Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,181
Heshima yenu wakuu,
Kila nikisikia na kusoma sakata zima la BOT na jinamizi zima la ufisadi jinsi linavyotishia uhai wa Taifa letu Tukufu Tanzania na wananchi wake,huwa ninapata uchungu mkali kwani kwa dhamana na Ridhaa ya watanzania waliokua wanahimizwa kwa kampeni chungu nzima za kuhamasisha uandikishaji na upigaji kura na hatimaye kuwapa baadhi dhamana halali za kuongoza achilia mbali wale wliotumia njia haramu kuhalalisha ridhaa bado kwa miaka mingi sasa tumejitahidi kuvumilia aidha kutokana na asili za malezi yetu au kwa kuzidiwa na vitisho,dharau , kejeli na matusi yaliyopindukia kutoka kwa viongozi walewale waliotokana na Dhamana yetu huku wakimis-use the term "Gorvernment servant".Eti wao ni watumishi wa serikali .
Pia,naona itakua ni jambo la busara na la ujasiri na la kuonyesha mfano wa kukataa na kupambana na mfumo au kasumba ya kutoreact dhidi ya mawaziri wanaotusababishia umaskini.Leo hii ukiangalia Japan serikali yao ina nidhamu kwani kuna kasumba ya kuwajibisha au ya mhusika kuwajibika mwenyewe pale linapotokea suala linalomuhusu mtumishi wa serikali ktk kuhusika na ubadhirifu.Ukiangalia nchi zilizopiga hatua Afrika hgakuna utovu mkubwa wa nidhamu kama uliopo hapa Tanzania.
Hivyo basi kama tunayo nia ya kujenga taifa lenye uchumi mkubwa linaloheshimika duniani na linalojitahidi kuinua hali ya maisha ya wananchi wake basi sisi kama kikundi flani chenye maslahi tunaweza kuanzia hatu hiyo huku tukimulika wale ambao wanabomoa huku tulikoanza kujenga,basi kwenye hili sakata la BOT kama tunataka kumkaripa na kumwajibisha Bi.Zakia Meghji,basi hatuna Budi kumuwajibisha Basil Pesambili Mramba na Katibu wa wizara Mhe.Mgonja kwani hawa kwa nafasi zao wangeweza kuwa kiini cha kuokoa maisha ya Watanzania kadhaa waliofarikia au kuwa maskini ambao walisababishwa na upotevu wa fedha hizo.
Kwa mfano huyu mhe.Mramba amekua mtu wa matusi na ambaye ameliingizia taifa hasara kubwa huku akitoa majibu ya kejeli na Matusi kwa watanzania waliompa dhamana ya kuwa hapo alipo
Rejea kauli zake za kutetea Ununuzi wa ndege ya Rais,Rada nk
Rejea utetezi wake wa safari za Rais
Rejea hotuba za mkutano wake wa kisiasa huko Jimboni kwake Rombo baada ya Bunge kupitisha bajeti tata na iliyokua na udhaifu mkubwa akiwa waziri wa Miundombinu hapo mwaka juzi.
Kwa jamii iliyostaarabika na yenye kuangalia huko mbele tuendako na kujal hali ya vizazi vyetu vya baadae na KUFUTA KABISA huu utovu wa nidhamu wa viongozi wetu basi baada ya huyu mheshimiwa kuruka vizingiti vyote basi ni muda muafaka kwetu kuanzisha kampeni au mchango wowote wa kumwajibisha waziri huyu.
Mtanzania yoyote mwenye uchungu na nchi yako jitolee kwa jasho na Damu kuliokoa Taifa letu.Kumbuka Amerika ilijengwa kwa Moyo wa wananchi na viongozi wenye uchungu na nchi yao na wenye uzalendo wa kweli.Sasa tuanzie hapa tulipo kwa Tanzania inawezekana tu.
Mungu ibariki Tanzania
Naomba kutoa hoja