna tofauti kubwa ua uelewa kati ya Arumeru na IGunga.......ccm wasitegemee propaganda ,vijarida...,mauwaji ,tindikali ...zitawasaidia kupata ushindi.....sanasana hata wakiwavika wafanya vurugu Sare za Chadema ....tayari wananchi wameshagundua .....na utafiti wa kiiteligensia unaonyesha wananchi wanawafuatilia kwa karibu sana ....Hawa mamluki...,wakazi wa Arumeru wana ushirikiano wa kipekee nje ya chama ......msishangae mkaamka asubuhi mkakuta Hao mamluki 200 wote wamechinjwa na mapanga na wameru ......kwani hii Siri imeshaliki hata kwa wananchi wa kawaida....na Hao wamekuwa common enemy wa kuwachonganisha wameru ....nao hawataki kuuliwa Kama Wana IGunga .

  Watu wa usalama wa Taifa ingilieni haraka kusaidia Hawa mamluki warudi makwao haraka......WAmeru watawachinja........na IKULU ITABEBA LAWAMA......KWANI HII TAARIFA KWA SASA INAFUATILIWA HADI NA VUOMBO VYA NJE NCHI....HAO MAMLUKI KILA WAMESHAWEKEWA SURVEILLANCE YA KITAALAMU KABISA NA KILA MWENENDO WAO ...UNADAKWA NA KUREKODIWA .....NA MUDA SI MREFU WATAZINGIRWA..NA MAAFA YATAKUWA MAKUBWA SANA....NA HII INAWEZA KUSABABISHA WAKUU WA USALAMA ,POLISI NA HATA RAIS WETU APELEKWE THE HAGUE ..SIKU AKITOKA MADARAKANI...

  CHUKUENI TAHADHARI......! Anaepata ujumbe huu ..Amuambie na mwenzake....!!! Amani ya nchi yetu ,na umoja wetu Kama taifa ni muhimu kuliko tamaa ya ccm kushinda Arumeru!!!!! Wekeni tu uwanja sawa na haki .mshindi wa jimbo la Arumeru ...hatakuwa RAIS WA JAMHURI,!
   
 5. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,277
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Hao Greenguards jana walikimbilia mashamba ya Maua na kituo cha polisi
   
 6. R

  Real Masai Senior Member

  #6
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM wameprove failure tayari..Wameru c wana Igunga.Mwana ngoja tuendelee kusambaza Ujumbe
   
 7. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi huu utaratabu wa chama kuwa wanaendesha vikundi vya kigaidi kama Green Guard unatoka wapi? kwanini serikali wanaruhusu kitu hiki? kuna hatari ya hali hii kutufikisha kule ambapo Somalia wapo sasa!!.
   
 8. k

  kastarehe JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kweli walioletwa ni "jamaica mockers" wa pale mjini musoma maeneo ya Kariakoo na soko la saanane basi ni vijihuni na wezi walioshindwa std vii na form four failures wa shule za kata. Wanatembea na mapanga na visu pale musoma!! kazi zao kuu ni uporaji wa barabarani, uvutaji wa bangi na uvunjaji nyumba!
  Hao watumiaji wa bastola ni TISS waliojichanganya kunusuru mabwana zao wa ufisadi. CC majambazi.
  Nilishakomenti hapa tena kuwa hizi ni dalili za utawala uliofitinika! Hat wakifanyaje meli imekumbwa na dhoruba inazama. Kweli laana imewafika:
  -Ni lini ilifikirika eti chama dola/tawala kingeweka bendera za upinzani kwenye magari yao ili kuvuta hadhira ya mkutano?
  Ni lini ilifikirika eti wanachama wa chama dola/ tawala kinachomiliki kodi za wananchi wangevaa sare za chama pinzani ili kufanya fujo ili kuepuka zomea zomea!! yetu macho!! Jamani enyi mnaong'ang'ania hiyo maiti CCM hamhisi harufu?!
   
 9. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ingekuwa ni cdm waliofanya hivyo-hii habari ingepewa kipoindi maalum huko tbc
   
Loading...