Grayson Nyakarungu majibu yangu kwa hoja za 'Mbwazoba' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Grayson Nyakarungu majibu yangu kwa hoja za 'Mbwazoba'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyakarungu, May 15, 2011.

 1. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Dear Mbwazoba,

  Kwanza kabisa nakupa hongera kwa kazi yako unayoifanya humu JF bila kuchoka, bila kujali unaifanya kwa manufaa yako binafsi au ya chama.

  Thread zako karibia zote, zinaonyesha una kitu nyuma yako kinachokusukuma kufanya hivyo, kitu hicho yawezekana kikawa ni ukweli unaopenda kuusema au hofu inayokusababisha uamue kuweka viziba njia ili wanaotishia uwepo wako katika nafasi anuai washindwe.

  Ila ndugu yangu Mbwa, umekosa kitu kimoja tu katika taarifa zako,kitu hicho ni utulivu na chanzo cha taarifa zako, ndio maana hata jina langu umekosea kuandika, na post zako nyingi sana huwa hauko tayari kuweka wazi vyanzo vyake.

  Wewe waweza kuwa ni mmoja wa wagombea au la! ila hali ya post zako inaonyesha una mgombea unayemtaka ashinde japo hauko tayari kuweka wazi msimamo wako.

  Naomba nikupe majibu ya hoja ulizotirirka nazo hapa JF juzi:-

  i) Kuhusu kusoma chuo cha diplomasia ambacho hukusema ni cha wapi,
  Ni kweli mimi nilisoma pale Kurasini 2005, nilisoma mambo ya uhusiano wa kimataifa, japo haina mwingiliano wowote na usalama wa taifa, kama ulivyosema.

  ii) Ukaribu wangu na Marando na mzee Mrema,
  Kwanza kabisa natamani kujua, kama wewe ni mtanzania au la! watanzania tunaishi kama ndugu, na hatuna ubaguzi wa asilia wala wa kiukanda, sasa unaposhangaa ukaribu wangu na mzee mrema, inadhihirisha kabisa wewe ni mgeni kwenye tamaduni ya Tanzania, je umejaribu kufuatilia ukaribu wangu na mzee huyu, je umefanikiwa kujua kama kuna/hakuna ukoo unaotuunganisha, hata kwa kuoana? Na hata hivyo mimi sina ukaribu wowote na mzee mrema, ndugu yangu zoba, kuwa makini sana na vyanzo vyako visivyokuwa na ukweli.
  Mzee marando ni mwanasheria/ni mwanachama wa chadema/anatokea mara ninakotokea, hivyo nina kila sababu ya kuwa karibu nae, kwanza ili nivune hekima na maarifa alizonazo, pia ndugu mbwa, huyu marando anatokea mara, je umefuatilia na kujua kama sina ukoo nae? mbona unajishushia uwezo wa kuonekana great thinker?

  iii) Kuwa na uwezo wa kujua mambo mengi,
  Kaka/dada mbwa, kila mwenye juhudi za kutafuta maarifa, atayapata na kila mwenye kusubiri ataletewa hayo maarifa, katika kipimo kisichomtosha, mimi ninajuhudi za kujifunza mambo yote yenye manufaa kwa jamii, kwa hiyo sioni kama kuna tatizo la mimi kujua muziki (kuandika, kuimba, kupiga vyombo n.k).

  Pia nakuahidi, siku nikija DSM (kwa sasa niko kazini Mwanza), nitakuchukua twende nyumbani kwangu, ili ukaone, na ujue ni kwanini ninayajua hayo yote yanayokupatia wasiwasi, utafanikiwa kuona maktaba ndogo, yenye vitabu vya mambo mbalimbali, hivi vyote ninavisoma na vinanisaidia kuyajua hayo unayoyahoji.


  iv) Kusafiri kwangu,
  Kama ulivyosema kuwa mimi ni daktari, na ni mfanyakazi wa halmashauri ya jiji la mwanza, hivyo katika taaluma yetu, kuna vitengo maalum, vinavyompa mtumishi nfursa mbalimbali.

  Kwangu mimi, ninahusika na kitengo cha magonjwa ya milipuko kwa jamii, hivyo utashangaa kunisikia tabora, shinyanga, kigoma bukoba, singida, mara na mwanza au geita.

  Hii haizuiliki, na ikiwa utaonekana ni mtu unayejituma na kujitoa sana, kuwa huruma, kutokuwa na kinyaa, kutokuwanyanyapaa wagonjwa, basi hapo utakuwa unatumwa kila siku kama mimi.

  Pia uligusia mikoa ya kusini, bwana mbwa, napenda nikuombe uwe makini sana katika kufuatilia maisha ya mtu, kabla hujaanza kutoa comments kumhusu.

  Mimi nimeishi mtwara miaka 4, nilikuwa mratibu wa vijana wa kanda ya kusini (mtwr,lindi na ruvuma)katika makundi ya vijana wanaojitolea katika jamii, southern volunters clubs(svc), hivyo mpaka sasa, mimi ni senior member ninayetegemewa kwa ushauri huko, pia nina jarida langu linaitwa sauti ya chinga linatoka kila mwezi huko mtwara.

  YOTE HAYO HAPO JUU, HAYANA UHUSIANO NA KITENGO CHA USALAMA WA TAIFA.

  NA HIYO JKT NAOMBA UNIKUMBUSHE ILIKUWA WAPI NA ILINI?

  Siandiki haya kwa kujitetea, ila nataka uwe macho sana na tuhuma, na aina yoyote ya hoja zako unazoleta hapa jamvini,hoja za ukabila na udini ni aibu kwa chadema haziwezi kupewa nafasi kamwe.
  MWISHO, MIMI NI MGOMBEA NAFASI YA UWENYEKITI BARAZA LA VIJANA CHADEMA (BAVICHA)
  SINA SHAKA NIKICHAGULIWA NITAFANYA MAKUBWA ZAIDI YA HAYO NILIYOYAFANYA NDANI NA NJE YA CHAMA.

  NAMI NITAWEKA CV NA TAMKO LANGU HADHARANI,WEEK HII.


  MAONI YA MTU YAHESHIMIWE, ILA YAANGALIWE!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hongera sana na kila la heri...nimefarijika na majibu haya
   
 3. M

  Mbwazoba Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unipeleke kwako, wewe unanifahamu mimi.
  umejuaje niko dar....
  mausalama wa ukweli huwa hamusemi n'go.
  haya dogo piga kazi nimekuchemsha na umewaka kweli, nahisi unatamani ukinikamata utaninyonya macho, nyie wakurya sio kabisa.
   
 4. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Ndugu mbwazoba,
  kuna jambo ambalo ni muhimu sana kwa wewe kulijua, unatakiwa ujifunze maana halisi ya mtu kuitwa usalama wa Taifa, pia ueleze usalama wa taifa aliyeshika ethics, anamadhara gani kwa chadema.
  pia uwaeleze chadema ni kwa nini wamwogope usalama wa taifa.
  Chadema haiwezi/ na haina sababu ya kuwaogopa watu wa usalama wa taifa.
  Note: yote haya utayafafanua vizuri, ikiwa umejifunza na kujua, ni nini maana ya usalama wa taifa.

  nyumbani kwangu, nitakupeleka kwa mwaliko tu ndugu yangu,ili ujifunze kitu chenye manufaa kwako.
   
 5. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ya nini Kujibishana na Mtu anajejiita Mbwa Mtoto wa Zoba?
   
 6. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  acha kudanganya watu dogo,kama wewe ni mfanyakazi jiji huko unakosafiri tabora,singida,iringa nako unafanya kazi za halmashauri ya jiji? tuambie chuo umesoma wapi usitudanganye kwamba umesoma udakitari wakati wewe umesoma nursing. jiji umeajiliwa lini we nae ni muongo tu. puuuuuh
   
 7. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Chonde Chonde Baba usiendelee kujibizana na Mbwa,mwishowe nawe utabweka kama yeye.!
   
 8. M

  Mbwazoba Member

  #8
  May 15, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani mimi sio mbwa, mimi ni mbwazoba na sio mbwa zoba
   
 9. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  nenda Nyakarungu umeeleza vizuri, nakutakia kila la kheri kwenye kugombea
   
 10. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  duh,bora umejibu coz tetesi alwayz huzua donda!!
   
 11. M

  Mbwazoba Member

  #11
  May 15, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haya bwana umemaliza, kamataneni wenyewe mm simo tena.
   
 12. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #12
  May 15, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Eeeh bandugu,pumzika kwanza,si ushajibiwa!!njoo kivingine na kama una data na unayoyasema gray kakuruhu mwaga data...nahisi kama kama umetumwa na una maslahi binafsi...wewe ni mbwa, na la pili zoba kwa hiyo ni sahihi mbwa mtoto wa zoba!! sasa unasahisha nini na unakataa nini...au hiyo space huitaki...??mweee!!
  Ukiendelea kuja kihovyo-hovyo tutakuweka kwenye ignore list!!
   
 13. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #13
  May 15, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Ndg IGWA,
  Naomba nikusaidie kuhusu hili

  MIKOA YA TABORA, SINGIDA, KIGOMA, SHINYANGA,MARA, MWANZA NA GEITA iko kwenye orodha inayoitwa kitaaluma Regins WithSame Endemic D'ses (RWSED), yaani mikoa yenye magonjwa endelevu yanayofanana, hivyo watumishi wa afya wa kanda husika ya kiafya hufanya ziara za kitabibu na na mafunzo kwa jamii husika, hivyo usiogope utakuwa unanisikia mara kwa mara mikoa hiyo, ila sio mikoa ya iringa unakosema na sijui tulionana lini huko, hata hivyo wewe nakujua hisia zako ni sawa na za bwana zoba za kudai kuwa mm eti ni usalama wa taifa, poleni kwa kushituliwa na huyo jamaa, naomba tusubiri mdahalo wa wagombea na ndipo tutafahamiana vizuri, pia niliambiwa na katibu mkuu wa chama kuwa wapo wagombea wenzangu wamenishitaki kuwa mm nazunguka kufanya kampeni za bavicha, masikini wa mungu kumbe niko kikazi jamani.


  MAONI YA MTU YAHESHIMIWE, ILA YAANGALIWE
   
 14. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #14
  May 15, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  pole sana ndugu yangu nyakarungu Mungu huwa hamfichi mnafiki kumbe ID ya mbwazoba ni yako unaanzisha ishu ili upime akili za watu hata kama utaondoa hiyo post yako uliyojibu tuhuma kwamba wewe ni nurse kupitia id ya mbwazoba tumeisha kusoma, alafu tangia siku ile uanzishe mashambulizi kwa Heche wenye akili tulijua moja kwa moja kwamba ni wewe leo umeumbuka, lakini pia jibu haya kwa kutumia id yoyote kati ya hizo zako mbili, we kama ni daktari umesoma chuo gani? na wewe ni mfawidhi kwenye hospital ipi? acha uongo.
   
 15. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #15
  May 15, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  duh!!!!!!! kweli mungu hamfichi mnafiki ndugu yangu,
  yaani mbinu zako hizo ni za kitaifa gani sijui, umejaribu kila mbinu halali umekwama na umeamua kuanza uzushi ndani ya JF?
  NIKUSAIDE TU, KAMA UNATAKA KUJUA NIMESOMA CHUO GANI, SUBIRI NITATOA CV YANGU WEEK HII,TEMBELEA OFSI ZA HALMASHAURI YA JIJI, KAULIZIE KILA KITU ABOUT ME NDUGU,MAANA NAONA UNAHASIRA NA MIMI SANA, HADI UMEANZA UZUSHI WAKO ILI IWEJE SASA?
  NINGEWEZA KUKULIZA JE UMETUMWA NA NANI, LAKINI IUMEWEKA WAZI MWENYEWE.

  POLE NDGU YANGU KWA KUJARIBU USIYOYAWEZA.
   
 16. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Amesema atakupeleka kwake kwa maana umehoji kwa nini anajua vitu vingi. Umeuliza amejuaje uko Dar na wewe mwenyewe unamtuhumu kuwa mtu wa usalama. Wewe ndiye usiye na hoja, maana hata kama Grayson ni mwanausalama, wapi katika katiba ya chadema anapozuiliwa kugombea? Mwache dogo afanye siasa, wewe endeleza majungu yako.
   
 17. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #17
  May 15, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kama anasema uongo, pana kamati ya usaili; ndiyo itakayomhukumu na sio ninyi wapinzani wake mnaojaribu kumchafua tu. Nilidhani hizi siasa za maji taka zimezoeleka zaidi katika chama changu cha magamba, kumbe na huko kwenu zipo!
   
 18. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #18
  May 15, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Je na ID ya igwa pia ni ya grayson? acha kutuzingua wewe!
   
 19. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #19
  May 15, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Aiseh!Mmbwa Zoba kumbe hii ID yako pia tumekusoma..Nyaka mpotezee huyu Jamaa watu Waoga kama hawa aidha kama ye binafsi ndo Mgombea,Ndugu,Jamaa au Marafiki zake huwa wanakufa Mara nyingi sana kabla yakufa Rasmi huyu nae ndo vifo vyake hivi.
   
 20. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #20
  May 15, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  nyie hamfai kabisa kwa kuanzisha hizi taarabu/mipasho hapa
  mimi nilijua kuna issue kumbe mnajuana hacheni KUCHAFUA CHAMA na magungu yenu
   
Loading...