Grayson na Demokrasia

Nyakarungu

JF-Expert Member
May 1, 2011
472
375
'Ni watu, kwa ajili ya watu Na watu'.

Hii ni tafasri iliyotolewa na mwanaharakati wa kimarekani aliyeitwa Linkon,
Kwa lugha ya kiingereza ilisomeka hivi 'is the people for the people by the people'

Hapa mwanaharakati huyu alimaanisha kuwa, demokrasia ni njia inayotumiwa na watu, kwa ajili ya manufaa yao, na wakiwa huru kuitumia.


Binafsi naamini sana katika nguvu demokrasia, japo kuna wakati demokrasia huonekana kutoa ushindi hata pasipo sahihi,(the truth can't be determined by majority vote) ila kwa sababu, nguvu yake inaheshimika na kusimamiwa, haipo njia mbadala zaidi ya mapinduzi.

Ndugu zangu, nafurahi kuandika mistari hii hapa, nikiwa na shauku kubwa, ya kuwaomba mtoe ushauri nasaha kwa wagombea wa nafasi kadhaa, kwenye baraza la vijana chadema (bavicha).

Hivi sasa, tupo katika mchakato wa kujindaa na uchaguzi huo, utakaofanyika 28 may 2011, michakato hii imeshika kasi sana, hasa baada ya vijana wengi nikiwemo mimi, kujitokeza kugombea nafasi anuai.

Lakini, kwa kuwa uchaguzi huu utafanyika kwa njia ya kidemokrasia, na kwa kuwa wingi wa kura ndio unampa ushindi mtu katika nafasi aliyogombea, na kwa kuwa kila mgombea, ana mbinu yake ya kuwashawishi wajumbe wamwone kuwa anafaa kuchaguliwa, na kwa kuwa wagombea tuna hulka na haiba tofauti, na kwa kuwa tunaheshimu demokrasia kama jina la chama chetu linavyoisadifu.
Basi
Imetokea tabia, ya baadhi ya wagombea kupiga simu kwa wajumbe mikoani, badala ya kueleza sababu ya wao kugombea na kwa nini wao wanafaa, inasikitisha sana kwa mgombea kutoa maneno ya uongo na uzushi eti kuwa wagombea halisi ni wawili tu, na wengine wamepandikizwa ili wapunguze kura zake, hapa nagundua kuwa, tafasri ya demokrasia haijaingia vizuri mioyoni mwao, na je, ni wapi imeandikwa kuwa yeye ndiye mgombea anayefaa? je kama ingekuwa hivyo, basi angeteuliwa tu, na sio kuwasumbua wajumbe toka mikoani, kwenda dar es salaam kupiga kura.
Na wala uongozi wa kitaifa usingeweka huru form za wagombea.

Je, kwa nini aina hii ya uongo na uzushi ivumiliwe? nani ana haki miliki ya kura za mikoa fulani? mgombea wa aina hii, anataka watu tuamini kuwa yeye anauhakika wa kushinda? je, anataka kutuambia nini uvumilivu wake endapo atakosa nafasi anayogombea?
Hivyo uhuru wa demokrasia, uheshimiwe na kulindwa.
Ni hayo tu ndugu zangu, ila "mtaka heshima kwa nguvu, huishia kukata tamaa"


MAONI YA MTU YAHESHIMIWE, LAKINI YAANGALIWE.
 
Tunashukuru kwa andiko lako lakini nilitegemea lalamiko lako ungelipeleka kwa uongoz wa juu ili watoe angalizo kuliko hapa JF Lakini naamini wajumbe watakao piga kura si vilaza au mbumbumbu kiasi washindwa kupambanua anayefaa, ondoa hofu kama unafaa watakuchagua kama kura zisipotosha umungemkono mwenyako
 
Back
Top Bottom