Gray Mgonja kuwa Governer?

Zanaki

JF-Expert Member
Sep 1, 2006
545
75
Kuna habari kuwa Gray Mgonja anakwenda kuwa Gavana wa BOT na Dr Dau anakwenda kuwa DG wa TRA....Mgonja kwa sasa ni Permanent Secretary Treasury na Dr Dau,(huyu ni mchezaji mpira wa zamani wa Yanga) yeye yuko NSSF. Bado nafuatilia hili suala kwa ukaribu sana,na habari zaidi ziko njiani
 
Tumeisha maana kama Mgonja ataenda kuwa Gavana sasa kuna nini tena ?maskandali ya hazina na mesheni zote Mgonja yumo kuna mahala alitajwa kuhusika hata na stika na visa za kuingia ni mradi wake na mzungu wa Holland . Majumba kibao huko Marekani nasikia mwenye ukweli wa majumba haya afafanue leo unampa bank jamani haya na kasi zote hizi .
 
Zanaki,

Huyu Dr Dau, ndo nani vile unaweza kunisaidia jina lake lote na ni mwaka gani alichezea Yanga.
 
Huyo Mgonja ni yupi huyo? Wenye vitu vyake mwageni hapa, mimi jamani huyo kanipita pembeni, lakini ninamjua msaidizi wake shujaa mama Joyce Mapunjo, ambaye nimemshuhudia kwa macho yangu akimrekebisha rais wetu akiwa waziri,

Kuwa waziri hapa umekosea sio sawa ulivyosema au unavyofikiri, mzee mzima akampa bonge la jicho, na mama naye akasimama na kumpa macho, na kwenye makatibu akamchagua, Mama Mapunjo you are my hero! na ninakuombea upewe ukatibu kamili na baadaye uwaziri,

ila wazee huyu Mgonja simfahamu vizuri ingwa nimemuona sana, wenye data mwageni uwanja uko huru huu!
 
jina kamili ni Ramadhani Kitwana Dau (PhD .) msomi huyu na sijawahi kumsikia akicheza mpira. Dr.Dau alikuwa akitajwatajwa na vyombo vya habari kuwa atapewa nafasi kubwa katika serikali ya JK. zaidi ya kuwa mkurugenzi mkuu wa nssf sifahamu habari zake zozote.

Gray Mgonja alikuwa mkurugenzi bot kabla ya kuazimwa na hazina kama naibu katibu mkuu. baadaye mkapa akampandisha cheo kuwa katibu mkuu na majuzi JK amemteua tena katika wadhifa huo.

Mchango wa gray mgonja katika kuwezesha tanzania kuingia HIPC ni mkubwa na unaheshimika. vilevile anaifahamu BOT kutokana na utumishi wake huko, na vilevile kama mjumbe wa bodi ya bot kutokana na wadhifa wake wa katibu mkuu hazina.

kuna wanaodai wanafahamu MADHAMBI mengi ya gray mgonja, lakini hizi tetesi za ugavana zinatokana na rekodi yake ya kazi pale hazina.
 
Dau na mpira...Dau na mpira! Huikumbuki hio? Yes,Dau was a footballer with Young Africans i think,and maybe thats the main reason why he is so friendly with Magori(TFF vice Chairman) who is also a director at NSSF
 
jokaKuu,
Mbona hukuendelea na hayo madai? Nasikia amekuwa na miradi na Mramba. Pia kuna jumba keshanunua California.
 
Jasusi,

Yaani baada ya jamaa kupata Scandal ya Quality group, "kakata" kidogodogo kwa jamaa wanampa "ulaji" mwingine ili tusahahu?

Tanzania ina wenyewe!

Nimechoka kabisa
 
Dau toka NSSF kumeoza na rushwa na migogoro ya interest.Leo akiletwa hazina JK atakuwa anafanya nini ? Gray kuijua hazina na wizi wa mali zetu ni kigezo awe gavana ?
 
Jasusi,
ninachofahamu mimi ni role ya Gray Mgonja katika jitihada za Tanzania kurekebisha mahusiano yake na vyombo vya fedha vya kimataifa, na kufaulu kuingia katika mpango wa HIPC. amefanya kazi kubwa pale hazina na ndiyo maana amepandishwa cheo toka naibu kuwa katibu mkuu kamili.

aidha, siyo haitakuwa ajabu kama atateuliwa gavana. Gilman Rutihinda alikuwa na role na wadhifa kama huu wa Mgonja, na baadaye akateuliwa kuwa gavana benki kuu.

kuhusu TUHUMA, kama amelimbikiza mali isivyo halali basi nashauri kwa dhati kabisa aondolewe hata katika wadhifa alionao sasa.

Mwisho, naomba uposti majina ya watanzania ambao ni safi, na wana elimu na uzoefu wa kuweza kuwa gavana wa bot, na kamishna wa tra.
 
jokaKuu,
Nilitaka kuendeleza tu mada. Sina majina wala wasifu wa Watanzania walio safi na wenye uzoefu wa kuwa gavana wa bot. Ningekuwa nayo ningekwenda kugombea ubunge.
 
Kuna habari kuwa Gray Mgonja anakwenda kuwa Gavana wa BOT na Dr Dau anakwenda kuwa DG wa TRA....Mgonja kwa sasa ni Permanent Secretary Treasury na Dr Dau,(huyu ni mchezaji mpira wa zamani wa Yanga) yeye yuko NSSF. Bado nafuatilia hili suala kwa ukaribu sana,na habari zaidi ziko njiani
Hatari nan ampe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom