Great Awakening Africa: Madhehebu makongwe chukuaeni tahadhari

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
2,536
2,000
Great Awakening ni movement kubwa sana ya Dini ilio tokea Marekani, kuanzia Karne ya 18 hadi mwanzoni mwa karne ya 20 hii ilipelekea kuanzishwa kwa madhehbu chungu nzima kule Marekani.

Kabla ya hii movement Dini kubwa Marekani wakati huo ilikiwa ni Anglican ilio letwa na mkoloni Mwingereza.

Great Awakening ilikuwa na phase kama 4 hivi na hii vuguvugu ilipelekea kupungua nguvu sana kwa Anglican kama dhebu kubwa kabisa Marekani.

Na Angalican/Church of England ilikuwa ni kama dini ya kikoloni wakati huo ikipelekwa Marekani na Waingereza na Anglican pia ilianza baada King Henry VIII kuachana na Roma.

Kanisa la Methodist church America likiwa ndo la kwanza kabisa kuanzishwa kutokana na hii Movement. Methodist church hata Uingereza ilikuwepo ambapo watu walijimega kutoka Church of England.

Baadae yakafuata mengi sana kama wakina SDA chini ya Elen G White na wenzake mwaka 1863, Church of God chini ya Elder Richard Spurling mwaka 1886, na nyingine nyingi sana.

Greate Awakening Africa.

Hii ya sasa haina tofauti sana na ya America, na hii ya sasa inaongozwa na Manabii, watoa miujiza, kivutio kikubwa ni miujiza.

Greate awakening ya marekani ilitaka watu waache dhambi na wamwamini Mungu na mwamko wa kumjua Mungu ulikuwa mkubwa sana kipindi hiki na hapo ndo wakajitokeza watu kama William Miller alie waambia wafuasi wake kwamba Mwisho wa Dunia ni October 22 1844 hii ikapelekea matatizo makubwa sana na inabatizwa jina la Great Disapointment.

Hii ya sasa watu wana Mjua Mungu sana ila sasa wanavutwa na miujiza, watu wanataka kuona miujiza tu mtu kapona kanda na kadhalika, mtu anaacha dhehebu lake la awali anakimbilia miujiza.

Hii Movemnet ina impact kubwa sana kwenye Makanisa makongwe kama Roman, Angalican, SDA, Lutheran, na mengineyo.

Hawa manabiii si kwamba wanaenda Vijijini ku recruit waumini wapya kama walivyo fanya hao wakongwe.

Hawa Manabii wako City centre make ndo kuna pesa, vijijini huwakuti kabisa make hakuna pesa huko.

Manabii hawa wako mijini tena City Centre wanacho fanya ni kuchukua waumini kutoka kwenye Madhehebu Makongwe kwa kigezo cha miujiza.

Waumini wa hawa Manabii ni walikuwa waumini wa either Roman, SDA, Lutheran, Angalican Islamic, na mengineyo.

Hii vuguvugu haitawaacha salama haya madhebu kama hawatakuja na mikakati ya Kidini ya kupambana na hawa Manabii feki.

Historia inajirudia sana ukiangalia Uprotestant ulivyo anzisishwa na Wakina Maritin Luther karine ya 16 na kuibomoa vilivyo Romab Cathoric na the sam inafanyika sasa.
 
Marytina

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,283
2,000
Tatizo hamna dhehebu lenye ukamilifu hata kwa 50%

Sasa hiyo imetoa mwanya kwa yeyote anayeielewa Bible kuhoji the conducts ya dhehebu lake mwishowe kuja na jibu ya kuwa inabidi hili na hili lisiwepo.

Ukienda RC na Lutheran huku tunabatiza WATOTO.

Tena baba wa ubatizo anakiri Iman kwa niaba ya kuchanga

Ukija TAG kuna Mambo ya kushangaza kwamba binti wa TAG hairuhusiwi kuolewa na mlutheri au mkatoliki au yeyote nje ya TAG

Ukija kwa mwamposa anakuuzia maji, kinyume na biblia

So Mambo magumu kwa kweli na michango makanisani Kama TAG na PEFA unaweza kujihisi mungu hatakimaskini kanisani
 
Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
1,720

Ukiangalia kwa haraka haraka utaona kabisa Changamoto kubwa ni kutokuwa na Imani thabiti. Miujiza hiyo inaweza pia kutokea ukiwa katika dhehebu lolote as long as linamwinua Kristo na Baba Yake (Mungu Baba).

Habari zingine zinakuja tu kama wewe muumini hutakuw msoma neno lazima uyumbe sana. Soma neno la Mungu na mengi utafunuliwa. Michango makanisani kwa kweli ni kero kubwa basi tu. Sio huko tu PEFA na TAG, Nenda SDA nao siku hizi michango ni mingi asikwambie Mtu.

Uongozi wa Juu unapanga tu na kuyashusha huku bila kujali hali za kiuchumi za waumini wake. Ila mimi binafsi, kama sina nafasi sana huwa sishawishiwi na maneno maneno au kuogopeshwa na Mahubiri kutishana eti usipotoa Fedha itakuwa hivi na hivi..! Mungu anajua watu wanapitia mambo gani ila watu wake wanafanya kukadiria tu yaani.
 
Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
6,237

Tafuta kumjua Mungu na mtafute Mungu kwani anapatikana.

Usiende kanisani ili watu wakuone mtakatifu.

Usiende kanisani kwa ajili ya kutafuta mafanikio au miujiza.

Jifunze neno la Mungu bila mipaka ya kwamba mimi ni dhehebu fulani basi simsikilizi fulani kwa sababu siwa dhehebu langu. Kikubwa pia tutenge Muda wa kusoma Neno la Mungu.
 
Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
1,720
2,000
JUKWAA LA DINI LIRUDISHENI JAMANI, Tunaomba sana sana. Jukwaa la dini lilikuwa jukwaa langu pendwa sana Baada ya Jukwaa la Jamii intelligence. Jukwaa la dini limenisaidia kupata majibu kwa maswali yangu kadhaa nikiyokuwa nayo. Uongozi wa JamiiForums, tunatambua mnayo mambo mengi sana ya kufanyia kazi lakini hili jukwaa la dini tunaomba mlirudishe.
 
Umesema vyema.

Watumishi makanisani wanalazimisha tu utoaji kwani ndio riziki yao.

Na wengi wao hawajui hata kufundisha kuhusu utoaji.

Kumtolea Mungu sadaka kuna njia nyingi si fedha tu, na kumtolea Mungu sadaka yataka mahusiano mazuri kwanza wewe na yeye
Akwambie utatoa kiasi gani, sehemu gani na wakati gani na baada ya hapo ataachilia kitu kwako kipya.

Mimi ni Mlutheri kanisa letu halina sheria sana, na kimapokea naona wapo vizuri tu.

Lakini kwenye swala la sadaka aiseee ni wizi tu umejaa na Watumishi i mean wachungaji wengi ni wale wa kujituma wao na wala si kutumwa na Mungu, kazi zinawashinda kabisa.
 
Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
3,149
2,000
Wanaohama ni wachache sana kuliko wanaoingia.

Na mnaosema michango ndio inawakimbiza waumini , je huko ndio wanaweza kulipa lakimoja ya kuombewa? Bado hujanunua mafuta, hujanunua MAJI n.k

Unaweza ukaona michango uliyokuwa unatoa RC ni michache kuliko huko kwenye Ministry.

Tubuni na kuiamini Injili na sio suala la kutegemea miujiza.
 
Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
6,237
2,000
JUKWAA LA DINI LIRUDISHENI JAMANI, Tunaomba sana sana. Jukwaa la dini lilikuwa jukwaa langu pendwa sana Baada ya Jukwaa la Jamii intelligence. Jukwaa la dini limenisaidia kupata majibu kwa maswali yangu kadhaa nikiyokuwa nayo. Uongozi wa JamiiForums, tunatambua mnayo mambo mengi sana ya kufanyia kazi lakini hili jukwaa la dini tunaomba mlirudishe.
Jukwaa la dini mbona lipo, sema labda kama wewe tu ndo huna Access ya kuchangia huko.
 
Kamukhm

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,652
2,000
Hii ni topic inayofikirisha sana.

Umewahi kujiuliza ikiwa Mungu ni mmoja, kwanini madhehebu mengi, hasa kwenye sisi wafuasi wa Kristo?
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
54,571
2,000
Mleta mada naomba unijibu hili swali ujapopata wasaa...

Hivi hayo madhehebu uliyoyataja kama 'madhehebu kongwe', yalianzishwa na nani?

Yaliteremshwa toka mbinguni au yana mwanzilishi ambaye ni mwanadamu?
 
MasterGamaliel

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
551
500
Tafuta kumjua Mungu na mtafute Mungu kwani anapatikana.

Usiende kanisani ili watu wakuone mtakatifu.

Usiende kanisani kwa ajili ya kutafuta mafanikio au miujiza.

Jifunze neno la Mungu bila mipaka ya kwamba mimi ni dhehebu fulani basi simsikilizi fulani kwa sababu siwa dhehebu langu. Kikubwa pia tutenge Muda wa kusoma Neno la Mungu.
Umenena vema, tunapenda kujumuika na wenzetu kanisani, Tatizo michango imezizidi sadaka,
Ningependelea makanisa yawe na Sadaka 3 tu yaani:-
1.Sadaka kuu (ya kuendeshea kanisa kila siku,),
2.Sadaka ya maendeleo ya kanisa, (ujenzi na usambao)
3. Sadaka ya kuwawezesha wastahilio kuinuliwa, (wenye dhiki na walio chini wasaidiwe wainuke).
Watu wasali waende!

Yesu alifanya hayo tu!
 
Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
6,237
2,000
Umenena vema, tunapenda kujumuika na wenzetu kanisani, Tatizo michango imezizidi sadaka,
Ningependelea makanisa yawe na Sadaka 3 tu yaani:-
1.Sadaka kuu (ya kuendeshea kanisa kila siku,),
2.Sadaka ya maendeleo ya kanisa, (ujenzi na usambao)
3. Sadaka ya kuwawezesha wastahilio kuinuliwa, (wenye dhiki na walio chini wasaidiwe wainuke).
Watu wasali waende!

Yesu alifanya hayo tu!
Kuna mikutano ya injili, sadaka ni moja tu.

Hakuna cha mala jengo, shukrani, utumishi, ahadi, mala sijui jenga nini..

Tusikubali kushikwa fikra na madhehubu yetu.

Nawashukuru sana Lutheran kwa kunitunza kiroho ningali mdogo kabisa.
Wamekua njia kunileta kwa kristo.
Lakini hawatoweza kunizui kwenda mahali kwingine kumtumiki na kumwabudu Mungu wangu.
 
Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
1,720
2,000
Hivi unaweza ukawa na akili timamu ukawa kanisa la masanja makanizaji?? Hahahahhhaaa

IMG_1350.jpg
 
Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
1,720
2,000
IMG_1349.jpg

Masanja ni mjinga sana yani.! Katuwekea picha za wanawake wenye makalio makubwa .! Yaani
 
Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
1,720
2,000
Umenena vema, tunapenda kujumuika na wenzetu kanisani, Tatizo michango imezizidi sadaka,
Ningependelea makanisa yawe na Sadaka 3 tu yaani:-
1.Sadaka kuu (ya kuendeshea kanisa kila siku,),
2.Sadaka ya maendeleo ya kanisa, (ujenzi na usambao)
3. Sadaka ya kuwawezesha wastahilio kuinuliwa, (wenye dhiki na walio chini wasaidiwe wainuke).
Watu wasali waende!

Yesu alifanya hayo tu!

Kuna kipindi nilitaka kuweka “UZI NIULIZIE KAMA KUNA MTU ALIWAHI PATA MUUJIZA KUPITIA KUTOA SADAKA NA ZAKA KWA WINGI KANISANI ATOE USHUHUDA WAKE”

Mimi hadi leo sijawahi toa zaka kwakweli. Maana kama sadaka natoaga sasa hiyo Zaka inakujaje kujaje japo niagizo la Mungu ila kutoa 10% ya mshahara siojambo rahisi
 
MasterGamaliel

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
551
500
Kuna kipindi nilitaka kuweka “UZI NIULIZIE KAMA KUNA MTU ALIWAHI PATA MUUJIZA KUPITIA KUTOA SADAKA NA ZAKA KWA WINGI KANISANI ATOE USHUHUDA WAKE”

Mimi hadi leo sijawahi toa zaka kwakweli. Maana kama sadaka natoaga sasa hiyo Zaka inakujaje kujaje japo niagizo la Mungu ila kutoa 10% ya mshahara siojambo rahisi
Kuna uzi humu unajadili michango mingi ya kanisa RC
 
Kibukuasili

JF-Expert Member
May 15, 2010
916
250
Mojawapo ya tatizo kubwa ni uvivu wa kusoma na kulielewa neno la Mungu. Soma Biblia na vitabu vingine vya dini na historia ya dini yako upate ufahamu mzuri wa kile unachoamini. Hapo hakuna mtu yeyote, si mchungaji, padri wala nani, atakuyumbishayumbisha. Bila hivyo makanisa ya "miujiza" yataendelea kupata waumini.
Kuhusu tishio kwa makanisa "kongwe" sio kweli. Wanaoingia kwenye miujiza na wanaotoka ni kama sawasawa tu. Wapo wanaoingia lakini wakikosa miujiza waliotarajia wanarudi kwenye makanisa yao ya awali.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom