Graduates wengi mkiweka aibu na uoga pembeni, basi mtaani mnaishi

Naungana na mtoa mada kwenye kukimbia mji au mtaa wa nyumbani ili kufanya yako kwa uhuru maana hata mimi imenisaidia hio watu hawatakiwi kujua unapambanaje na hata mambo ya kuji expose kwenye mitandao ya kikuda unayaweka kando.
Mitandao ya kikuda ni ipi mkuu ?
 
Aibu na Uoga ni janga kubwa sana. Asikuambie mtu, mtu asikuambia mimi sina mtaji ila ukweli ni Aibu na Uoga.

Kuna Mtumishi mmoja Baba yake na Mkurugenzi wa Jamiiforums aliwahi tuambia mafanikio huanza pale Uoga na Aibu zinapoondoka

Tuna hivi vitu moyoni.

1.Wazazi watanielewa kweli kijana wao mwenye Degree?

2.Hivi Shemeji yangu akisiki itakuwaje?

3.Hivi Mchumba wangu atanielewa kweli kwamba ni mimi niliyekuwa Chuo?

4.Marafiki zangu watanielewa kweli?

5. Majirani vipi?

Combination ya hivyo vyote humfanya mtu aone bora akae tu kisingizio kiwe sina mtaji

Unaondoaje AIBU na UOGA?

1. Jitoe ufahamu kabisa, weka pamba masikioni hapa na pale ambapo inafikia stage wanakuona kama unerukwa na akili ila wewe na Mungu wako ndio mnajua unacho kifanya.

Hii hatua ni ngumu sana kujitoa ufahamu sio mchezo manake inabidi kweli uwe na roho ya Chuma au Roho ngumu sana.

2. Hama nenda mbali na wanako kujua. Kama home ni Korogwe pale na wanakujua ulikuwa Chuo kikuu basi nenda Karatu Arusha anza makazi pale fanya chochote hata kuuza vocha na sigara na karanga.

Hii ni njia nzuri sana manake unakuwa mbali sana na unakuwa kivyako vyako au na mshikaji wako na mnafanya mambo.

3. Usijaribu kumshirikisha mtu yoyote yule hata Wazazi wako kwamba unataka kufanya nini au unafanya nini bali waje kujua wenyewe baadae sana.

Kitendo cha kuwaambia Wazazi au Ndugu na Jamaa na Marafiki kwamba kwa sasa nataka nifungue kibanda cha kuuza Vocha wengi hawatakuelewa na watakukatisha tamaa balaaa.

Hii inachangiwa na imani kwamba Chuo kikuu ni ni levo tofauti.

4. Jitenge na ma-met zako au Marafiki walio na kazi watakutia Uoga zaidi manake ukiwa unawaona wanatokea kazini utaumia zaidi.

5. Washikaji na ndugu na Jamaa wakiwa wanakupigia pigia simu wewe wajibu in short una kibarua unafanya sehemu. Ili kukata mazungumzo manake wakipiga ukaawambia unauza Vocha Dah, hawatakuelewa kabisa kabisa.

Jitahidi kuwakatisha na wajibu in short tu.

MWISHO
Achana na kwamba una Degree hata ikibidi watu wengi waambie hujaenda shule au uliishia tuu Form four.

Ondoa Aibu na Uoga wacha watu wakuone kama umechanganyikiwa, wacha wakuseme, wacha wakucheke, wacha wakukebehi ila mwisho wa siku unajua unacho kifanya.

Kwa sasa Naishia hapa.

MAFANIKIO HUANZA PALE TU AIBU NA UOGA VINAPO TOWEKA
Umeongea ukweli mtupu sana humu. Ni wazi vijana wengi tunaishi kwa matumaini na hii inatokana na jamii tulizolelewa nazo ambazo nyingi zinaamini ukisoma basi mafanikio yatakufuata nyuma, kitu ambacho kwa miaka ya karibuni kimekuwa hakitekelezeki. Ni wakati sasa vijana tusahau kuwa tuliwahi vaa majoho na kuudhuria mihadhara ambayo ilitupa matumaini makubwa juu ya maisha baada ya chuo.

Vijana tunakwama wapi ? Kwa nini tunakosa ubunifu na kila mmoja kutaka auze nguo, mikoba, mashuka na simu ? Je nani atamsupport mwenzake ?
 
Kwenye ubunifu ndiyo shida. Kuna mwanangu nilimpa idea tena inasolve tatizo. Akanijibu kwa nini tusifuge kuku?
Yaani tunapenda vinavyofanywa tu hatuwezi vipya
 
Kwenye ubunifu ndiyo shida. Kuna mwanangu nilimpa idea tena inasolve tatizo. Akanijibu kwa nini tusifuge kuku?
Yaani tunapenda vinavyofanywa tu hatuwezi vipya
Tatizo kubwa ni kwamba tunataka kufanya vitu vinavyoendana na hadhi fulani pasipo kuangalia maslahi. Ndio maana ni rahisi kuona graduates wenye vidgree waliojiajiri basi wakifabya biashara online, wakiuza simu, wakiuza mikoba, wakiuza nguo za kiume na sasa wakiingia kichwa kichwa kwenye kilimo wakati kuna biashara au ideas ndogo ndogo mtu akizifanyia kazi zinaweza kumpa faida kubwa na kuwa na mzunguko mkubwa wa hela ukilinganisha na hizo.
 
Hata hiyo ya kuuza vitu online ni Idea nzuri sana mkuu.
 
Niliwahi kuishi maeneo flani,tajiri mkubwa wa lile eneo alitajirika kwa kuanza na biashara ya kuuza vitumbua,alikuwa anatembeza mkono kwa mkono nyumba kwa nyumba,alipofanikiwa akaendeleza mambo mengine,maduka,hoteli n.k.Baada ya miaka kadhaa nilikuwa kwenye mkoa mwingine nikamshawishi mtu mmoja naye aanzie kwenye biashara hiyo kwani alikuwa hana mtaji wa biashara,mpaka leo haongei na mimi anasema nimemdharau sana...
 
Back
Top Bottom