Gradutes na wasomi wa IT naona kama mmelala sana.. fursa nyingi sana hii .com era

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,526
habari wadau.

najua humu kuna wataalamu wengi wa Information technology...

na hii ni digital era...internet imerahisisha mambo ndio maana kina facebook wakatajirika...

mtu kama uber tax yeye ametumia utaalamu wake wa IT na kufanya biashara ya tax dunia nzima bila kuwa na gari yake hata moja.. anatumia magari ya watu kuwadalalia na wateja na yeye kupiga hela huku hata oil hajui inauzwa bei gani..

kuna mahitaji mengi sana ya IT mitaani kuwanzia mafunzo.. ambayo ni hela pia maana humfundishi bure..

kutengeneza mifumo ya book keeping kwenye maduka, magenge, wauza chips ku keep records zao.. hapo hela nyingi zipo... ukawauzia mfumo kwa bei ndogo na kila mwezi ukawa unawachaji service fee kama 10,000 tu... hawawezi kataa kama mfumo wako unawarahisishia kazi zao

kutengeneza mtandao kama max na jamiiforums yake hapa.. napo naona unapiga hela nyingi za matangazo na adsense..

kutengeneza online tvs... etc...

najiulizaga graduates wa IT na wataalamu wa IT kwa nini wanalia njaa... au kulalamika hawana ajira huku laptops wanazo.. ambao kwa ndio mtaji tosha ukichanganya na ujuzi waliosomea vyuoni??
 
wengi hawana starting point, wanasubiri mwenzao aanzishe jambo wao waendeleze!!!
 
Mkuu ulichoandika kina ukweli, ila kumbuka issue siyo idea tu ya mfumo(software) africa changamoto kubwa siyo kutengeneza hiyo mifumo.. changamoto kubwa iko kwenye soko.. soko bado lina watu wenye uelewa mdogo wa bidhaa zetu sisi software developers. ili utengeneze na upate hela unahitaji investment kubwa sana ya kufanya marketing, kitu ambacho kwa mtu huyo mwenye uwezo wa kumiliki tu laptop ataishia kuwa na bidhaa nzuri ila mfukoni amechoka.

Note:
Haya nazungumza kutokana na uzoefu wangu mwenyewe nina miaka minne sasa na kampuni yangu(IWACHU COMPANY LTD) ya kutengeneza mifumo ya nanma hiyo, nashukuru kwa kiasi naona mafanikio ila changamoto ni kubwa kuliko unavyoona ukiwa nje.
 
Ukiwa ndani ya box ni kazi kuona yaliyopo nje kama system zinatengenezewa sana tatizo watu uelewa wao bado mdogo sana
 
Back
Top Bottom