Great Thinnkers - what do we need to be included in the New Constitution?

Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,269
4,569
1. All professional firms to be owned 100% by Tanzanians- legal practice, Accounting and Audting, Consulting Engineer, Architechture etc.

2. All professional firms to be locally registered. Global firms to be allowed to operate in the Country using local names.

3. Multi Nations company to be allowed to operate in the Country by registering a company with Tanzanians. Foreign subsidiary not be allowed to operate in Tanzania.

4. Special seats for member of Parliament to abolished, instead special seat for ward leaders to be increased.

5.

6.
 
Mkuu hizo sheria zote zipo Tanzania, lakini hakuna anayefatilia hizo sheria,
 
Mkuu hizo sheria zote zipo Tanzania, lakini hakuna anayefatilia hizo sheria,

Hazipo. Mfano Accounting and Auditing firm inaruhusu 50% -50%; wanachofanya mgeni ni kumtafuta mtanzania anaandika kampuni baadaye anafrustrate yule mtanzania anabaki yeye mwenyewe. India hawaruhusu Big Four kufanya shughuli kwa majina yao na hii imesaidia kuleta usawa kwa audit firms zote kwani mbele ya sheria za India zote ni sawa na wanatumia standards zinazofanana
 
7. Wabunge wasiwe mawaziri
8. Vyeo vya wakuu wa mikoa na wilaya vifutwe
9. Tume huru ya uchaguzi isiyoteuliwa na Rais prefably bunge
10. Matokeo ya urais yahojiwe mahakama rufaa/mahakama ya katiba
11. Direct election ya mameya (wasichaguliwe na madiwani)
12. Viongozi wa Taasisi nyeti waidhinishwe na bunge after a gruling debate (IGP, M'kiti wa NEC, Director of TAKUKURU, Baraza la mawaziri, Majaji wa mahakama ya rufaa, Wakurugenzi wote wa mashirika nyeti ya umma etc)
13. Muundo wa muungano ubadilishwe prefably serikali tatu
14. Kundoa kinga ya Rais kwa makosa aliyoyafanya as individual na sio kama Rais eg Mkapa kujiuzia kinyemela mgodi wa makaa ya mawe ya kiwira kwa bei poa
15. Kuruhusu independent candidate na Pia mbuge asipoteze ubunge wake wakati anapohama chama kwasababu hajachaguliwa na chama bali wanannchi ndio wawe na uwezo wa kumu-impeach kama hawakuridhika
16. Kufuta sheria 40 kandamizi zilizoorodheshwa kwenye tume ya Jaji Nyalali
17. And Very controversial to allow dual citizenship
18. Tusiwe na cheo cha Waziri mkuu, tufuate presedential system, tuwe na Rais na VP full stop.
19. Muundo wa baraza la mawaziri uuelezwe waziwazi katika katiba sio kila rais anayekuja anakuja na wizara zake. (Wenzetu wamarekani wizara zao ni hizo hizo tangu wakati wa George Washington)
20................. Nitaorodhesha nyingine baadaye
 
Ahsante natumaini wanasiasa hayo yapo vichwani mwao. Mimi na wewe tungeangalia zaidi zile fursa ambazo zisipozibwa wageni wanaweza kumiliki uchumi wetu kila nyanja. Mfano kutoa viza kwa wageni kuendesha migahawa au kutembeza bidhaa mitaani n.k
 
  • Kuwe na mihimili mitatu ya uongozi katika nchi,serikali,Bunge na Mahakama na mhimili mmoja usiinuke juu ya mwingine.
  • Bunge liwekwe moja kwa moja na wananchi kupita uchaguzi mkuu ambapo watu wenye sifa ndio wachaguliwe kuongoza wananchi.
  • Rais awe kiongozi wa umma na awajibike pale anapotumia madaraka vibaya.
  • Jaji mkuu ateuliwe na rais lakini asiwe valid hati uteuzi wake upate ridhaa ya wabunge. Pia asiachishwe kazi hadi kwa ridhaa ya Bunge.
  • Rais aunde serikai kwa kuteua watu anaoona wanafaa kuwa mawaziri
  • Mbunge mwenye jimbo la uchaguzi asiruhusiwe kuwa waziri ili kuliwakilisha vyema jimbo lake bungeni na kuepuka kuigonganisha mihimili miwili,yaani serikali kwa maana ya waziri na Bunge kwa maana ya Mbunge kwa mwakilishi mmoja.
  • Kusiwe na wabunge wakuteuliwa maana km dhana ya ubunge ni uwakilishi wabunge wakuteuliwa wanamwakilisha nani!
  • Mkuu wa Majeshi na vyombo vyote vya usalama ateuliwe na raisi ila uteuzi huo upate ridhaa ya Wabunge
  • Tume ya Taifa ya uchaguzi isiteuliwe na Rais/isiwe chini ya ofisi ya Rais...ichaguliwe na Bunge!
  • Rais ashitakiwe kwa makosa atakayofanya ktk kipindi chake cha Urais.
  • Mshindi wa pili ktk kinyanganyiro cha Urais awe mbunge moja kwa moja na awe kiongozi wa Upinzani Bungeni.
  • Spika wa Bunge asiwe na jimbo la uchaguzi na asiwe na chama chochote cha siasa!
  • Viongozi wa Mikoa/Wilaya na vijiji wachaguliwe na wananchi kupitia uchaguzi mkuu na baadae kuunda serikali zao zitakazosimamiwa na serikali kuu badala ya kuteuliwa na Rais km sasa!
 
Unafikiri Bunge lenye wingi wa wabunge wa chama tawala wanaweza kumkataa mteule wa Mwenyekiti wao? Kwa nini Katiba isisema Rais apeleke majina matatu ili bunge lipige kura na kupata Jaji Mkuu?
 
"Unafikiri Bunge lenye wingi wa wabunge wa chama tawala wanaweza kumkataa mteule wa Mwenyekiti wao? Kwa nini Katiba isisema Rais apeleke majina matatu ili bunge lipige kura na kupata Jaji Mkuu?"

Hili linawezekana kwa kua nina imani wapo watu wengi sana ndani ya nchi hii ambao ni makini,watakaoheshimu katiba(ambayo haipo bado) watakaoheshimu utawala wa sheria....wadilifu kiukweli na wasiohongeka ...wapo...wapo wengi

Kama ulifuatilia Waziri Mkuu alipokuwa anathibitishwa; kuna mama alisimama akatoa hoja kuwa Mh Pinda apite bila kujadiliwa, wabunge wa chama chake wakipiga makofu, kilichofuata na kupiga kura. Jee katika wabunge wate hakuna aliyekuwa na mchango hasi kama mteule angejadiliwa?
 
"Kama ulifuatilia Waziri Mkuu alipokuwa anathibitishwa; kuna mama alisimama akatoa hoja kuwa Mh Pinda apite bila kujadiliwa, wabunge wa chama chake wakipiga makofu, kilichofuata na kupiga kura. Jee katika wabunge wate hakuna aliyekuwa na mchango hasi kama mteule angejadiliwa?"

Nafikiri mimi nimewaza hivyo,nimeongozwa na imani zaidi na nikafikiri kutakua na kanuni ya kuwaadabisha wenye hisia binafsi,km yule mama mathalan...na kwa kua JF ni kisima cha fikra wewe unazungumzaje kuhusu Raisi kuteua watendaji wake wakuu?
 
Tuchukulie tuu wakuu wa mashirika ya umma, utaratibu ni kuwa bodi za makampuni husika zinatakiwa kufanya mchakato wote na kupeleke jina kwa Raisi kwa ajili ya uteuzi. Tofauti na utaratibu huo kuna shirika nadhani ni Tanesco Raisi alimteua mtu ambaye hata hakuwa kwenye orodha ya watu waliosailiwa. Kuna consulting companies zenye uweze wa kusaili na kupata watendaji kwa mujibu ya vigezo vinavyotakiwa, Raisi asiwe anateu watu
 
kumbukeni kuna maombi mengine yanakuja na cost.....tusije tukajifanya too democratic tukaishia kuwa maskini, au kuomba misaada zaidi kutoka nje ili tufanye uchaguzi tu.....tusipolipa sisi madeni watalipa watoto na wajukuu zetu.
 
Nilwahi pia kushauri juu ya muundo wa Bunge kwamba, kwa mtazamo wangu, uwe hivi: Kusiwe na nafasi ya (kugombea) UBUNGE badala yake kuwe na nafasi za URAIS na UDIWANI tu kama ifuatavyo:-

(i) MADIWANI wawe (automatically) ndio "(WA)MBUNGE" wa jimbo ambalo Kata zao zipo kwa utaratibu huu ufuatao.

(ii) Mara baada ya uchaguzi mkuu, madiwani wa jimbo husika majina yao yapangwe ki-afabeti.

(iii) Diwani wa kwanza (au wa mwisho kadiri itakavyoonekana inafaa), atawakilisha jimbo Bungeni kwa mwaka wa kwanza.

(iv) Mwaka wa pili, jimbo litawakilishwa na diwani anayefuata, hivyo hivyo hadi diwani wa mwisho.

TATIZO: Ikitokea jimbo husika lina kata tano, excellent; kila kata itakuwa na nafasi sawa ya uwakilishi jimboni kwani uchaguzi mkuu wa Tz ni kila baada ya miaka mitano. Tatizo linakuja pale ambapo kata katika jimbo ni pungufu au zaidi ya tano. Suluhisho ya hili ni kama ifuatavyo:-

(i) Zikiwa pungufu ya tano, ile kata iliyoanza uwakilishi, inaweza kurudia tena uwakilishi ndani ya kipindi kile cha uhai wa Bunge.

(ii) Kata zikiwa zaidi ya tano, zile kata ambazo hazikupata nafasi za kuliwakilisha jimbo ziwe za kwanza kuwakilisha jimbo msimu mwingine wa Bunge.

Kwa hiyo utaona kinachozumgumzwa hapa sio uwakilishi wa mtu bali ni KATA ndio inayowakilisha kwa niaba ya wananchi wa jimbo husika.

FAIDA ZA MFUMO HUU:-

(i) Yale mazoea ya mtu mmoja tena kutoka eneo moja tu la jimbo kuwakilisha wananchi kwa hata miaka 30 utakuwa umekwisha. Badala yake utaona ushirikishaji wa wananchi wengi zaidi na kimsingi ndio hasa dhima ya Bunge kama chombo cha wananchi badala ya kuwa na watu wale wale kana kwamba ni wafame wa majimbo "yao".

(ii) KUWA KARIBU ZAIDI NA WANANCHI: Asilimia kubwa ya wabunge wetu wa leo wanaishi Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, na miji mikubwa. Kiukweli hawajui zile adha za kweli zinazowakumba wananchi wao. Bila unafiki, MADIWANI wetu wako karibu zaidi na wananchi tena wanaishi katika maeneo yao hivyo wanaweza kuwa wawakilishi bora zaidi kuliko hawa ma-profesa na wafanyabiashara wakubwa wenye malengo yao kinyume na dhana nzima ya uwakilishi.

(iii) MGAWANYO MZURI WA MAPATO/KEKI YA TAIFA: Kile ambacho kingeweza kwenda kwa mbunge mmoja tu kwa miaka mitano (tena kwa sinzia tu bungeni), kinaweza kugawanywa kwa watu/MADIWANI watano.

(iv) GHARAMA ZA CHAGUZI NDOGO: Garama ya sasa ya kurudia uchaguzi mdogo wa ubunge nadhani ni mzigo usio wa lazima. Tukifuata mfumo huu, gharama hizi zitakuwa zimekufa kifo cha kawaida.

(v) GHARAMA ZA UENDESHAJI BUNGE - MAGARI: Haya masuala ya kwamba eti serikali inaingia gharama kubwa kwa mfano kukopesha wabunge magari itakuwa imekufa - gari linakuwa la jimbo na litakuwa linatumiwa na diwani atakayekuwa anawakilisha jimbo kwa mwaka ule baada ya hapo linahamia kwa diwani anayefuata na anadhibitiwa na madiwani wenzake. Haya mambo ya kutumia rasilimali za serikali kama kubebea magari ya umma majani ya kulishia wanyama wa mbunge yatakwisha.

(v) GHARAMA ZA UENDESHAJI BUNGE - ASANTE BAADA YA MIAKA MITANO: Haya mabo ya kugawana mamilioi ya pesa kila baada ya miaka mitano kwa wabunge wastaafu (hata kama watagombea tena uchaguzi unaofuata) ambao ni mzigo mzito kwa walipa kodi utakwisha.

(vi) ... nk.

HASARA ZA MFUMO HUU: Sioni hasa kubwa za mfumo huu.

VIKWAZO VYA MFUMO HUU:

(i) FIKRA POTOFU: Utamsikia mkubwa fulani akitoa hoja kwa mfano "... Bunge letu linafuata mfumo wa Wesminster na ndio tulioamua kuuridhia ..." kana kwamba ulishushwa kutoka Mbinguni! Hivi, jamani nauliza, hatuwezi kuwa na kitu chetu wenyewe hata wengine wakaiga kutoka kwetu? Au sisi ndio wa kuiga tu. Hebu na sisi tuwaoneshe wenzetu maana halisi ya demokrasia (ushirikishaji wananchi) nini kwa kuwa na mfumo wetu wenyewe. Kama wazee wetu akina Mtemi Kimweri, Isike, Mkwawa, na wengineo wengi waliweza zama hizo sisi wa dunia ya leo tunaojidai tumeenda shule tuanashindwa hata na wazee hao? Aibu! KAMA KUSOMA NI KUNAKILI KILA KITU, HERI KUTOKUSOMA.
 
(1) kufuta nafasi ya wakuu wa wilaya na mikoa, kazi hizo zifanywe na wakurugenzi
(2)kupunguza idadi ya wanajeshi warudishwe kua askari wa polisi(hawana kazi tofauti na kunywa bia na sukari ya bure na kutongoza wake za watu)
(3)wenye nyumba za kupangisha walipe kadili wanavyolipwa(pay as you earn)
 
Nafasi zifuatazo ziondolewe;
1. Mkuu wa mkoa: na timu yake
2. Mkuu wa wilaya: na timu yake
3. Katibu Tarafa
4. Wabunge viti maalum
5. madiwani viti maalum
6. Wizara zote chini ya Ofisi ya Rais
7. Wabunge kutoka Znz katika Bunge la URT
8. Ofisi ya maadili ya viongozi wa umma (TAKUKURU inatosha)

Pia Katiba Mpya izingatie Haya
1. Itaje wizara za kudumu za serikali ya Tz
2. Ripoti ya CAG iwasilishwe bungeni serikali
3. Udhibiti wa kuhamisha mafungu ya bajeti (Re-allocation) bila idhini ya Bunge
4. Safari za Rais nje ziwekewe mipaka, pia za Mawaziri
5. Kura ya kutokuwa na imani na Rais iwekwe bayana
6. Mamlaka ya rais kuvunja Bunge yaelezewe bayana na sababu ziidhinishwe
7. Mbunge asiondolewe nafasi yake kwa kuhama chama
8. Idadi ya mabunge/madiwani (viti) itokane na asilimia ya kura katika uchaguzi mkuu
9. Ushindi wa Rais utokane na asilimia 50% ya kura
10. Iwapo asilimia 50% haikufikiwa uchaguzi urudiwe kwa wawili waliopata kura za juu
11. Mirahaba ya madini 50%
12. uraia wa nchi mbili (Dual citizenship)
13. Haki za binadamu zidaiwe mahakamani
14. Watanzania walio nje wapige kura
15. Makampuni ya nnje yatumie sheria za Tz za mikataba
16. Spika/Meya/ Mwenyekiti halmashauri achaguliwe na wananchi
17. Adhabu za watumishi wa umma wanaohujumu mali
18. Rais awajibike kwa makosa yake binafsi akiondoka madarakani
19. Noti za nchi ziwe na sura ya Nyerere na Karume tu
20. Nyumba na mali za nchi zisiuzwe kiholela
21. Rais ateue wakurugenzi ila wathibitishwe na bunge
20.
19.

Jamani ni mengi kwa uchache ni hayo tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom