graduation ya gharimu maisha yake yote..soma hi kwa mnaingia vyuo na mnaograduate | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

graduation ya gharimu maisha yake yote..soma hi kwa mnaingia vyuo na mnaograduate

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mao ze dong, Sep 1, 2012.

 1. Mao ze dong

  Mao ze dong JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Habari zenu wasomi?
  Huwa cku ya graduation inakuwa cku ya furaha bahada ya kumaliza battle ya muda mrefu,migomo,kukusa ela ya msoc,n.k machungu huishia ktk cku hiyo.ILA angalia graduation isije ikakugharimu maisha yako yote,soma ich kisa

  Kijana mmoja aliyekuwa akijiandaa kwa mahafali ya kuhitimu chuo kikuu, kwa
  muda mrefu alikuwa akiitamani gari moja ya kifahari ya kimichezo iliyokuwa
  ikiuzwa katika duka moja la magari, na akijua dhahiri kuwa baba yake ana
  uwezo wa kununua gari hilo na kumpa yeye kama zawadi yake kwa kuhitimu
  masomo vyema, na alimwambia baba yake kuwa hicho ni kitu alichokipenda
  Mno.
  Kadri siku zilivyokuwa zikisogea kuelekea mahafali kijana huyo alisubiri
  kwa hamu kuona dalili za baba yake kumnunulia gari hilo . Siku yasiku
  ikafika na asubuhi ya siku hiyo ya mahafali, baba yake alimwita kwenye
  chumba chake cha kusomea na kumwambia'Najiv unia kuwa na mtoto bora kama
  wewe'na pia akamwambia ni kwa kiwango gani anampenda. Akamkabidhi
  kijifurushi cha zawadi kilichofungwa vema kwenye karatasi safi za kufungia
  zawadi. Akiwa mwenye hamu kubwa lakini akiwa amekatishwa tamaa alifungua
  kifurushi hicho na kukuta ni Biblia nzuri yenye jalada la ngozi na juu yake
  kumeandikwa jina la kijana huyo kwa maandishi nadhifu yaliyonakshiwa(decorated) kwa
  dhahabu. Kwa hasira akamfokea baba yake akisema'Yaani pamoja na pesa zako
  zote
  unanipa biblia?' akatoka hima ndani ya nyumba hiyo na kuiacha
  biblia.
  Miaka mingi ikapita na kijana akawa ni mtu wa mafanikio sana kibiashara.
  Alikuwa na nyumba nzuri na familia bora, lakini akagundua baba yake ni mzee
  sana sasa, na akadhani ni muhimu kwenda kwake... Na alikuwa hajawahi kumuona
  tena toka siku ile ya Mahafali. Kabla mipango yake haijatimia, akapokea
  waraka wa simu ukimtaarifu kuwa baba yake amefariki dunia, na amemrithisha
  kila kitu alichokuwa nacho kijana wake wa pekee. Hivyo alitakiwa kurudi
  nyumbani haraka kusimamia mali za
  babayake.
  Alipofika nyumbani kwa baba yake , alipata uchungu na majuto ya hali ya juu
  rohoni. Akaanza kupekua baadhi ya nyaraka muhimu za baba yake ndipo!
  alipoikuta ile biblia ikiwa vile vile kama alivyoiacha miaka kadhaa nyuma.
  Huku akilia alifungua kurasa za biblia. Baba yake kwa umakini mkubwa
  alipigia mistari maneno yaliyopo katika Mathayo 7:11, yanayosema'basi
  ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema,je! Si
  zaidi sana Baba yenu aliye Mbinguni atawapa mema wao
  wamwombao?. Wakati akisoma maneno hayo, funguo za gari zikadondoka kutoka
  katika kurasa za mwisho zabiblia. Ikiwa na jina pamoja na alama ya
  lile duka la kuuza magari ya kifahari ya kimichezo aliyokuwa akiyapenda sana . Kukiwa na tarehe ile ya siku yake ya mahafali huku imeandikwa ...
  IMELIPIWA PESA KAMILI.

  Usipoteze ulichonacho kwa kutamani
  usichonacho: Lakini kumbuka ulichonacho sasa ni moja kati ya vitu ulivyo
  vitamani huko siku za nyuma. IKIWA ZAWADI UPEWAYO HAIJAFUNGWA KWA KADRI
  UTAKAVYO, NI KWA SABABU HIVYO NDIVYO HALI BORA KABISA YA UFUNGWAJI WAKE
  ULIOPATIKANA! SIKU ZOTE SHUKURU VITU VIDOGO: KWANI HUWA NA VITU VINGINE
  NDANI YAKE!
   
 2. sop sop

  sop sop JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 650
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  daaaaaaah
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Ujumbe mzuri tushukuru kwa yote!
   
 4. M

  Microsoft JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 207
  Trophy Points: 60
  daaaaah aixeeee !!!!
   
 5. A

  Apex JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 429
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yes kaka poa xana.
   
 6. Upcoming

  Upcoming Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Mungu tusamehe!!
   
 7. N

  NIMEKIMBIA CCM Senior Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  asante,
  zawadi ni zawadi tu
   
 8. Mao ze dong

  Mao ze dong JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  duh,design ndo umeokota izo funguo,maana ulivyoshangaa
   
 9. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Somo zuri. Wengine nao wazingatie! Nani kama BABA?
   
 10. QUALIFIED

  QUALIFIED JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 13, 2012
  Messages: 747
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  kweli uamuzi wa haraka hakunaga kitu mkuu umetisha
   
 11. siansakala

  siansakala Member

  #11
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wana art utawajua tu humu
   
 12. Z

  Ze Blessed Senior Member

  #12
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umetisha mkuu, thanx
   
 13. s

  sugi JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  C mchezo,dogo alikuwa na haraka kupita upesi!
   
 14. Mao ze dong

  Mao ze dong JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  una maana gani?maana kuchonga ni art,kupaka rang ni art,kuchora ni art nk lakini kuandika sio art
  tiririka
   
 15. E

  Eselo Member

  #15
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we must thanx for everthing
   
 16. Sauli

  Sauli JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 45
  hii umetranslate mkuu, tunaijua
   
 17. Mao ze dong

  Mao ze dong JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  sema unaijua coz kuna wengine walikua hawaijui na ni somo zur kwa wote
   
 18. Wkaijage

  Wkaijage Senior Member

  #18
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mwambye afunguke,
   
 19. M

  Mchokozi JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe peke yako acha kutusemea mimi siijui, asant ujumbe mzuri sana
   
 20. piper

  piper JF-Expert Member

  #20
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Thnx kwa ujumbe mzuri
   
Loading...