Graduates wa IFM ni wazuri sana kazini

Nimekua nikiajiri graduates kutoka vyuo mbalimbali kwa muda sasa. Navutiwa na utendaji kazi wa graduates wa IFM. Je kwanini hicho chuo akipandishwi kuwa university?
Ila tusifiche na mimi nimekuwa nikichukua mabinti wa IFM several times ni wazuri katika utendaji wao wa kazi.
 
sikubaliani nawe! kwanza ni wezi,pili utamkuta ana-upper second lakini hawana uwezo wa ku-think strategically, ni watu wanaopenda kujikweza sana. hawajui kazi kabisa, they don't want to work under presure .....pia wanapenda sana wapewe chance za kusafiri sana kuliko wengine.

hapo mkuu nakuunga mkono,lakini naona si IFM tu mbona hata pale Muhimbili kuna hii course ya BSc environmental health sciences yaani ni vilaza kinoma.Jamaa wana degree lakini hawajui kazi kabisa halafu ukiangalia ile course syllabus imechakachuliwa na baadhi ya masomo wame split ili yawe mawili kuwezesha kupata maksi za bure.Kuna wawili walikuja intern ofisini kwetu,jamaa hata kuandika proposal hawajui, halafu vibonde ile mbaya lakini cheti kina GPA kubwa.
 
Actually, I hate discussions of this kind. Why don't we sit and discuss and suggest the prospects of our higher education, about how we can improve the level of creativity of our graduate for future shining Tanzania? Who can stand out and vow "I'm a perfect one, I know each and everything about each and everything" ? Who can do that, so that we can challenge him/her? Ok, its my opinion.... I'm from Zanzibar University parsuing BBA (Acc & Fin) 2nd year.
 
By mlimbwende Nimekua nikiajiri graduates kutoka vyuo mbalimbali kwa muda sasa. Navutiwa na utendaji kazi wa graduates wa IFM. Je kwanini hicho chuo akipandishwi kuwa university?

Mhh post yako iko too general je una maana graduates wa kozi zote huwa unawaajiri hapo kazini kwako labda ungespecify ni kozi zipi halafu neno utendaji mzuri wa kazi ni subjective.Kutoa graduates wazuri sio kigezo cha kuipandisha taasisi ya elimu kuwa University.Vilevile huwa unawaajiri katika junior ,middle or senior position au ni mchanganyiko.Hata hivyo hicho sio kitu cha ajabu saaaaaana.Kwa wale wa UDSM, MUHAS, ARDHI,SUA hawana haja ya kuwa wakali kama unajua kazi unajua unajua tu,je na mwanafunzi aliyesoma Oracle University kwa mambo ya IT nae tusemeje! Hata hivyo hongera mlimbwende kwa kutoa mrejesho kwa hayo unayojionea.Kama ulitoa post ukiwa hauko biased saaaaaaaaaaaafi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom