GRAPHIC IMAGES: Hili Ndio Sakata la BIBI HARUSI ALIYETEKWA, AKABAKWA NA HATIMAYE KUNYONGWA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

GRAPHIC IMAGES: Hili Ndio Sakata la BIBI HARUSI ALIYETEKWA, AKABAKWA NA HATIMAYE KUNYONGWA

Discussion in 'Jamii Photos' started by MaxShimba, Oct 31, 2012.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [h=3][/h]

  [​IMG]
  Mwili wa marehemu Elizabeth Terezia (32) ulivvyokutwa.
  ---------------------------------------------------
  BI. Harusi mtarajiwa, Elizabeth Terezia (32), mkazi wa Mbezi Beach, Kinondoni jijini Dar es Salaam amebakwa, ameuawa kikatili na watu wasiojulikana wakati akitoka katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Kawe, Dar linaloongozwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima,

  <center style="background-color: transparent; border: 0px none; margin: 0px; outline: none 0px; padding: 0px; vertical-align: baseline; "><ins style="background-color: transparent; border: medium none; display: inline-table; height: 70px; margin: 0px; outline: none 0px; padding: 0px; vertical-align: baseline; width: 468px; "></ins></center>
  Kwa mujibu wa bwana harusi mtarajiwa, Edefonce Sikwembe (42) ambaye ni mkazi wa Kunduchi, Dar tukio hilo la kinyama lilijiri Oktoba 10, mwaka huu majira ya usiku wakati Elizabeth akirudi nyumbani kutokea kanisani hapo.

  “Siku ya tukio tulikuwa katika viwanja vya kanisa la Gwajima, nilimpigia simu mwenzangu kumwambia nakwenda nyumbani kuandaa biashara ambayo ningeifanye kesho yake,” alisema Sikwembe.

  [​IMG]

  Jeneza lenye mwili wa marehemu Elizabeth Terezia likiwa mbele ya waombolezaji.
  ---------------------------
  “Kwa maana hiyo yeye nilimwacha kanisani. Saa 2:30 usiku nikampigia tena simu kutaka kujua alipo, akaniambia yupo njiani anaelekea nyumbani kwao.

  “Saa 3:00 usiku nilimpigia tena, maana ilikuwa kawaida yangu akiwa nje ya nyumbani kumfuatilia anaporudi ili nijue alipo, lakini cha kushangaza akawa hapatikani, niliamini simu yake iliishiwa chaji.
  [​IMG]

  Marehemu Eliza enzi za uhai wake.
  ------------------------------------
  “Sikuwa na wasiwasi hata kidogo. Hata usingizi wangu usiku haukuwa wa mang’amunga’amu. Alfajiri ya siku iliyofuata nilipoamka nilimpigia simu tena nikiamini mchumba wangu Eliza alichaji simu usiku, lakini bado akawa hapatikani!

  “Hata hivyo, niliondoka nyumbani alfajiri hiyohiyo kwenda Buguruni ambako ndiko kuna biashara zangu. Njiani nilimfikiria sana Eliza, si kawaida yake kutopatikana hewani kwa muda wote huo.

  “Ilipofika saa 12 asubuhi, shemeji yangu anaitwa Lillian alinipigia simu na kuniambia Eliza tangu alipokwenda kanisani jana yake jioni hajaonekana nyumbani.


  [​IMG]

  Bwana harusi mtarajiwa wa marehemu Eliza, Edefonce Sikwembe (42) akiwa na simanzi.
  ------------------------------------------
  “Kuanzia hapo nilianza kupatwa na wasiwasi, tena mkubwa. Namjua Eliza, si mtu wa kwenda kulala mahali bila taarifa, hasa kwangu,”alisema bwana harusi huyo huku machozi yakimtiririka. Kabla hajaendelea, akasema kwa uchungu na kwa kifupi!

  “Da! Inauma sana kwa kweli.”
  Akaendelea: “Palepale nilifunga biashara, nikaondoka kwenda kwao ili nikapate maelezo mazuri. Lakini kabla sijafika Mbezi Beach, njiani maeneo ya Afrikana nilikutana na Lillian.


  “Tukaamua kwenda kanisani kwa Gwajima kwa ajili ya kuulizia. Njiani akili yangu iliwaza mengi, lakini yale mabaya sikuyapa nafasi na nilimwomba Mungu kwamba kama kuna baya lolote limemfika mpenzi wangu iwe ni filamu na si la kweli.

  “Tulifika, mawazo yangu yalitamani tuambiwe Eliza alilala pale kwa ajili ya huduma, lakini ikawa kinyume, tukajibiwa kuwa alipoondoka jana, hakurudi!

  [​IMG]

  Mwili wa marehemu Eliza ukiwa umetelekezwa pembeni yake kukiwa na biblia yake.
  --------------------------------------------------
  “Kuanzia hapo nilichanganyikiwa, nilikuwa nikitembea eneo la kanisa huku na kule nikiamini nitamwona Eliza wangu, lakini bila mafanikio.

  “Nikaenda kuuliza kwa majirani wa maeneo yale lakini majibu yao yalikuwa hawajamuona mtu na aina hiyo. Kuna wakati nilitaka kuamini kwamba, alifichwa eneo lilelile na wafichaji waliniona ninavyohaha kumsaka mchumba wangu.

  “Mwishowe, mimi na Lillian tulikwenda Kituo cha Polisi Kawe na baadaye Oysterbay kwa ajili ya kuulizia na kuripoti, nako hakukuwa na taarifa za mchumba wangu.


  “Baada ya hapo tuliendelea kuulizia na vituo vingine vya polisi na tulifika Hospitali ya Temeke, Amana na Mwananyamala ambako pia hatukumpata Eliza. Mpaka hapo bado sikuacha kupiga simu yake na iliendelea kutopatikana.” (akatokwa machozi).

  Akaendelea: “Siku ya nne tangu kutoweka kwa Eliza, shemeji Lillian alinipigia simu, akaniambia niende nyumbani kwao, nikahisi Eliza ameonekana. Njiani mapigo ya moyo yalikuwa yakienda kwa kasi.

  “Nilipokaribia kwao, niliwaona watu wengi wakiwa katika mfereji ambao upo karibu na hapo nyumbani, nikashtuka na kusimama kwanza, kisha nikatembea tena.

  [​IMG]

  Mama mzazi wa marehemu Eliza akiweka udongo kwenye kaburi la mwanae.
  ----------------------------------------------------
  “Lakini tayari mwili wangu ukawa unaishiwa nguvu kwani nyuso za watu wale zilikuwa za huzuni tupu. Kusema ukweli japo ni mwanaume, nilishindwa kujizuia, nikakaa chini hasa pia baada ya kuliona ‘Difenda’ la polisi likiwa katika eneo lile.” (Sikwembe akalia tena).

  Alipotulia, akaendelea: “Shemeji yangu alinifuata huku akilia na kusema, ‘shemeji hatumaye Elizabeth hatunaye tena duniani.’


  Sikwembe alishindwa kusimulia vizuri kutokana na kilio, lakini alisema ilionekana marehemu alitekwa na watu wasiojulikana, wakambaka na kumuua kwa kumnyonga kwa khanga kisha kutuupa mwili wake katika mfereji huo.

  [​IMG]

  Mwili wa marehemu Eliza.
  ----------------------------------------
  Alisema mwili wa marehemu ulikutwa ukielea kwenye maji machafu na umevimba huku nguo yake za ndani ikiwa pembeni yake sanjari na Biblia aliyokuwa nayo kanisani.

  “Elizabeth amekufa kifo cha kusikitisha sana, kinaniuma sana, maiti yake ilibidi ichukuliwe kwenye nailoni mpaka Hospitali ya Mwananyamala, lakini uongozi wa hospitali hiyo walisema chumba cha maiti kilijaa hivyo tukampeleka Muhimbili,” alisema mwanaume huyo.


  Marehemu alizikwa Oktoba 14, mwaka huu, Mbezi, Dar es Salaam na ilikuwa wafunge ndoa na Edefonce Desemba, mwaka huu na tayari vikao vya harusi vilishaanza kwa pande zote mbili. Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.


  Kwa Idhini ya Jicho Letu Blog
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Hii nchi ilipofika ni pabaya saana
   
 3. RR

  RR JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Asee....
  Ni visa au ni tamaa tu.....kubaka....kuua.......nothing worse than this to a woman!
   
 4. Kimagege

  Kimagege JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 284
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mungu ampokee kwake.
   
 5. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Wapi usalama wa taifa?
   
 6. Jagarld

  Jagarld JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,532
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Siku hizi simba anaweza akawa na huruma kuzidi binadam.
   
 7. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mfumo wa mauaji unapoasisiwa unajenga usugu kwa watu na ndio mwanzo wa watu kujichukulia hatua mkononi. najua angekuwa aliyeuawa ni polisi tungekuwa tayari tumesikia watu kadhaa wamekamatwa, kwa kuwa ni maskini raia unaweza usisikie chochote hadi mwisho wa dunia
   
 8. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Wasi wasi wangu ili polisi waweze kuwakamata wahusika lazima rais atoe agizo na wakati fulani mpaka atume watu kutoka ofisi yake, chukulia mfano wa kifo cha mwenyekiti wa halmashauri ya ya Rungwe, kamanda barlow - mwanza na wengine wengi. je kwa huyu muumini wa watu asiye na hatia je kweli polisi watasimamia? ktk maana ya kutoa fursa na nyezo zote zinazohitajika kuweza kuwatia hatiani wahusika? kazi ipo hapo!!!!
   
 9. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Wanapeleleza kupata taarifa za kiinteligensia kuzuia mikutano ya CHADEMA.
   
 10. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha sana,pumzika kwa amani binti, poleni wafiwa
   
 11. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha sana kwa kweli. R. I. P Eliza.
   
 12. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  oh!na hivi sio RPC ,wala wauwaji hawatapatikana !mbona tumefika hapa jamani!tanzania inaenda wapi yailahi!
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Watu wanaangalia sana sinema za kinaijeria na kujaribu kuiga matukio....RIP Eliza
   
 14. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  r.i.p bi eliza
  binadamu tunageuza roho zetu kuwa jiwe!
   
 15. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  speechless
   
 16. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #16
  Nov 1, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Ni rahici sana kwa polisi ku-trace wauaji kupitia cimu ya marehemu ambayo wauaji waliondoka nayo.. Sema Polisi wetu mpaka kuwe na msukumo au influence toka juu..
   
 17. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  siku hizi inteligensia haifanyi kazi?
   
 18. awp

  awp JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  inatia huzuni sana Rest In Peace Elizabeth
   
 19. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #19
  Nov 1, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  sio jambo la kushangaza ..kama mbunge alipigwa na wezi karibu na ikulu sie wananchi wa kawaida tutegemee nini?
   
 20. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #20
  Nov 1, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160

  kwani hiyo ilikuwa M4C??
   
Loading...