Green Bay Packers, alama kubwa ya jimbo la Wisconsin nchini Marekani

GREAT INVESTOR

Senior Member
Nov 13, 2018
128
295
Ukifika Jimbo la Wisconsin Nchini Marekani, kila corner utakoyopita basi lazima utakutana na na logo yenye herufi "G"iliyozungukwa na rangi ya kijani.

Herufi "G" inasimama badala ya neno Green Bay ambao ni mji maarufu sana hapa Wisconsin. Katika huo mji, kuna timu inayoshiriki Michuano ya American football inaitwa Green Bay packers.

Hii team ni habari nyingine, ina mafanikio katika huo mchezo, si mafanikio makubwa sana ila ina mafanikio..kwa ufupi hii team ni habari nyingine, ukifika kwenye huu mji habari kubwa utakazozipata ukiwa mgeni basi ni za hii team.

Hii team inachukua umaarufu mkubwa si kwa sababu ya maendeleo, ila ni kwa sababu ya watu kupenda KITU CHAO na kukisemea mazuri na kuringia walichonacho.

Kwa hapa Marekani, Mpira wa miguu si maarufu sana na wao wanauita Soccer, wakati hiyo American football inachezwa kwa mikono wao ndo wanaiita FOOTBALL. Jamaa wanapenda utofauti sana.

Jana nimepata bahati ya kuhudhuria moja ya game yao, katika uwanja wao wa nyumbani ujulikanao kama LAMBEAU STADIUM, huu uwanja ni kivutio kikubwa sana katika mji Green Bay. Mbali ya uwepo wa COVID-19 jana watu zaidi ya 72000 waliruhusiwa kushuhudia hii game... uwe umechanjwa au hujachanjwa, uwe na Barakoa au hauna.

Nimejifunza kitu kimoja, PENDA SANA KITU ULICHONACHO, HICHO NDO CHA KWAKO, KITUKUZE ACHA KUTUKUZA VITU VYA WATU WENGINE.

MVIMG_20210814_204333.jpg
IMG_20210814_192624.jpg
IMG_20210814_190632.jpg
IMG_20210814_190348.jpg
 
Hongera sana Mkuu kwa kuongeza jiografia mpya kichwani. Wamarekani sijui mpira wa Miguu uliwakosea nini. Vipi hii inshu ya betting nako vijana wanaichangamkia au hakuna?
 
View attachment 1893469View attachment 1893471View attachment 1893476View attachment 1893479
siku wabongo wa mikoani tukianza kuzipenda timu zetu, tuachane na hawa doto na kulwa wa kariakoo, mpira wetu utapanda sana!
 
Hongera sana Mkuu kwa kuongeza jiografia mpya kichwani. Wamarekani sijui mpira wa Miguu uliwakosea nini. Vipi hii inshu ya betting nako vijana wanaichangamkia au hakuna?
mpira wa miguu mwanzilishi ni mwingereza, na wao (US) wako kinyume na kila kitu cha mkoloni wao (UK).......

mfano,,,, tea vs coffee, right hand drive vs left hand, soccer vs football, PM/monarchy vs democracy, hata english yenyewe haifanani kihivyo, yan hawataki kila kitu cha mwingereza
 
Back
Top Bottom